Hakuna faida ya kumpeleka mtoto English Medium (mabasi ya njano)

Hakuna faida ya kumpeleka mtoto English Medium (mabasi ya njano)

Kuna huu mkumbo tulionao watu weusi wa kuigana igana mambo hata yasiyo na maana.

Hapa nitazungumzia huu mtindo walionao wazazi wengi kupeleka watoto wao English medium kwa minajiri kwamba wakapate elimu bora.

Inshort hakuna faida yoyote ya kumpeleka mtoto English medium kwa elimu ya bongo anayesoma English medium na anaesoma Changamkeni wote wanakula makapi na uchafu wa mfumo wa elimu ya hapa Tz.

Utofauti mdogo pekee uliopo wa anaesoma English medium na Changamkeni ni kukajua kakiingereza ka hovyo ka kuombea maji na kuita dad na mum basi.

Ila viwango vya ujinga na upumbavu vilivyo athiriwa na mfumo takataka wa elimu ya Tanzania wote vipo sawa baina ya anaesoma English medium na anaesoma Changamkeni.
siyo kweli kwamba wazazi wanawapeleka watoto english medium kwamba ni kuiga au hakuna utofauti kati ya english medium na shule zetu za kayumba. Utofauti ni mkubwa sana ukiachilia mbali maswala ya ada tuangalie faida

1: Shule za english medium kutokana na walimu kuwa wanalipwa vizuri wanakuwa na moyo wa kufundisha na kuwa karibu na maendeleo ya wanafunzi wao. Walimu hawana stress na wanajenga upendo na watoto. Muda mwingi watoto wanasoma na pia kupata muda wa kucheza na kupumzika

2: Hata madhari ya shule nyingi za english medium zinaridhisha sababu unakuta darasa watoto hawazidi 30 hivo ni rahisi kwa mwalimu kujua tabia ya mwanafunzi wake mmoja mmoja na kuweza kumsaidia.

3: Wazazi wanakuwa na amani zaidi wanapokuwa katika kutafuta pesa au mihangaiko yao ya kutafuta riziki mana shule zinakuwa na ulinzi wa kutosha na mazingira ya shule yanaridhisha.

4: Huna haja ya kuahangaika sana na twisheni kwwakuwa walimu wa english medium wanakuwa wanawafatilia sana wanafunzi wao na kuwasiliana pia na wazazi kama kunachangamoto ambayo mtoto atatakiwa kusaidiwa zaidi nyumbani.


5: Mambo ya kuchapana kama vile unataka kuua au unapiga mwizi hakuna hizi shule za english medium na zinajenga mtoto kuipenda shule na ndiyo msingi wa kwanza mzuri kwa mtoto kuipenda shule.

6: Shule hizi zinamjenga mtoto kuwa na confidence kwani lugha ipo juu na uthubutu wa kuongea mbele ya jamii upo kwa kuwa wanakuwa wanajifunza vitu vingi.
huo ni uchache ambapo shule zetu za kayumba walimu wana stress za mishahara, hasira muda wote na anaweza malizia kwa mwanafunzi kumchapa na kumuumiza.

walimu wengi hawana muda wa kufatilia watoto kwani wao wenyewe wanayakwao kichwani , darasa unakuta watoto wengi kiasi hata mwalimu kuweza fatilia kila mwanafunzi haweza.

Mazingira ya shule nayo ni utata hasa chooni na wanafunzi wakati wa mchana wananunua chakula toka kwa wanaoleta maeneo ya shule.

Mtoto wa kayumba inabidi umtafutie masomo ya ziada maana shule ni changamoto kumaliza silabasi.

Kiukweli kayumba zilikuwa zamani wakati tunasoma miaka hiyo ya 80 mpaka angalau 90.
 
Sema nn January pa motoo......
Ukute ndo Kodi inaisha December hii
Una manyokaa apo om
Bdo bills za maji na umeme
Msosi
Sema nn sis wanaume kupambn kiume tu[emoji109]
Kama una majukumu mazito hpo mbeleni, kipindi hiki weka anasa chini, kama ni wa pombe/totoz jaribu kuokoka kwa muda 😀
 
Private hata ile mbovu kabisa hukuti mwanafunzi anayehitimu elimu yake bila kujua kusoma na kuandika.


Leo ni mwaka 2012 ?

Mbona unaleta post za zamani kutetea hoja ya mwaka 2023
 
Sasa hizo shule ambazo sio ‘English medium’ zenye kutoa utayari wa maisha kwa mtoto ndio hizi za huku mtaani kwetu zenye kuitwa Shule za kata?

Shule zenye walimu 10 na wanafunzi 1500?

Maybe kwanza tuzungumze utayari wa aina gani na kwenye maisha yapi.
Utayari kwa maana kwamba Dunia ya Sasa mtu anatakiwa awe anajua kusoma na kuandika,kuwa na uwezo angarau wa kuuma ulimi hata dkk 3 mzungu au mgeni akija ktk biashara yake,haya yote yanatokea hapo shule ya kata,labda kama mtoto hakujua kilichompeleka.

Zama za mtu kuonekana wa ajabu kisa kasoma English medium zimeshayeyuka,maana hata hizo ajira za uhakika unazoweza kudhani unamhakikishia,zinaanza na malipo ambayo hayaendani na uwekezaji uliofanya.
Connection za michongo ya maana ni kwa wale wenye mianya serikalini na mashirika makubwa na nafasi ni chache,zinawindwa na wanasiasa na viongozi wa juu zaidi.

Miaka 25 ijayo watoto wenye miaka 0-10 Leo,watakuwa kwenye kundi la watu wenye sifa zote za elimu inayoonekana ya ajabu Leo,diploma,degree, masters nk,ila kipi walikuandalia wazazi wako kama backups ndio kitakubeba,angalia mfano Kenya tu hapo utanielewa.
 
Leo ni mwaka 2012 ?

Mbona unaleta post za zamani kutetea hoja ya mwaka 2023
Hakuna kilichobadilika toka wakati huo hali ndiyo inaendelea kuwa tete.





NB:Hao waratibu wa elimu/maafisa elimu wenyewe watoto wao wapo Private halafu mtu anakuambia hakuna tofauti.

Unafikiri watu wanapenda tu kuchezea pesa!
 
Tutafute hela Wazee shule bora za msingi zipo nzuri sana na mtoto akiwa na Msingi mzuri huko mbele hatosumbuka...
 
Najaribu kufikiria tu mtoto wangu wa miaka 7 namna atakavyoweza kwenda shuleni mwenyewe akivuka barabara na kupishana na bodaboda za hapa jijini. Nawaza jinsi wazazi tulivyo bize na mishe zetu na hakuna muda wa kuwapeleka shule. English medium na mabasi ya njano yanatusaidia sana sisj tulio busy na harakati
Yanasaidia sanaa
 
Tafta hela bro...achaa makasiriko,Na pesa za wezako
 
Shida sio English Medium bali gharama zimekua za juu sana, hizo sababu nyingine hazina mashiko sana cha kulalamika hapa ni gharama zao zime ruka sana.
 
Hahah unampeleka mtoto English medium akienda o level pia unampeleka private, advance private halafu anaenda chuo kimoja na coarse Moja na mtoto aliyesomea government akiisikia private tu
Nini chuo kazini je? Wewe umesoma government hujakutana na watu waliosoma private?
Kwani kuna shida yoyote? Mwisho wa siku elimu ya primary ndio msingi wa kila kitu.
 
Back
Top Bottom