Kuna huu mkumbo tulionao watu weusi wa kuigana igana mambo hata yasiyo na maana.
Hapa nitazungumzia huu mtindo walionao wazazi wengi kupeleka watoto wao English medium kwa minajiri kwamba wakapate elimu bora.
Inshort hakuna faida yoyote ya kumpeleka mtoto English medium kwa elimu ya bongo anayesoma English medium na anaesoma Changamkeni wote wanakula makapi na uchafu wa mfumo wa elimu ya hapa Tz.
Utofauti mdogo pekee uliopo wa anaesoma English medium na Changamkeni ni kukajua kakiingereza ka hovyo ka kuombea maji na kuita dad na mum basi.
Ila viwango vya ujinga na upumbavu vilivyo athiriwa na mfumo takataka wa elimu ya Tanzania wote vipo sawa baina ya anaesoma English medium na anaesoma Changamkeni.
siyo kweli kwamba wazazi wanawapeleka watoto english medium kwamba ni kuiga au hakuna utofauti kati ya english medium na shule zetu za kayumba. Utofauti ni mkubwa sana ukiachilia mbali maswala ya ada tuangalie faida
1: Shule za english medium kutokana na walimu kuwa wanalipwa vizuri wanakuwa na moyo wa kufundisha na kuwa karibu na maendeleo ya wanafunzi wao. Walimu hawana stress na wanajenga upendo na watoto. Muda mwingi watoto wanasoma na pia kupata muda wa kucheza na kupumzika
2: Hata madhari ya shule nyingi za english medium zinaridhisha sababu unakuta darasa watoto hawazidi 30 hivo ni rahisi kwa mwalimu kujua tabia ya mwanafunzi wake mmoja mmoja na kuweza kumsaidia.
3: Wazazi wanakuwa na amani zaidi wanapokuwa katika kutafuta pesa au mihangaiko yao ya kutafuta riziki mana shule zinakuwa na ulinzi wa kutosha na mazingira ya shule yanaridhisha.
4: Huna haja ya kuahangaika sana na twisheni kwwakuwa walimu wa english medium wanakuwa wanawafatilia sana wanafunzi wao na kuwasiliana pia na wazazi kama kunachangamoto ambayo mtoto atatakiwa kusaidiwa zaidi nyumbani.
5: Mambo ya kuchapana kama vile unataka kuua au unapiga mwizi hakuna hizi shule za english medium na zinajenga mtoto kuipenda shule na ndiyo msingi wa kwanza mzuri kwa mtoto kuipenda shule.
6: Shule hizi zinamjenga mtoto kuwa na confidence kwani lugha ipo juu na uthubutu wa kuongea mbele ya jamii upo kwa kuwa wanakuwa wanajifunza vitu vingi.
huo ni uchache ambapo shule zetu za kayumba walimu wana stress za mishahara, hasira muda wote na anaweza malizia kwa mwanafunzi kumchapa na kumuumiza.
walimu wengi hawana muda wa kufatilia watoto kwani wao wenyewe wanayakwao kichwani , darasa unakuta watoto wengi kiasi hata mwalimu kuweza fatilia kila mwanafunzi haweza.
Mazingira ya shule nayo ni utata hasa chooni na wanafunzi wakati wa mchana wananunua chakula toka kwa wanaoleta maeneo ya shule.
Mtoto wa kayumba inabidi umtafutie masomo ya ziada maana shule ni changamoto kumaliza silabasi.
Kiukweli kayumba zilikuwa zamani wakati tunasoma miaka hiyo ya 80 mpaka angalau 90.