Hakika Waislamu wana gharama na taratibu rahisi sana katika masuala ya ndoa

Hakika Waislamu wana gharama na taratibu rahisi sana katika masuala ya ndoa

Chief Wingia

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2013
Posts
2,653
Reaction score
4,744
Asalamu alaykum wanajukwaa pendwa la MMU natumai wote mubuheri wa afya.

Awali ya yote niwape hongera za dhati Waislam kwa utaratibu mzuri kuanzia kwenye posa yaani kuchumbia, ndoa na sherehe ya ndoa. Nimeshuhudia haya kwa majirani, marafiki, jamaa na wafanyakazi wenzangu.

Tukianza na posa/kuchumbia gharama inarange elfu 20 hadi 50 hapa hamna mbwembwe za sherehe wala nini. Nina ushuhuda kwa jamaa yangu aliyeposa kwa elfu 30 tu na posa ikakubaliwa.

Kuhusu mahari hawa wenzetu bint muolewaji ndio anaetamka gharama ya mahari yake na mara nyingi gharama ni kati ya laki tano hadi milioni moja, na hapo ukiona inazidigi hadi milioni ujue ni kwasabubu ya vitu vya kimila na kitamaduni vya familia/kabila la huyo bint, vitu kama fimbo na kofia ya babu ama vitenge vya bibi n.k.

Ila sitosahau kuna mfanyakazi mwenzetu hapa alioa kwa mahari ya "MASAHAFU" yaani kile kitabu cha KURAANI chenye gharama ya elfu 25.

Ukija kwenye sherehe ya ndoa sasa kusherekea ni siku ile ya ndoa tu hakuna mlolongo wa michango na masherehe
 
Ila pia kuachana ni rahisi.

Wakristo mpaka kupeana talaka ni shughuli pevu.
Mkuu ndoa nyingi za Kikristo zimeshakufa zamani na wengi wao wanaishi kwenye ndoa kwa mateso kwa ugumu wa kipengele hiki cha talaka.

Hivyo basi kwenye hotuba ya ndoa miongoni mwa maneno ni haya OANENI KWA HERI NA KAMA ITATOKEA MMEKOSEANA NA KUFIKIA KUACHANA BASI PIA MUACHANE KWAHERI.

Hii inamanisha katika Uislamu hakuna kugandana kama ruba.
 
Na ni rahisi kuivunja vilevile gentleman contract
 
Mkuu swala la gharama ni mipango baina ya familia mbili, waoaji na waolewaji.

Nina ushuhuda wa mshikaji wangu alioa ndoa ya kikristo kabsa na gharama yake haikuzidi hata 2ml (mahali ,posa na sherehe)

Gharama hua zinakua kubwa kwa kutaka show off. So kaa ukijua dini sio tatzo mkuu fikiria tu nje ya box.
 
Hili swala nilishawaambia na nnawambia tena hapa, Hakuna dini hata moja ndoa inakua na gharama, gharama mnazosemeaga kila leo ni zile za sherehe, hata Waikristo ndoa ni jambo jepesi kwao, Tofautusheni Ndoa na Sherehe, hivi ni vitu viwili tofauti kabisa, Ukimaliza ndoa kule mnakokuita kanisani mnaweza sepa sass zile mbwembwe baada ya Kanisani sio ndoa na wala hazina
 
Back
Top Bottom