Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Haki yangu kikatiba ya kushawishi/hamasisha wamuongezee muda Rais Magufuli

Status
Not open for further replies.

JERUSALEM 2006

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Posts
527
Reaction score
596
5G3TVR.png

1. Katiba ya Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa Taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tarehe 16 Februari 2020 nilianzisha uzi unaosema "KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFULI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18 (UHURU WA MAONI) , ibara ya19 ( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo Jamii Forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri Sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha Katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za wa Tanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,

KAULI MBIO YETU NI.

"H.E President Magufuli is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuli ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"

MWISHO

Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. Situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za Nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya Katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
 
Upvote 3
Sasa hayo ya msinga ni according to who? Says who? Wewe???

Ok, mimi ninabaki na langu moja, wewe baki na lakk la msingi

mkuu hakuna cha according to who, jamaa anavunja sheria wazi wazi hamwez hata kupepesa macho kusema haya yakuongezewa mwaka mnaona yana tija ? mna matatizo gani ??
 
1. Katiba ya Jamuhuri wa muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 na marekebisho yake ya 30th April 2000 yananipa haki zote kama raia halali wa taifa la Tanzania kuwa na mawazo huru juu ya jambo lolote ambalo halivunji sheria za nchi yetu.

Mimi kama Mtanzania tar.16/02/2020 nilianzisha uzi unaosema " KARIBU TUJIUNGE NA KUNDI LA MAGUFURI TENA 2025" na mjadala katika kundi hili ulikuwa unaendelea. Kwa bahata mbaya sana.

2. Katiba ya jamhuri ya Tanzania ( 1977) kuanzia ibara ya18(UHURU WA MAONI) , ibara ya19( UHURU WA MTU KUSHIRIKIANA NA MTU MWINGINE) kwa pamoja zinasema

Ibara 18.1 Bila kuathiri sheria za nchi, kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake,na kutafuta,kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru mawasilano yake kutoingiliwa kati.

Naomba nielezee ibara hii ya 18.1; ni kwamba nina uhuru wa kutoa mawazo yangu yoyote, katika chombo chochote ikiwemo jamii forums, bila kuingiliwa na yeyote.

Ibara 20.1 Kila mtu anastahili kuwa Huru, bila ya kuathiri sheria za Nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani, kuchanyika, na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama au mashirika yaliyo anzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo.

Nia yangu ni thabiti, ni kuanzisha mchakato wa kubadirisha katiba kwa kukusanya signatures zaidi ya million tano za waTanzania ili kuweza kukidhi matakwa ya kikatiba ya kumuongezea angalau muhala mwengine Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli,


KAULI MBIO YETU NI.
"H.E President Magufuri is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuri ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine chochote"


MWISHO;
Kama nilivyo quote vipengele vya katiba, basi naomba mawazo yangu yaheshimiwe. situkana, sijapanga kuua, wala sija panga kuvunja sheria za nchi, ninafuata taratibu zote ili kubarisha vipengere vya katiba ambayo siyo Msaafu wala siyo Bibilia.
Nchi hii bwana,wanaohamasisha uvunjaji wa katiba kwa mtu fulani kujiongezea muda hakuna anayewabugudhi Ila wanaohamasisha kuandikwa kwa katiba mpya,katiba itakayounda institutions imara za nchi yetu na zinazotoa haki sawa kwa kila mtanzania wanakamatwa.sasa najua why watu huwa wanajilipua
 
KAULI MBIO YETU NI.
"H.E President Magufuri is too valuable to retire, Tanzanians needs him now more than ever" " Mhe, Rais Magufuri ni wathamani sana kustaafu, Watanzania wanamuhitaji sasa kuliko kipindi kingine...

Valuable” kivipi?
Emu elezea hapo “Tanzania needs him”?

Ukitoa hoja zenye mantiki, labda unaweza pata watu wa kukuunga mkono, angalau kwa maandishi.
 
Nashawishi ili tubadirishe katiba ya sasa inayomnyima haki ya kuendelea na nngwe ya tatu Mhe. Rais.

So sivunji katiba, ila nashawishi ili tubadili katiba
Hivi askofu Mwamakula kakamatwa kwa kosa gani eti?
 
JJB,
Ngoja nikupe ushauri kwa sababu huna uzoefu wa kutosha humu JF kukufanya uanze kuwa mbishi.

Soma kwa makini ulichoandikiwa kwenye bandiko #135 ujaribu kuelewa kilichoandikwa hapo.

Na sio lazima ujibu kila bandiko ulilowekewa, lakini soma na ujifunze kuelewa kilichoandikwa badala ya kurukia tu na kujibu. Kufanya hivyo kunakufunua na kuonyesha mapungufu makubwa uliyonayo, hata katika mada hii unayoitetea.
 
