1. JESHI NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA
Njia mojawapo ya kawaida ya mapinduzi ya serikali ni jeshi kuingilia siasa na kuiondoa serikali iliyopo madarakani kwa kutumia nguvu. Kwa mfano walichofanya kina Ibrahim Traore wa Burukina Faso.
Hata hivyo, katika muktadha wa Tanzania, Baada ya majaribio ya mapinduzi yaliyoshindwa katika historia ya Tanzania, uhusiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama na utawala wa nchi umekuwa suala muhimu katika mijadala ya kisiasa.
Hoja kuhusu uhusiano huo ilipata uzito zaidi baada ya Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Oganaizesheni, Paul Chacha, kunukuliwa akisema:
“Hivi nani ambaye hajui vyombo vyote vya ulinzi na usalama ni mali ya Chama Cha Mapinduzi?”
Tupia jicho hata baadhi ya Teuzi kama wakuu wa Mikoa, utawakuta viongozi waliowahi kuwa kwenye vyombo hivi.
2. MSAADA WA SERIKALI YA NJE
Historia inaonyesha kuwa msaada kutoka nje ya nchi unaweza kuwa na athari kubwa katika mabadiliko ya utawala, hasa pale ambapo kuna migogoro ya ndani.
Mfano ni kuondolewa kwa Idi Amin nchini Uganda mwaka 1979, baada ya Tanzania kuingia vitani dhidi ya Uganda kufuatia uvamizi wa vikosi vya Uganda katika eneo la Kagera.
Vilevile, migogoro katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeonyesha jinsi uungwaji mkono wa nje kwa makundi yenye silaha unavyoweza kuongeza nguvu na muda wa migogoro. M23 ni mojawapo ya makundi ambayo yamehusishwa na madai ya kupata msaada kutoka nchi jirani
3. MFUMO WA UTAWALA NA UKOSEFU WA NGAZI HURU ZA KIMAENEO
Mfumo wa majimbo huwa unatoa mamlaka makubwa kwenye majimbo, watu wa majimbo husika wanakuwa loyal sana kwenye majimbo yao kuzidi nchi, na ndio maana mfumo huu hupenyeza kirahisi ukabila , ukanda, n.k. ni mfumo huu ambao unatumika nchi kama Nigeria, Sudan, Congo na Ethiopia ambazo zimekuwa vitani kwa muda mrefu.
kwenye mfumo huu mwanamapinduzi anaweza kupata "ngome" kwenye jimbo, na kulitumia kama sehemu ya kuanzia (launchpad). Mfano ni kinachoendelea Congo, Kabila katangaza kikundi chake kwenye Ngome yake.
Tanzania ni mazingira tofauti, Leo hii, hata ukiamua kuanzisha harakati zako huko ndani kabisa Ruvuma, usidhanie kwamba umbali wa eneo lako utakupa nafasi ya kujipanga bila changamoto. Mtandao wa utawala na taasisi za serikali unaanzia ngazi ya kijiji, kata na tarafa hadi wilaya na mkoa. Hivyo, nafasi ya kuendesha harakati kwa kujitenga na mifumo iliyopo ya mamlaka ni finyu sana.