Hakuna jipya chini ya jua: Kinachomkuta Marekani nchini Iran kiliwahi wakuta watangulizi wake

Mifano iko mingi mno, ambayo MADUNYA na MABAZAZI wakiisoma wataelewa, lakini kwasababu watanzania wengi ni wazee wa kupita njia rahisi (Short-Cut) sidhani kama hata watajisumbua zaidi ya kumuuliza Grok na ChatGPT.

ENIWEI ntaendelea...
Hawa Madunya na Mabaazazi wapo humu wanapiga shortcuts na kusubiria muendelezo nitakuwepo hapa
 
Good analysis,
Kama bado mifano na maelezo yote hayo bado kuna mtu anakaza fuvu hakika atakuwa na shida mahali.
Kama hadi raia wa na viongozi wa USA na Israel wanakiri kupoteza katika hii vita wewe nani unashupaza shingo?
Hapo kuna mifano miwili ya mwisho ya muhimu zaidi ameielezea umeisoma yote kwa pamoja lakini?
 
Wasalaam Ndugu MALCOM LUMUMBA

Mwanzoni nilidhani Iran anakatazwa kumiliki silaha za nyuklia kwa sababu ya usalama wa Israel pale mashariki ya kati, ila naona URUSI pamoja na kwamba ni mshirika wa IRAN pia anakubaliana na MAREKANI kuwa Iran hastahili kumiliki nyuklia. Naomba kujua sababu ya msingi kwa nini Iran anakatazwa kumiliki silaha ya nyuklia?
 
Huwa nalipenda sana somo la historia.

1. Ukisoma historia kwa kina utafahamu ukweli kwamba hakuna jipya chini ya jua.

2. Yote unayoyafanya yalishafanywa na wenzako huko nyuma.

3. Wewe unachofanya ni kujenga juu ya msingi wa mwingine tu.

4. Wanaoamini kwamba historia ina vitu vipya ni MADUNYA na MABAZAZI wa Tanganyika tu.

Mataifa makubwa yamekuwepo tangu ustaarabu ulipoanza kuandikwa kule Mesapotamia, China na Misri. Hivyo Marekani kama dola (Empirial State) lenye nguvu hapa duniani halina jambo jipya. Kinachomkuta Marekani nchini Iran, kimeshawahi kuyakuta madola makubwa (Imperial States) nyingi miaka 3000 kabla ya Marekani kuzaliwa.

Kama binadamu tungekuwa tunaishi miaka 4,000 basi tusingeshangazwa na mataifa kama Marekani, kwasababu tungekuwa tumeishi kushuhudia madola mengi nyuma kama Ashuru (Neo-Assyrian Empire), Babel (Neo-Babylonian Empire), Makedonia (Macedonian Empire), Rumi (Dola la Rumi), Chin (Qing Dynasty), Han (Han Dynasty), Song (Song Dynasty), Tang (Tang Dynasty), Muga (Mughal Empire), Madola ya kiislamu (Rashidun, Ummayed and Abbasid Caliphates) Mongolia (Mongolian Empire), Uhispania (Spanish Empire), Ureno (The Portuguese Empire), Uingereza (The British Empire) n.k

Kama ambavyo viumbe hai vina sifa kuu, basi hata madola (Empires) huwa zina sifa zinazofanana sana ambazo hupelekea kuzaliwa (Birth), kukua (Growth/Ascendancy), Kukomaa (Zenith), kudorora (Shrinking) na kuanguka (Collapse). Wanahistoria wameyaona haya kwenye madola yote yaliyowahi kutawala miaka 500 iliyopita. Ndiyo maana kuna swali huwa wengi wanapenda kuuliza: Hivi Warumi(Western Roman Empire) wakati dola lao linakaribia kuanguka walifahamu kwamba lilikuwa linaanguka au walikuwa hawafahamu ???

Ukisoma historia utafahamu kwamba wengi walikuwa hawafahamu na waliamini kwamba Rumi inaweza ikaendelea kufanya inavyotaka bila kukumbwa na changamoto yoyote kwasababu wao ndiyo wakubwa wa dunia (The Known World). Ila kumbe kama ambavyo mchwa huwa anaanza kula mbao kwa ndani, ndivyo matatizo ya Rumi yalivyokuwa bila wao kuyaona. Marekani inapitia kipindi kigumu mno katika historia yake ya miaka zaidi ya 250. Marekani kama dola kubwa duniani (An Imperial State) ambalo limeshawishi dunia tokea mwaka 1945, limakuwa na nguvu kuu nne:

a) Umoja wa kitaifa (National Cohesion)
b) Nguvu ya kijeshi (Military Power)
c) Nguvu kubwa ya ushawishi (Soft Power/Cultural Influence and Propaganda)
d) Nguvu kubwa ya kiuchumi

Tofauti na madola ya zamani ambayo yamekuwepo kipindi ambacho dunia haijawa na mfumo wa fedha wa pamoja (International Monetary System), Marekani ametumia nguvu yake kiuchumi hasa dola kama moja ya silaha hatari za kuzorotesha maaduia zake. Zamani kabla ya mfumo wa fedha wa pamoja (International Monetary System) mataifa yalikuwa yanatumia mbinu kama Protectionism na Sanctions kama silaha za kiuchumi.