Nchi hii bwana,wanaohamasisha uvunjaji wa katiba kwa mtu fulani kujiongezea muda hakuna anayewabugudhi Ila wanaohamasisha kuandikwa kwa katiba mpya,katiba itakayounda institutions imara za nchi yetu na zinazotoa haki sawa kwa kila mtanzania wanakamatwa.sasa najua why watu huwa wanajilipua

Hivi wewe nani kavunja katiba?

Nipe Ibala ipi ya Katiba imevunjwa kwa mimi kutaka Kipengele fulani cha Katiba kibadilike?

Usiongee manno matupu, ongea with facts and references
 
Taasisi imara duniani hazitegemei watu kama tanzaniaj inavyomtegemea kichaa wake.
Mfano israel kuna maandamano ya muda mrefu kwa sababu PM amenunua nyumba kwa kinachodaiwa rushwa.
MAGUFULI alinunua nyumba za NIC akiwa wazir ulishawahi sikia zikitajwa popote?
Aliwauzia nyumba za umma mahawala zake kina kajala wa kebys ambao hawakuwa watumishi ulishawahi kusikia akitaja popote?
Yeye alighiribu WAKULIMA wa KOROSHO huko kusini aliadhibiwa na mamlaka yyte?
Anatapanya peas za umma bila hata kulishirikisha bunge hapo kuna taasisi au kuna mtu?
Soma vizuri uelewa maana ya separation of power checks and balance. Ukikuta hayo matawi yanaingiliana hapo hakuna taasisi imara.
WALAANIWE WAMTEGEMEAO BINAADAM

Nani kakudanganya taasisi Imara hazitegemei watu??

Nani anaunda hizo taasisi, mizimu??
Watu Imara ndio wanao unda taasisi imara, ukiwa na baba kichaa nyumbani lazima na watoto watakuwa vichaa.

Kwa hiyo hatuwezi tu kuweka yeyote awe Rais, ni lazima tuwe na mtu Mzalendo kama Rais Magufuli.

Kipi ji kigumu kuelewa??


Kwa hiyo ulitaka na sisi tuwe Kama Israel?? Eti kwa kuwa kuna porojo mtaani basi watu wakaandamane?

Please!!!!
 
Hivi wewe nani kavunja katiba?

Nipe Ibala ipi ya Katiba imevunjwa kwa mimi kutaka Kipengele fulani cha Katiba kibadilike?

Usiongee manno matupu, ongea with facts and references
Pole Sana,
 
"Or you just insensible"?

Wewe jifunze hiyo lugha kabla ya kujianika utupu wako.

Idiot.

Kama hujaelewa chukuwa dictionary usome, huna sababu ya kutukana.

Au umeongezeka nn baada ya kutukana?
 
Kama hujaelewa chukuwa dictionary usome, huna sababu ya kutukana.

Au umeongezeka nn baada ya kutukana?
Wewe unaniuliza kama najua maana ya "contradicting" wakati wewe mwenyewe hiyo lugha kwako ni mgogoro.

Kuandika sentensi ilyonyooka tu umeshindwa.

Acha ujinga.
 
Ok magufuli kaongeza..je ao maraisi wengine watakao kuja unazani awatatak kuongeza nao afu ukute ni wala rusha. Fikiria future ya taifa mkuu!

Wakitaka kuongeza wao au ni wananchi ndiyo watawataka??

Hivi, kwa kuwa katiba inasema urais mwisho ni 2 terms then mnataka hapa kusiwe na discussion??

Mbona Ubunge na Udiwani hauna Limit? Je? Ni kigezo gani kilitumika kutokuweka limit kwenye Ubunge lakini kikaweka limit kwenye Urais?

Je, Kwa nini wananchi wenyewe wasipewe mamlaka ya kuamua kama kuwe na ukomo kupitia sanduku la Kura? Hii nchi si ni ya vyama vingi? Kwani ni utawala wa kifamle?

Kwa nini wananchi wasiamue limit ya mtu kupitia sanduku la kura?

Huu ndo mjadala ninaoutaka sio matusi
 
Nani kakudanganya taasisi Imara hazitegemei watu??

Nani anaunda hizo taasisi, mizimu??
Watu Imara ndio wanao unda taasisi imara, ukiwa na baba kichaa nyumbani lazima na watoto watakuwa vichaa.

Kwa hiyo hatuwezi tu kuweka yeyote awe Rais, ni lazima tuwe na mtu Mzalendo kama Rais Magufuli.

Kipi ji kigumu kuelewa??


Kwa hiyo ulitaka na sisi tuwe Kama Israel?? Eti kwa kuwa kuna porojo mtaani basi watu wakaandamane?

