Hakuna jamii iliyolala Tanzania kama watu wa kusini

Kusini mjanja alikua Sijaona Nangwanda tu
 
Masasi na mtwara ndio kunatazamika kidogo.

Ukienda lindi pale hamna kitu,mji ndani ya dk kumi ukiwa unatoka dar kwenda kusini basi kuanzia mwanzo wa mji pale kusini na mwisho wa mji wenyewe ndani ya dk 15 tu ushamaliza unaanza kuona mashamba ya chumvi.

Ama kwa hakika nyumbani kumepoa mno.
 
Mkuu unadhani dawa za kupuliza zina ufanisi wowote katika kuongeza kuzaa kwa mkorosho ?
 
Matusi yametosha wazee embu mtuwache


Maendeleo ya mchongo hayasaidii wazawa pahala popote acha watu wa kusini tupande step kwa step

1.Tuliweza kuandika historia yetu kabla ya hayo majiji yenu ya michongo mi naamini katika muda

NB:
TEMBEENI TANZANIA NI KUBWA SANA MKIACHANA NA HAYO MAJIJI MAKUBWA, KARIBU MIKOA YOTE ILIYO BAKI TWAFANANA TUU MSIANZISHE HII MIJADALA MKALETA CHUKI MIONGOMI MWETU SISI SOTE NI WATANZANIA

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Pwani ya kusini mwa Tanzania kuna nini. Kule nimewahi fika jua linachomoza saa 11 alfajiri yaan utaamka tuu. Ni kwamba wanafaida ya kuamka mapema kufanya shughuli za uzalishaji mali. Au wazee wa kobazi wamewateka kiakili.
 
kwa hiyo wewe wafurahia kusini kuwachwa nyuma na kujifahari nyie kupendelewa?
 
Ukweli nimechokoza mada hii kwa kuwa Nina njia niliyofikiria ninuarubali wa mabadiliko ktk jamii ya wakusini.

Hata hivyo nilitaka kusikia kutoka kwa wadau wenyewe kabla sijaleta mwelekeo wa njia mpya ya kutembea nayo.

Hadi sasa sijapata wazo mbadala zaidi ya kauli zinazoonyesha unyonge kutoka kwa wadau.

Mwelekeo sahihi. Chanzo cha tatizo nini:-
Kuelekea kupata suluhisho lazima tujue chanzo kikuu cha tatizo mini, lazima tujue tulipojikwaa na sio tulipoangukia.


Kikwazo kikubwa kimojawapo cha kanda ya kusini kusahaulika ktk masuala maxima ya maendeleo ni kuwa Tanzania ni kubwa na mfuno was serikali kuu hauna na wala hautapata uwezo was kupeleka maendeleo Tanzania yote. Mfumi huu unalazimisha kuwepo ubaguzi kwa baadhi ya kanda.


Kuendelea kukumbatia mfumo huu wa utawala was Serikali kuu kwa jamii ya watu wa kusini, Mfumo ambao ushakuwa mkongwe wa miaka zaidi 60 ya Uhuru. Kuuendelea kuuegemea ni sawa kuupa sapoti mgomba dhaifu ukizaa mkungu mkubwa wa ndizi ili usinguke unazuia na nguzo. Lkn ndizi hizo zikishakomaa hupati manufaa yake. Serikali kwasasa ccm imeelemewa na maitaji ya wa tz. Lkn kubwa zaidi imeelemewa na madeni kiasi kwambainaelekea kuvuka mstari wa kukopesheka.


Mwelekeo

Ni lazima jamii iamke usingizini wa fofofo na ifanye Maamuzi magumu, maamuzi mapya, lkn lazima yafanyike maamuzi magumu. Kwa kuukataa mfumo huu ulioelemewa.

