Hakukuwa na sababu ya Profesa Mkenda kuzungumza aliyoyazungumza hadharani. Kiongozi ni kuwa na Kifua na Uvumilivu

Hakukuwa na sababu ya Profesa Mkenda kuzungumza aliyoyazungumza hadharani. Kiongozi ni kuwa na Kifua na Uvumilivu

Muulize mkenda, alafu umuulize kama inawezekana kwanini anatudanganya watanzania.
Embu nijibu kuwa unafikiri Waziri anaweza kushindwa kumpigia Simu RAIS ? Unakumbuka hotuba ya RAIS ambayo alisema namna anavyopogiwa simu na Mheshimiwa waziri wa Fedha kuelezwa masuala mbalimbali ya wizara?
 
1738430648950.jpg
 
Ndugu zangu Watanzania,

Sote tumeyasikia maneno na kauli za Waziri wa Elimu Mheshimiwa Profesa Adolph Mkenda akilalamika kuwa alizungushwa kupata nafasi ya kuonana na Mheshimiwa Rais wetu Mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan.

Mimi Mwashambwa nimejiuliza maswali ya je kulikuwa na sababu zipi za kuyaongea hayo masuala hadharani? Yalikuwa na umuhimu upi na sababu zipi? Alishindwa nini kuyaongea faragha alipopata nafasi ya kuongea na kuonana na Mheshimiwa Rais?

Je waziri hana njia nyingine za kuwasiliana na kufikisha ujumbe wake kwa Rais? Je waziri hawezi kuwasilisha jambo hilo kwenye kikao cha Baraza la mawaziri na kutoa dukuduku lake na kero yake ili mambo yazungumzwe na kuonyana humo humo badala ya kuleta hadharani?

Pia soma:
Juu ya Waziri Wa Elimu kuna Naibu Waziri Mkuu, Waziri Mkuu ,Makamu wa Rais kabla ya kumfikia Rais Mwenyewe. Sasa kwanini asingemtumia hata mmoja wapo kati ya hao kupeleka jambo lake na kero yake hiyo?

Hata alipopelekewa kikaratasi mezani kwake kwanini na kulikuwa na sababu gani ya kujibu kwa jeuri kuwa yale aliyokuwa anayaongea yalikuwa ni Sehemu ya hotuba yake? Kwanini alikuwa anaonyesha kana kwamba yupo kwenye mgogoro na wasaidizi wa Rais na sasa anataka kuwachongea na kutunishiana misuli hadharani? Yalikuwa na sababu gani hadi ya kusema kuwa tuliambiwa tuongee kwa saa mbili tu?

Kwanini Waziri ambaye ni Profesa kabisa anakosa kifua na uvumilivu pamoja na subira ya mambo madogo kama hayo? Kama jambo dogo kama hilo linamshinda kuvumilia na kukaa kimya bila kuonyesha hasira zake hadharani,anaweza vipi vumilia mambo makubwa na kukaa nayo mpaka anaingia kaburini? Unapokuwa kiongozi mkubwa ni pamoja na kubeba maumivu na kutunza siri kwa gharama kubwa na Maumivu.

Hivi kama Rais Samia Mama yetu kipenzi asingekuwa na kifua na uvumilivu na kuamua kuzungumza kila kitu hadharani. Unafikiri angezungumza mangapi mazito baada ya kuapishwa kwake kuwa Rais? Au mmesahau ni nini Mkuu wa Majeshi wetu mstaafu Mheshimiwa Jenerali Venance Mabeyo alichokisema na kilichotokea baada ya kifo cha Hayati Mwalimu Daktari John Pombe Joseph Magufuli?

Mmesahau Kauli ya Jenerali Mabeyo kuwa kuna watu walisahau katiba inasema nini na kwamba akawakumbusha Matakwa ya Katiba mara baada ya kufa kwa Rais? Hivi mnaichukuliaje kauli hiyo? Mnaelewa Maana yake? Mnataka niwafungulie mabano ili muelewe?

Je mnafikiri watu hao waliosahau matakwa ya katiba Hawapo hai? Mnafikiri hawapo Tanzania? Mnafikiri hawapo serikalini?? Mnafikiri Mama yetu Mpendwa hawafahamu? Mnafikiri Mama yetu kipenzi hafahamu kilichotokea baada ya kifo cha Hayati? Au mnafikiri amekaa kimya kwa sababu hajui kitu?