Please!!!!
Taasisi imara hazitegemei watu,mfano huyo magufuli unayemtetea is so weak,kinachompa maguvu ni power iliyowekwa kwenye taasisi ya urais na katiba.ila nje ya hiyo taasisi hata mie namtoa kwa KO in Just 3 minutes
 
Anachofanya askofu na unachofanya wewe Wala havina tofauti,Ila tuna shangaa wewe hukamatwi

Askofu kahamasisha maandamano.
Mimi, nimeunda TELEGRAM group kwa ajili ya kufuata taratibu zote za kisheria katika kufanya amendment za Katiba.

Kosa langu liko wapi?
 
Valuable” kivipi?
Emu elezea hapo “Tanzania needs him”?

Ukitoa hoja zenye mantiki, labda unaweza pata watu wa kukuunga mkono, angalau kwa maandishi.

Valuable kwa maana ni wathamani sana, tumekaa zaidi ya miaka 30 tangu baba wa Taifa ndio tukampa Rais Magufuli, hatuwezi kukubali kukaa kipindi kirefu kama hicho wakati Rais bado yupo.

Sina haja ya kumuelezea kwa chochote, amefanya mambo mengi in 5 years kuliko mtu yeyote kwa terms zao zate walizokaa madarakani.

Just mention anything, amegusa maeneo yote ya nchi.

Mnachotaka ni nini.

Ndio maana ninasema we need him now more than ever
 
Nchi hii bwana,waohamasisha uvunjaji wa katiba kwa mtu fulani kujiongezea muda hakuna anayewabugudhi Ila wanaohamasisha kuandikwa kwa katiba mpya,katiba itakayounda institutions imara za nchi yetu na zinazotoa haki sawa kwa kila mtanzania wanakamatwa.sasa najua why watu huwa wanajilipua

Anachokifanya Mh. Raisi ndio kimepelekea azma hii.

1.Kuweka umeme zaidi ya vijiji elfu 10 ndani ya miaka mitano tu, wakati alikuta kuna vijiji 2000 tu vyenye umeme.

2. Kujenga miradi mikubwa ya nishati ikiwemo bwawa la nyerere lenye MW 2115 na mabwawa mengine madogo madogo.

3. Kujenga SG railway kwa rwli ya kati

4. Mtandao wa barabara za rami sasa uko kila mkoa na unaunganisha mikoa yote.

5. Hospitali na vituo vya Afya ndio usiseme.

6. Elimu Bure mashuleni.

Jamani, mambo ni mengi, na yote nimetaja ni maendeleo.

Sasa kama hauoni, na unaona biashara zinazofungwa ila huoni zinazofunguliwa basi unashida kubwa

Unataka “maendeleo” yanayoletwa na mtawala fulani au unataka “maendeleo endelevu”yasiyofungamana na mtawala?

kama ni ya kwanza, basi angalau jifunze kwenye historia ili kuona tatizo lake. Nyerere alitawala kwa miaka 25! na sera ya ujamaa na kujitegemea. Umeona kilichotokea baada ya kuachia ngazi?

kama unataka ya pili, kwa maoni yangu, historia imeonyesha kuwa tunahitaji mipango ya kitaifa sio ilani za vyama + katiba inayowapa wananchi madaraka zaidi (katiba ya warioba ni mwanzo mzuri) na sio hii ya kifalme.
 
kila.la kheri nimesoma hapo naona upo sawa vipengele umeviweka na uheshimiwe.anayetaka kukupinga nayeyey aweke vipengele. je hiso sain lin?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JJB,
Ngoja nikupe ushauri kwa sababu huna uzoefu wa kutosha humu JF kukufanya uanze kuwa mbishi.

Soma kwa makini ulichoandikiwa kwenye bandiko #135 ujaribu kuelewa kilichoandikwa hapo.

Na sio lazima ujibu kila bandiko ulilowekewa, lakini soma na ujifunze kuelewa kilichoandikwa badala ya kurukia tu na kujibu. Kufanya hivyo kunakufunua na kuonyesha mapungufu makubwa uliyonayo, hata katika mada hii unayoitetea.

Wewe uzoefu unao? Tumeanza kutishiana uzoefu tena?

Je! Hoja yangu ni mufilisi kama zenu?
 
ukiwa na baba kichaa nyumbani lazima na watoto watakuwa vichaa.
Seems you're beyond repair!
ni lazima tuwe na mtu Mzalendo kama Rais Magufuli.
Umejitwisha jukumu ambalo huna uwezo nalo.

That's all I can say to you.

Huna uwezo wa kushawishi?

Lugha hakuna, ufahamu wa jambo unalotetea huna; utategemea kupata watu wa kukuunga mkono huko kwenye mitandao unakowaita waje muweke shinikizo la kubadili katiba?

Tafuta msaada mkuu, kama kweli unayo 'commitment' ya kazi unayotaka kuitimiza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom