Hakuna jambo nzuri kama kuwa huru, usikubali kuwa Mbuzi wa kafara

Hakuna jambo nzuri kama kuwa huru, usikubali kuwa Mbuzi wa kafara

Hcho kiwanda umekianzishia kwenye hi nchi ambayo haina uhuru(kwa mjibu wako) na unategemea kuwa mzalishaji mkubwa kwa nchi hii ambayo unaiponda?

HUONI KWAMBA UNAIGIZA?
Mimi ni mtanganyika,mtanzania hapa ni kwangu ..hiki kiwanda nimekianzisha nyumbani kwetu na ni kweli kuna uvujanj mkubwa wa haki za kisiasa,rushwa uonevu uko juu! Ila hyo sio sababu ya mimi Kukimbia nchi yangu,Hivyo basi nitaendelea kupambana humu ndani ili kesho yetu iwe bora kwa sisi sote hadi nyie chawa!.
 
Watu hatuna ajira,tumepambana kufungua vibiashara vya kusukuma siku kodi utitiri na mazingira magumu sana ya biashara vinatuacha hoi na madeni teleee! Uo uhuru uko wapi mambiligisi 😤
Wakati mwingine unaweza kuta Tatizo ni wewe na si serikali,unadhani kwanini wengine biashara zao zinaenda kwenye nchi hii hii
 
Tunataka kiongozi bora, tatizo ni kwamba wale wenye akili na maono wengi wanatoka katika familia masikini. Tufanyeje ili tuwaingize kwenye siasa? Maoni yako ni mazuri, unamaanisha usiingie kwenye siasa kichwa kichwa.
Ewaaa umenielewa
 
Salaam jamiiAfrica.

Unataka kuwa huru?

Unataka kuwa na Amani?

Unataka watoto wako uwalee na wafurahie uwepo wako?

Unataka kufaidi mema ya Dunia,japo asilimia 0.01?

Jitenge na siasa,kaa mbali na wanasiasa.

Acha kuiongelea siasa.

Kaa kimya fanya mambo yako ,usifanye vitu Kwa kutafuta sifa,

Wewe siyo
Nelson Mandela,
Kwame Nkrumah,
John Okello,
Che Guevara,

Wewe ni mtoto wa masikini, wazazi wako wanakutegemea,na wanahitaji msaada wako pengine.

Kama familia yako hata ikiungana haina uwezo wa kuchanga pesa inafika milioni 5, bro/sister achana na siasa.

Ni rahisi watu kukusifia na kukuona Shujaa lakini ni ngumu wao kujitokeza wakawa na misimamo kama yako,

Ni rahisi mno watu kukupigia makofi na kukupa michango ya bukubuku na kukutanguliza front huku wakikuita mwamba , Shujaa,mwanaharakati na majina mengi ya kinafiki ,na wewe ulivyo na kichwa maji unajiona Samora Machel.

Wakuu pambaneni na maisha,
Sote tunajua,vitu na miundimbinu mingi ni dhaifu,bidhaa na materials bei ghali,Ajira hazitoshi pamoja na mengi lakini tunakaa kimya Kwa hatima ya vizazi vyetu.

Asalaam Aleykum jamiiy'aa
Mawazo ya kijinga kabisa!
Ndugu, tambua kuwa Maisha ni Siasa na Siasa ni Maisha!
Subiri JF ifungiwe na mwanasiasa tuone kama utaweza hata kuandika huu upuuzi! Nonsense!
 
Unazungumzia uhuru au kuwa huru kivipi?

Kama ni uhuru naoujua mimi... Bs hukuwa na sababu ya kuja kueleza yote hayo.

Acha watu wawe huru kufanya yale wanayoona ni sahihi kwao.

Madhara au maanguko yao wewe hayatakugusa kwa chochote.

Ukiogopa wewe, unatakiwa ukae kimya.. Na sio ushawishi wengine waogope!!