Mwaka 1588 wakati Malkia Elizabeth wa Uingereza amegoma kulamba miguu ya Papa wa Rumi, Vatican ilituma vikosi vya mamia ya meli kumsulubisha ila vikashindwa. Njia viliyotumia ni kuweka vikwazo kwamba mataifa yote ya Kiroma hayatakiwi kufanya biashara na taifa la Kiprotestanti la Uingereza. Pona pona ya Uingereza ilikuja baada ya Sultan Murad III wa Uturuki (Ottoman Empire) kuruhusu Uingereza ifanya biashara kwenye himaya yake.

====================================================================================
SASA BASI kule Iran Marekani alikuwa na nyenzo kuu mbili za kusulubisha Maayatollah na Mamullah. Nguvu ya kijeshi (Military Power) na Nguvu ya Kiuchumi (Economic Power). Mwaka 2011 Raisi Obama alitumia nguvu ya uchumi kulazimisha Iran ije kwenye meza ya mazungumzo mwaka 2014 na kusaini mkataba wa nyuklia (The Iran Nuclear Deal), ambapo mabenki ya Iran yalitolewa kwenye mfumo wa SWIFT na nchi kuwekewa vikwazo vya kutisha.

Kipindi hiki Marekani katumia mbinu zote na bado ameshindwa kuwang'oa Maayatollah na Mamullah wa Iran. Wataalamu wengi wanasema Marekani ameigeuza Iran kuwa taifa lenye kisirani na huenda likaamua kutengeneza kweli silaha za kinyuklia, jambo ambalo litakuwa na hatari zaidi.

===================================================================================
MABAZAZI na MADUNYA kwa kukosa maarifa hawataki kuamini kwamba Marekani imeshindwa nchini Iran mbali. Mbinu zote, kuanzia vikwazo vya kiuchumi (Sanctions), Mauaji (Targeted Assassinations) na Uvamizi Mkubwa wa Kijeshi (Overwhelming Invasion) vimefeli kabisa. Ukisoma historia jambo kama hili limeyakuta madola mengi mno.

MIFANO YA KIHISTORIA:

1. Roman-Parthian War (The Carrhae Disaster)

Mwaka 53 B.C, Bilionea wa Kirumi Marcus Crassus ambaye alikuwa tajiri mkubwa Rumi alivamia Uajemi (Parthia) ambako leo hii ni Iran akiwa na wanajeshi zaidi ya 40,000 ambao ni wazoefu wa vita (Military Veterans). Warumi ndiyo walikuwa na jeshi bora kipindi hicho. Basi Bilionea Crassus kutaka sifa akavamia Parthia. Kule akakutana na wanajeshi 10,000 ambao walikuwa wamezidiwa idadi na Warumi.

Kiongozi wa jeshi la Kiajemi, Surena akifahamu fika kwamba hawezi kupambana na Rumi kwenye vita ya wazi (Pitched Battle) aliamua kutumia mbinu mbadala (Asymmetric Warfare) kusababisha hasara kubwa kwa Rumi. Alitumia milima ya Iran kama silaha, ambapo alisubiri wanajeshi wa kirumi waingine katikati kwenye korongo, halafu wao wakawazunguka pande zote.

Surena akatengeneza ukuta wa duara ambao ulizungukwa na wapiga upinde, ambao walianza kufyatia mishale bila kupumzika kwa masaa. Nje ya huu ukuta wa kwanza ukatengenezwa ukuta wa pili wa mikakati (Logistics and Supply) ambapo walikuwa wanaleta mishale mipya.

Warumi mara ya kwanza waliweka ngao zao kuzuia mishale wakidhani waajemi wataacha baada ya muda. Bahati mbaya waajemi wakawa wanafyatua mishale masaa bila kusimama wakisababisha hadi angala linakuwa jeusi kwa wingu la mishale. Mwishowe ngao za waajeshi zikaanza kuvunjika na wenyewe baada ya kuona hivyo morali ikaisha, mishale ikaanza kuwachoma wakaanza kufa kwa maelfu.

Ile wanataka kukimbia wakazungukwa na jeshi la wapanda farasi wa kiajemi waliokuwa wamevaa vyuma (Cataphracts) ambao walianza kuchinja warumi waliochoka. Crassus alikamatwa na Surena akayeyusha dhahabu ya moto na kumwangushia kichwani. Roma na ubabe wake alinyooshwa.

2. First Battle of Dongola

Mwaka 642, wavaa kobazi wametoka huko Mashariki ya kati wamewachakaza Warumi na Waajemi vibaya mno na kugeuka kuwa dola lenye nguvu duniani kwa wakati huo (The Rashidun Caliphate), wakajichanganya na kusema wavamia ufalme wa Kikristo uliopo Sudan uitwao Mekuria.

