Hakuna furaha kwenye uuaji, damu ya binadamu ina roho

Hakuna furaha kwenye uuaji, damu ya binadamu ina roho

Hapana walimdeport kumrudisha kwao. Senator hakuwahi kushitakiwa kabisa na polisi wanadai sio suspect ila private investigator na dereva wa zamani wa senator na yule kijana akiyekuwa deported wanaamini aliyemuua yule mrembo ni senator.
Senator inaelekea alimuua kuficha uhusiano wao maana alikuwa binti wa kiaka 21 wakati senator ana umri mkubwa
Duuh dunia kuna nyakati ipo unfair kama hiyo issue na ile issue ya kenya.Zote zipo unfair kwa wahanga mkuu
 
Umeongea kwa uelewa wako ila sio uelewa wa watu wote
Dunia ina watu zaid ya 7 billion je unazan wote wana experience km yako je unazan wote wanahisia km zako
 
Kuna kitu wauaji huwa wanajihisi"Upweke"sababu hakuna furaha kwenye kutoa roho ya mtu hasa pale mnapokutanisha macho kwa ghafla wakati wa tukio husika.

Anakutazama kwa macho ya kukuuliza "Kwanini mimi"? Hata unapomvizia kwa ghafla pale mwili wa binadamu anapoanguka chini unajihisi hatia, ukimwekea sumu utajihisi hatia, ukimpiga risasi utajihisi hatia and ect.

Nazungumzia aina zote za mauaji sababu ukitoa uhai wa mtu lazima hisia mkondo(Sindikizi) za uhai wake utazihisi. Hakuna furaha kwa wauaji hata kama hawajashiriki moja kwa moja, nafsi zao huwasuta.

Sijui Mungu aliumba vipi roho ya mwanadamu sababu ukifanya dhambi ya kuua lazima ukose amani ya moyo. Mungu sijui aliweka nini katika hili, wauaji huwa hawana furaha na amani maisha yao yote hata kama walichofanya ni siri.

Asilimia kubwa ya wauaji huwa wanajuta baadae kimoyo moyo kuhusu walichofanya.
Nakazia tu mkuu; Na ndio maana siku zote watu wanamwomba Mungu kusitokee vita kwani vita huacha maumivu makali zaidi kuliko yale yatokanayo na risasi na mabomu.
 
Kwahiyo kwenye vita watu huishi na hatia siku zote???
Namaanisha baada ya vita watu hai hubaki na maumivu makali zaidi ya yale maumivu ya risasi na mabomu(war trauma) i.e. Athari za kisaikolojia zitokanazo na vita e.g. watu wameona maiti zilizoharibiwa, watu wameona wapendwa wao wakiuliwa waziwazi, watu wamenusurika kifo kiajabu-ajabu n.k.
 
Namaanisha baada ya vita watu hai hubaki na maumivu makali zaidi ya yale maumivu ya risasi na mabomu(war trauma) i.e. Athari za kisaikolojia zitokanazo na vita e.g. watu wameona maiti zilizoharibiwa, watu wameona wapendwa wao wakiuliwa waziwazi, watu wamenusurika kifo kiajabu-ajabu n.k.
Haaah nimekuelewa mkuu.Kumbe kuona mtu aliyekufa vitani kunaweza kukuharibu kisaikolojia???
 
Back
Top Bottom