Hakukuwa na sababu ya Profesa Mkenda kuzungumza aliyoyazungumza hadharani. Kiongozi ni kuwa na Kifua na Uvumilivu

Kaonyesha umma wa Wanzania kuwa Rais amekuwa ni wa watu fulani tu.
Ikiwa waziri ni ngumu kumuona, usitegemee raia wa kawaida atakufikiria kwa lolote.
Kama mteule wake anafanyiwa hivyo basi tujue nchi haiko salama.
 
Pale jamaa mwenye elimu ya hapa na pale anapompa lekcha mtu mwenye digrii nne, mwalimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini na nje ya nchi,waziri wa elimu hapa Tanzania.
Kwa hiyo wewe kwa akili yako hiyo hiyo uliyonayo unaamini kuwa mtu akiwa Profesa anakuwa kama Mungu mtu? Anakuwa Alfa na omega? Anakuwa na akili nyingi kupita wote ndani ya Taifa na hata nje? Anakuwa hawezi kukosea? Anakuwa malaika atembeaye Duniani? Anakuwa mtakatifu asiyekosea wala kutakiwa kusahihishwa? Anakuwa wa kuabudiwa na kupewa sifa?
 
..Prof.Mkenda hakukosea ktk kauli yake.

..Nilichogundua ni kwamba Prof ni mmoja kati ya mawaziri wanaopima kauli zao kabla hawajazungumza.

..hebu kaleta hotuba ya Prof ili wasomaji waone kama kuna ulazima wa makelele yote haya.
Kiuongozi alichokifanya Mheshimiwa Waziri siyo sahihi hata kidogo
 
Kiuongozi alichokifanya Mheshimiwa Waziri siyo sahihi hata kidogo

..hakukosea chochote kile.

..nenda kasikilize hotuba yake.

..infact Prof amemzungumzia Rais vizuri sana.

..tatizo CCM mmezoea kupotosha sasa imefika wakati Watanzania wanaamini jambo la uongo kuliko ukweli.

..hili ni tatizo mmelilea CCM sasa imefika mahali Watanzania wamekuwa wagumu kufanya tafakuri za kina, na wepesi mno kupotoshwa.
 
Kati yako wewe na Profesa Mkenda unafikiri akiongea kwenye hadhara nani atasikilizwa?

Profesa kaongea ukweli na ndio hali aliyopitia na huyo mama yako alikuwepo pale kasikiliza hakuongea chochote kama hizi sarakasi unazoleta hapa.

Kwa kukusaidia sio kila kitu kinaongelewa kwenye simu kama unavyodhani, utatoaje wasilisho lenye takwimu ,michoro, jedwali kwenye simu ?

Sasa nashangaa wabeba mabango kama wewe ndio mnaumizwa kwa waziri kuongea ukweli alipozuiliwa kutoa wasilisho lake.

Taaluma na UCHAWA havikai sehemu moja .

Profesa Mkenda apongezwe na mchawa na vidampa wapuuzwe.
 
Najua huna uwezo wa kujibu hoja zangu.
Wewe mpuuzi kweli kweli yaani naianzishe kampuni inayojiendesha kwa faida halafu nisijue maana ya kampuni, na hiyo ndiyo unaita hoja? Nimeshapata jibu kwa nini hupati uteuzi,watu wamekufanyia vetting wakaona hutoshi,kwa akili hizi hata mimi siwezi kukupa ajira.
 
Uko sahihi kabisa imagine huyu kapuku Lucas Mwashambwa anayejigamba ni msomi wa chuo kikuu lakini ameweza kupotosha kiasi hiki, sasa hao wa form IV iatakuwaje,CCM ina hazina kubwa sana ya wapumbavu na majuha kama huyu mpotoshaji na chawa wa Samia Lucas Mwashambwa.
 
Kiuongozi alichokifanya Mheshimiwa Waziri siyo sahihi hata kidogo
Yuko sahihi 100% ila akili yako ya sisimizi imeshindwa kuelewa alichosema ndiyo umekuja na conclusion ya kijinga hivi. Baba yako hiyo hela aliyokupelekea shule bora angefugia nguruwe ingemlipa.
 
Sasa Nini hoja ya huyu Waziri kulalamika kushindwa kumfikia Mama...!

Hana namba yake!?
 
Nimekuwa nasisitiza hili hapa mara kadhaa lakini mtoa maada kajitoa akili.

..Mkuu hii habari imepotoshwa.

..Na tatizo letu vijana hawana muda wa kuhakiki taarifa wanazopewa.

..Mkenda alisema ilikuwa vigumu kwa yeye na timu yake kupata muda wa kwenda kufanya presentation kwa Raisi.

..Na sababu zake ni Raisi kuwa na ratiba ambayo ni tight sio kwamba Raisi hataki kuonana na Waziri.

..Prof pia akaeleza kwamba yeye na timu yake walipangiwa masaa mawili kufanya presentation.

..Lakini walipomueleza Raisi kwamba they have been given two hours, Raisi akasema anawapa siku nzima ya kuwa naye kuwasilisha hoja zao. Na baada ya hapo Raisi aliwapa commitmet kuwa atatekeleza ushauri waliompa.

..Prof hakulaumu wala kumlalamikia yeyote yule katika hotuba yake. In fact alimzungumzia vizuri sana Rais Mama Samia.
 
Kuna wasaidizi wa rais walikuwa wanamnyima nafasi ya kuongea na rais. Hata alipokuwa anatoa hotuba walimpelekea kimemo kumwambia atoe hotuba asitoe porojo, akasema hii ndiyo hotuba naitoa.

Kuna katibu wa rais (si katibu mkuu kiongozi, katibu wa rais) anamu isolate rais kutoka kwa mawaziri wake na watendaji wwngine wa serikali.

Hii habari inajulikana muda mrefu tu kabla hata ya malalamiko ya Mkenda.
 
Siyo kweli na acha upotoshaji wako hapa wa kusema katibu wa Rais anamtenga na kumuweka mbali Mheshimiwa Rais na Mawaziri wake.
 
Mm niko upande w prof kwakua yuko kwenye baraza l mawaziri je mtendaji w kijiji uko kilosa au tukuyu anaweza kumuona CHURA? Za ndani nikua tangu mwaka umeanza huu 2025 Baraza la mawaziri hawajaa kaa. TAIFA linajiendea tu.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Sasa Nini hoja ya huyu Waziri kulalamika kushindwa kumfikia Mama...!

Hana namba yake!?
Ndio Maana nimesema ya kuwa waziri hakuwa na sababu ya kulalamika juu ya juu ya jambo hilo kwa sababu anazo njia nyingi sana za kuwasiliana na Mheshimiwa Rais ili apate nafasi ya kuonana naye moja kwa moja kwa ajili ya kuwasilisha jambo kama hilo alilokuwa analitaka. Lakini pia kuna vikao vya mawaziri huwa vinafanyika mara kwa mara . Na majuzi juzi tu hapo vilifanyika.
 
Mm niko upande w prof kwakua yuko kwenye baraza l mawaziri je mtendaji w kijiji uko kilosa au tukuyu anaweza kumuona CHURA? Za ndani nikua tangu mwaka umeanza huu 2025 Baraza la mawaziri hawajaa kaa. TAIFA linajiendea tu.
KAZI ni kipimo cha UTU
Unafahamu mara ya mwisho lilikaa lini na linatakiwa likae kila baada ya muda gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…