Hapo zamani, JWTZ ilikuwa na uwezo mkubwa wa kukabiliana na vikosi vya Watutsi, wakiwemo wapiganaji wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda pamoja na Uganda (Muhoozi amewahi kutamka wazi M23 ni kaka zake)
Hata kama vikosi vilipokuwa vya Sadc, walipopata taarifa kuwa Tanzania ni sehemu ya vikosi hivyo, walikuwa wanakosa usingizi.
Tukio la kihistoria lIlikuwa ni mnamo 2013 pale Tanzania ilipokuwa sehemu ya jeshi SADC walipowafurusha kabisa waasi wa M23 kwenye ngome zao za mwisho huku kikosi cha Jwtz ikisifiwa kwa mchango mkubwa iliotoa. Hadi leo waasi wa M23 hawasahau muziki wa JWTZ wa mwaka 2013! 🔥 makomanda wetu walionyesha kazi ya kishujaa na kuwatimua kabisa waasi hao kwenye ngome zao za mwisho. Huu ulikuwa wakati ambao Africa ilisimama na kukiri kuwa JWTZ si jeshi la mchezo mchezo, kutokana na mchango wao mkubwa
Hata hivyo, hali ya medani imebadilika kwa kiasi kikubwa. Vikosi ambavyo zamani vilionekana kutetemeka vilivyosikia JWTZ, vimeendelea kuimarika kijeshi hadi kufikia hatua inayozua maswali mengi kuhusu mabadiliko ya nguvu katika eneo hili.
Sitaisahau kamwe tukio la huzuni la mwaka jana. Jeshi letu la JWTZ Wakiwa sehemu ya vikosi vya SADC walijikuta kwenye unyonge ulioumiza mioyo ya wengi, mashujaa wetu walizingirwa na kukwama, bila namna ya kujihami wala kujinasua ilibidi waweke silaha chini. kilichofuata kilikuwa ni jeraha kubwa, Kwa huruma iliyojaa kebehi iliyofichika, waliruhusiwa kuondoka, lakini kwa masharti yaliyovua ukamavu wao. Walilazimika kuvua sare zao, wakaachia silaha zao nyuma, na kupandishwa kwenye mabasi ya kiraia kama wakimbizi wasio na watetezi. Aibu ilioje kuona jeshi letu kubwa, lile lililowahi kuwafunda adabu kundi hilo 2013, walisindikizwa chini ya ulinzi mkali (escort) wa Jeshi la Rwanda (RDF). Taswira ya mashujaa wetu wakisubirishwa mpakani mwa Rwanda, wakiwa chini ya ulinzi wa Rwanda, kufanyiwa ukaguzi mkali (Kupigwa search), huku wakipewa maelekezo, ilikuwa ni anguko kubwa la heshima ya kihistoria linaloendelea kuacha kovu na kilio cha chini kwa kila Mtu anayekumbuka jinsi JWTZ lilivyokuwa ikiheshimika.
Lakini kupitia hayo kuna jambo moja lilionekana clear, watutsi wanazidi kuimarisha majeshi yao, kufikia 2050 wanaweza kuwa na majeshi hatari sana kwa huu ukanda.