Vyama vyote vinavyoamini mfumo was serikali kuu vikataliwe.
Vyama vinavyoamini mfumo wa serikali tatu pia hauna faida kwa wana kusini. Tunahitaji mfumo ule wa kikoloni na baada ya Uhuru. Mfumo wa seriKali za Majimbo ambapo kusini lilijulikana kama Southern Province. Kwa lugha nyepesi lazima wanakusini waunganishe nguvu na kusimama au kuanzisha chama kitakachi amini na kusimamia mfumo wa serikali za majimbo yatakayokuwa na Uhuru zaidi wa kujiamulia mambo yao wenyewe.

Jambo hili so geni na wala halitakuwa geni. Kwasasa serikali ya ccm imelipatia nguvu na Uhuru zaidi jimbo moja tu la znz. Tunahitaji chama ambacho kitazipa nguvu Majimbo na uhuru was kujiamulia uchumi wao, utamaduni wao, elimu yao, mambo yao ya kijamii nk

kila jimbo lihodhi 75% ya rasilimali zake. 25% ziende serikali kuu kwa ajili ya kujiendesha na kwa ajili ya kusaidoa majimbo yasiyo na rasilimali yajitengenezee artificial rasilimali. Eg elimu maalum kama ya engineering au IT.

Hakuna haja kukumbatia chama Kama bendera kufata upepo. Kipindi Fulani nilikwenda kufanya kijiutatfiti kwa kuwauliza kwann mmetoka CUF na kwenda ACT wengi walijibu tumemfata Maalim . nikawauliza maalim akishinda urais znz jamii ya watu wa kanda ya kusini mtafaidika vp urais wa Maalim Seif (Mungu Amrehemu) hawakuwa na jibu. Hawakuwa na jibu kwa kuwa Maalim seif alijipambanua kuwa anapigania Uhuru zaidi wa znz kujiamulia mambo yao wenyewe.

Ndugu zangu najua wamenielewa lkn watakuja na swali moja kuuliza. Sasa kama tutaipunguzia nguvu serikali kuu sasa hayo madeni ya tri 71 ya serikali kuu atalipa nani!??

Jibu rahisi ni guys mind ur business. Else majimbo husika yaliyonufaika na madeni hayo ndio watakuwa walipaji wakuu. Nawatalipa kulingana na faida kayozaliswa na miradi hiyo.

Ndugu zangu hili wazo linaingia akilini, je linatekelezeka?!?


R U ready U my fellow guys kufata njia hii
 
Ebu niambie lindi inafanana na mkoa gani hata Tanzania kwajinsi palivyo nyata...ukweli lazima usemwe mikoa ya kusini hasa lindi na mtwara..mmezubaa sana changamkeni achaneni na umwinyi.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ndugu zangu hili wazo linaingia akilini, je linatekelezeka?!?
Kaka wazo lako zuri sana na linatekelezeka vizuri ikiwa serikali yenyewe itaamua vizuri kufanya hivyo kutokana na misukumo mbalimbali.

Ishu ni kuwa endapo serikali itaamua kulitekeleza hili haraka iwezekanavyo basi inaweza kusaidia kuinua mikoa hiyo.

LAKINI ikiwa haijawa tayari maana yake hatuwezi kusubiri wawe tayari kufanya lazima tutafute njia nyingine ya kuinua mikoa hiyo kwa wakati huu ambapo serikali haijawa tayari kuanzisha serikali ya majimbo.

Na huo mbadala ndio tunatakiwa kuujadili sasa hivi na mbadala huo ni bora iwe na mipango ambayo inatekelezeka kwa sasa hivi bila kusubiri idhini ya serikali.

Mbadala huo uwe hauna kikwazo chochote kwa wananchi kuchukua hatua kwa upande wao.

Mimi naona kwa sasa kwanza ELIMU ELIMU ELIMU elimu ambayo itachange mindset za watu wa kusini.

Elimu hii isitolewe na watu wa vyama fulani tu kwa sababu kampeni ya elimu hiyo itageuzwa na kufanywa kuwa kampeni ya kisiasa na uchama.