Jibu ni kuwa anafahamu kila kitu na ameamua kukaa kimya na kuendelea na kazi kwa sababu anajua maana ya uongozi. anajua maana ya kutunza siri. Anajua Ukubwa ni jalala. Anajua jambo gani linapaswa kuzungumzwa hadharani na lipi halipaswi kuzungumzwa hadharani. Anajua kuna mambo yanapaswa kukaa kifuani na kubakia kama siri mpaka Kifo.

Na huo ndio uongozi. Ndio Ukubwa.Ndio uongozi unavyotaka hivyo kwa kiongozi wa juu kuwa na kifua ,kutunza siri,kuwa na subira, uvumilivu na kujizuia kuongea vitu kwa msukumo wa hasira,jazba, mihemuko na kukurupuka. Kama Rais Samia angetaka kuongea kila kitu hadharani basi Nchi ingesimama. Nasema tena kuwa NCHI ingesimama hii.

Viongozi wetu jifunzeni kuwa na siri,vifua, uvumilivu na subira. Tumieni busara na hekima katika kuzungumza hadharani na chagueni maneno ya kuzungumza mbele ya hadhira. Na ikiwezekana someni hotuba mlizoandaliwa kuliko kutumia hisia bila mantiki kuzungumza na kujikuta mkiharibu na kuleta taswira mbaya kwa jamii .

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Hatuna Rais
 
My humble opinion, na si kwa ubaya.

Kuna uwezekano mkubwa Prof ameongea hayo out of akiwakilisha mawaziri wenzake ambao nao wanakutana na changamoto hiyo hiyo, ila Prof kafanya tu kufikisha ujumbe,, Bi Mkubwa na team yake wajue sasa wananchi tunajua namna anavyofichwa ili aweze timiza majukumu yake.

Hii haina tofauti na Mabeyo alivyosema Magu alivyomwambia in public, japo mengine aliyaficha. Au CDF Nkunda alivyotahadharisha swala la wahamiaji haramu ambao wako kwenye vyombo vya maamuzi.

Si kwamba Bi Mkubwa hana hizo taarifa, ila ni kama watu wanazichezea taarifa hizo bila kufanya chochote.
 
Siyo kweli na acha upotoshaji wako hapa wa kusema katibu wa Rais anamtenga na kumuweka mbali Mheshimiwa Rais na Mawaziri wake.
Katibu wa rais analalamikiwa na watu wengi tu, si kwenye hili la Mkenda tu.

Unabisha?
 
Uwe na adabu na uache kuropoka ropoka hapa kama toto lililokosa malezi ya wazazi wake.
Wewe ni choko mwenye njaa na tamaa nyie ndo mnaofirwa kirahisi kisa mpate teuzi za chama sijui mzaliwa wa wapi hizi kwenu hakuna wanaume wakufunze uvumilivu?
 
Alichoongea yupo sahihi ndio maana Nchi ina ujinga mwingi kwa sababu ninyi msiojua kitu ndio mnaandika andika hovyo na kuamini mnavyoandika mpo sawa..
 
Huyo Mama angekuwa na uvumilivu, Mzee Kibao na kina Soka wangekuwa huko waliko leo hii?

Acha ujinga!!
 
Kama waziri anazungushwa kumuona raisi,Je,kwa mwananchi wa kawaida aliyetokea huko Kolomije itakuwaje?!!!Hii nchi ni ya ajabu sana!!!
 
Embu nijibu kuwa unafikiri Waziri anaweza kushindwa kumpigia Simu RAIS ? Unakumbuka hotuba ya RAIS ambayo alisema namna anavyopogiwa simu na Mheshimiwa waziri wa Fedha kuelezwa masuala mbalimbali ya wizara?
Siwezi kukujibu am just a citizen kijana, and you being a teacher huwezi kuelewa hata ishu za madiwani zikoje, kaa kimya siku ukiteuliwa msemaji wa serikali au CCM popoma unavyofanya sasa.
 
Kama waziri anazungushwa kumuona raisi,Je,kwa mwananchi wa kawaida aliyetokea huko Kolomije itakuwaje?!!!Hii nchi ni ya ajabu sana!!!
Kwa hiyo wewe unataka utoke zako huko kolomijo na kwenda kuonana na Rais moja kwa moja Utafikiri unaingia sokoni? Kwani huko uliko hakuna viongozi? Umepita huko na ikashindakana kusaidiwa? Itakuwaje watanzania zaidi ya million 60 tukitaka kwenda Wote Ikulu kupeleka shida zetu na kuonana na Rais?
 
Kama angenyamaza tungejuaje kama kuna shida hata ofisi nyeti ya serkali waziri ambaye ndiyo mshauri wa rais kuingia kwa kibali? Hii ni insubordination kwa wananchi waliomchagua mbunge.
 
Back
Top Bottom