Hakuna jambo nzuri kama kuwa huru, usikubali kuwa Mbuzi wa kafara

nawaza tu kwa sauti, NYERERE angekuwa na mawazo haya sasa hivi tanzania ingekuwa kama SA!
 
Watu hatuna ajira,tumepambana kufungua vibiashara vya kusukuma siku kodi utitiri na mazingira magumu sana ya biashara vinatuacha hoi na madeni teleee! Uo uhuru uko wapi mambiligisi 😤
 
Nyerere na Karume wangejitenga na siasa, ungekuwa wapi leo?
Usichokijua ni kwamba, siasa inakuamulia hadi bei ya mkate&maisha Yako na uzao wako.
Muhimu tu;
Fanya siasa safi,pinga uovu, tenda haki.
Nyerere na wengineo hawakuwa keyboard warriors!

HIVI MNATAKA UHURU WA KISIASA AU MNATAKA UHURU WA KUFANYA VURUGU?

MNATAKA UHURU WA KISIASA AU MNATAKA UHURU WA KUTUKANA?

haya nyerere wetu wa sasa ingia frontline
 
Kwa hiyo ukae usubiri yakutokee wewe? Wewe jamaa kama ni baba wa familia, basi ni failure kwa kizazi chako.
Mimi ni Baba wa familia niliyechagua maisha yangu
 
Nyerere na wengineo hawakuwa keyboara warriors!

HIVI MNATAKA UHURU WA KISIASA AU MNATAKA UHURU WA KUFANYA VURUGU?

MNATAKA UHURU WA KISIASA AU MNATAKA UHURU WA KUTUKANA?

haya nyerere wetu wa sasa ingia frontline
Frontline?Hana ubavu huo
 
Watu hatuna ajira,tumepambana kufungua vibiashara vya kusukuma siku kodi utitiri na mazingira magumu sana ya biashara vinatuacha hoi na madeni teleee! Uo uhuru uko wapi mambiligisi
Kitendo tu cha kufungua biashara ni uhuru mkubwa sana..
Ni nchi gani ambayo haina kodi hapa duniani?
 
Well said
 
Siasa safi inahusiana na maendeleo ya mtu na nchi

nimezalisha kiwanda kidogo ambacho by 2030kitakua kiwanda kikubwa ….
Hcho kiwanda umekianzishia kwenye hi nchi ambayo haina uhuru(kwa mjibu wako) na unategemea kuwa mzalishaji mkubwa kwa nchi hii ambayo unaiponda?

HUONI KWAMBA UNAIGIZA?
 
Hcho kiwanda umekianzishia kwenye hi nchi ambayo haina uhuru(kwa mjibu wako) na unategemea kuwa mzalishaji mkubwa kwa nchi hii ambayo unaiponda?

HUONI KWAMBA UNAIGIZA?
Hawa ndio wanachangia Kwa kiasi kikubwa kuwapoteza wenzao,yeye projects zake zinaenda lakini Mdude hajulikani alipo
 
Tunataka kiongozi bora, tatizo ni kwamba wale wenye akili na maono wengi wanatoka katika familia masikini. Tufanyeje ili tuwaingize kwenye siasa? Maoni yako ni mazuri, unamaanisha usiingie kwenye siasa kichwa kichwa.
 
Tuzike ama tusafirishe
Unazungumzia uhuru au kuwa huru kivipi?

Kama ni uhuru naoujua mimi... Bs hukuwa na sababu ya kuja kueleza yote hayo.

Acha watu wawe huru kufanya yale wanayoona ni sahihi kwao.

Madhara au maanguko yao wewe hayatakugusa kwa chochote.

Ukiogopa wewe, unatakiwa ukae kimya.. Na sio ushawishi wengine waogope!!

Kila mtu alikuja duniani kwa njia zake na ataondoka kwa njia zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…