Kampeni hiyo isijikite katika kuilaumu serikali mbele ya wanakusini kwa sababu kuilaumu serikali itawafanya wao waendelee kulala na kuona kwamba wao hawana kosa lolote katika udororaji wa mikoa hiyo bali serikali na hiyo itaendelea kuwafanya wawe mapono tu wajione hawajakosea popote.

Kampeni hiyo iwaeleze wanakusini kwa busara wapi wamekosea na nini wafanye kuboreaha maisha ya mtu mmoja mmoja kwanza kabla ya kuboresha public issues.

Watu wa kusini wanahitaji kujikwamua na ujinga kwa kuwapa elimu pana.

Wanahitaji kujikwamua na njaa na umasikini pia na hapo ndipo shida inapokuja.

Pia waelimishwe vijana wa kusini umuhimu wa kuwa na malengo na kuacha kuishi katika njia ambazo wazazi wao wamepita.

Elimu hiyo itolewe huku watoaji elimu wakiwagawa watu kwa mujibu wa makundi yao,vijana wa shule wapewe elimu kwa mujibu wa maeneo yao,wazazi wapewe elimu kwa mujibu wa maeneo yao pia.

Yani elimu hii iguse kila mtu wa kusini,kila rika elimu hiyo isijihusishe na chama fulani bali elimu hiyo iwakusanye watu wa vyama vyote.
 
Hata dodoma kwenyew ni vile vile tuuu
Mataa yapo barabara vyuo mahospitali lkn


Bado:
Sisi wavivu tunapata supu ya pweza kabla hata jua kutoka

NB:
Point yangu ni kwamba hayo maendeleo yanawanufaisha vipi wazawa
 
Mnatamba sana wazee wenzangu wakati tunawajua vizuri tuu nje ndani na hata tukija huko mikoani kwenu kufuata elimu mnaongoza kutoa maboko kiufupi tuko juu sema tuu hamtaki kukubali
 
Ingependeza zaidi na kusomeka vizuri na kueleweka kama ungeliielezea kwa lugha ya kidplomasia zaidi na pia kichwa cha habari kisichokuwa na ukakasi. Kwanini usingesema tu "Serikali ikumbuke kupeleka miradi ya maendeleo kusini?
Mbona miradi ya maendeleo kusini ipo tena hata zaidi ya kaskazini? Huyu aliyeandika huu uzi anaendaga kusini kweli. Barabara kutoka Dar-Lindi-Masasi-Mtwara lami. Barabara kutoka Masasi-Tunduru-Songea lami. Kutoka Songea-Mbinga-Mbamba Bay lami. Songea-Njombe-makambako-Mbeya lami tena ya siku nyingi. Wilaya ya Nanyumbu ina stand ya kisasa(Mangaka), Songea wana stand ya kisasa(Shule ya Tanga). Njombe wana stand na soko la kisasa. Wakati mkoa kama Manyara ni vumbi tupu. Hakuna stand wala soko. Wilaya ya Mbulu ambayo mji wake ulijengwa na wajerumani tangi 1905 mpaka leo ni vumbi. Wilaya za Kieto na Simanjiro vumbi. Mi naona wamejengewa miundo mbinu mizuri kuliko kanda zingine. Ninachokiona ni wapole siyo waongeaji wala siyo watu wa sifa mfano km wachaga, wana ushamba flani hawatembelei maeneo mengi wao wanajua Tanzania ni Dar ukiuliza habari kwa mfano ya Arusha hajui chochote anaweza kukuambia Arusha ni kubwa kuliko Dar Es Salam..
 
Nakuelewa sana mkuu
 
Utaskia sijui elimu nini nini


Wakati top ten Lindi imeingia mara 3 mfululizo na hakuna mtu ameliona ilo


Ukusanyaji wa mapato halimashauri ya wilaya ya kilwa imesha fanya maajabu mara kibao tuu


Hata ivo watu wake wana furaha na at least wanajua namna ya kuishi

HABARI YA SGR SIJUI AIRPORT NI MUDA TUUU
UKIFIKA ZITAKUEPO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…