Kila mtu alikuja duniani kwa njia zake na ataondoka kwa njia zake.
Najua huwezi kujua hilo,eti tumwache na Uhuru wake.

Ushajiuliza,kwamfano ndugu yako wa damu,

Yupo jela Kwa kesi za kisiasa ,huku nyuma
Kaacha mke na watoto,je utawasaidia?

Na kama utawasaidia,huoni tayari umebeba majukumu mengine wakati muhusika si marehemu
 
Mawazo ya kijinga kabisa!
Ndugu, tambua kuwa Maisha ni Siasa na Siasa ni Maisha!
Subiri JF ifungiwe na mwanasiasa tuone kama utaweza hata kuandika huu upuuzi! Nonsense!
Mjinga wewe unayeandamana kwenye keyboard,
Kuna takribani watu 5000 wapo mahabusu Kwa kesi za kisiasa
 
Fanya leo,weka identity kamili,jitokeze pigania ukombozi wa kweli,hakika utakuwa mmoja wa watu wa shoka
Upo sahihi kaka,wengi humu ni wanafiki,ukiongea kma hv utaskia ukombozi....yan ukombozi utafkiri nchi ipo Kwenye Hatar kubwa,na hii ni ukiingia tu Huku mitandaoni ndo utahisi nchi inawaka moto muda si mrefu,ukiwaangalia hao raia Hawana hta hyo Habari kila mtu anapambana na maisha yake.
 
Mimi ni mtanganyika,mtanzania hapa ni kwangu ..hiki kiwanda nimekianzisha nyumbani kwetu na ni kweli kuna uvujanj mkubwa wa haki za kisiasa,rushwa uonevu uko juu! Ila hyo sio sababu ya mimi Kukimbia nchi yangu,Hivyo basi nitaendelea kupambana humu ndani ili kesho yetu iwe bora kwa sisi sote hadi nyie chawa!.
KAMA UNA UCHUNGU WE CHAWA WA FORD FOUNDATION, UNAPATA WAPI NGUVU YA KUFUNGUA KIWANDA ILI HALI WATANZANIA UNAOWAPGANIA HUJUI WALIPO, WALIOTEKWA?(kwa mjibu wenu)
 
Upo sahihi kaka,wengi humu ni wanafiki,ukiongea kma hv utaskia ukombozi....yan ukombozi utafkiri nchi ipo Kwenye Hatar kubwa,na hii ni ukiingia tu Huku mitandaoni ndo utahisi nchi inawaka moto muda si mrefu,ukiwaangalia hao raia Hawana hta hyo Habari kila mtu anapambana na maisha yake.
Watu ni wanafiki mno
 
Watu hatuna ajira,tumepambana kufungua vibiashara vya kusukuma siku kodi utitiri na mazingira magumu sana ya biashara vinatuacha hoi na madeni teleee! Uo uhuru uko wapi mambiligisi 😤
Sawa,sasa mpo wapi muonekane basi
 
Inaelekea kichwa yako ina tope. Kaa na mawazo ya kijinga. Bye
Hapo ulipo simu yako ina bundle la kutosha, pengine benki Una akiba ya kutosha, watoto wako wanasoma kifupi mambo yako ni safi,ulishawaza mtu akiwa locked familia yake inajisikiaje,vipi kuhusu masuala ya uchumi
 
Najua huwezi kujua hilo,eti tumwache na Uhuru wake.

Ushajiuliza,kwamfano ndugu yako wa damu,

Yupo jela Kwa kesi za kisiasa ,huku nyuma
Kaacha mke na watoto,je utawasaidia?

Na kama utawasaidia,huoni tayari umebeba majukumu mengine wakati muhusika si marehemu
Huo mfano wako una utofauti gan na ikiwa ndugu yangu kapotea hajulikani halipo? Na napoziuliza mamlaka hazinipi majibu..

Na yeye pia ameacha mke na watoto..!
 
Back
Top Bottom