Ile kuvamia wakakutana na jangwa na binadamu wataalamu mno wa kufyatua upinde. Waarabu wakaanza kufa, ikafika mahali wasudani wakawa wanawauliza "Mnataka kupige mshale wapi ?" kama kejeli, Mwarabu mmoja akajibu na kuonesha alama ya jicho akiwa mbali akidhani hawezi fikiwa. Msudani alifyatua mshale na ukamfikia palepale jichoni.

Hii ndiyo ilikuwa vita ya kwanza dola kubwa la kiislamu, lenye maelfu ya askari kushindwa na ufalme mdogo ambao hauna askari wengi. Lilikuwa somo gumu kwa waarabu na wakaamua kugeuza njia kulekea huko Morocco na Tunisia.

=======================================================================
Mifano iko mingi mno, ambayo MADUNYA na MABAZAZI wakiisoma wataelewa, lakini kwasababu watanzania wengi ni wazee wa kupita njia rahisi (Short-Cut) sidhani kama hata watajisumbua zaidi ya kumuuliza Grok na ChatGPT.

ENIWEI ntaendelea...
​
Good analysis
 
Okay good question,
Ishu ni kuwa Iran anatishia wakubwa wengi sio USA na Israel pekee,
Sababu zinazofanya Marekani apambane na Iran ndio zinazofanya Russia asitamani Iran kumiliki Nyuklia,
Iran akishakuwa na Nyuklia bei za mafuta Duniani ndio atakuwa anaamua na mafuta ndio uchumi wa Dunia.

Pia Iran anamahusiano makubwa na China kwahiyo sarafu ya China ndio itakuwa fedha ya uchumi wa Dunia ikiwa Iran atakuwa na power ya kuamua nini afanye.

Nguvu ya Taifa ni Uchumi na Iran yuko sehemu nyeti ya Uchumi wa Dunia.
 
Asante mkuu.
 
Wasalaam Ndugu MALCOM LUMUMBA

Mwanzoni nilidhani Iran anakatazwa kumiliki silaha za nyuklia kwa sababu ya usalama wa Israel pale mashariki ya kati, ila naona URUSI pamoja na kwamba ni mshirika wa IRAN pia anakubaliana na MAREKANI kuwa Iran hastahili kumiliki nyuklia. Naomba kujua sababu ya msingi kwa nini Iran anakatazwa kumiliki silaha ya nyuklia?
Hivi wewe unaweza kuruhusu serikali ya CCM ikamili nyuklia ???​
 
Huwa nalipenda sana somo la historia.

1. Ukisoma historia kwa kina utafahamu ukweli kwamba hakuna jipya chini ya jua.

2. Yote unayoyafanya yalishafanywa na wenzako huko nyuma.

3. Wewe unachofanya ni kujenga juu ya msingi wa mwingine tu.

4. Wanaoamini kwamba historia ina vitu vipya ni MADUNYA na MABAZAZI wa Tanganyika tu.

Mataifa makubwa yamekuwepo tangu ustaarabu ulipoanza kuandikwa kule Mesapotamia, China na Misri. Hivyo Marekani kama dola (Empirial State) lenye nguvu hapa duniani halina jambo jipya. Kinachomkuta Marekani nchini Iran, kimeshawahi kuyakuta madola makubwa (Imperial States) nyingi miaka 3000 kabla ya Marekani kuzaliwa.

Kama binadamu tungekuwa tunaishi miaka 4,000 basi tusingeshangazwa na mataifa kama Marekani, kwasababu tungekuwa tumeishi kushuhudia madola mengi nyuma kama Ashuru (Neo-Assyrian Empire), Babel (Neo-Babylonian Empire), Makedonia (Macedonian Empire), Rumi (Dola la Rumi), Chin (Qing Dynasty), Han (Han Dynasty), Song (Song Dynasty), Tang (Tang Dynasty), Muga (Mughal Empire), Madola ya kiislamu (Rashidun, Ummayed and Abbasid Caliphates) Mongolia (Mongolian Empire), Uhispania (Spanish Empire), Ureno (The Portuguese Empire), Uingereza (The British Empire) n.k

Kama ambavyo viumbe hai vina sifa kuu, basi hata madola (Empires) huwa zina sifa zinazofanana sana ambazo hupelekea kuzaliwa (Birth), kukua (Growth/Ascendancy), Kukomaa (Zenith), kudorora (Shrinking) na kuanguka (Collapse). Wanahistoria wameyaona haya kwenye madola yote yaliyowahi kutawala miaka 500 iliyopita. Ndiyo maana kuna swali huwa wengi wanapenda kuuliza: Hivi Warumi(Western Roman Empire) wakati dola lao linakaribia kuanguka walifahamu kwamba lilikuwa linaanguka au walikuwa hawafahamu ???

Ukisoma historia utafahamu kwamba wengi walikuwa hawafahamu na waliamini kwamba Rumi inaweza ikaendelea kufanya inavyotaka bila kukumbwa na changamoto yoyote kwasababu wao ndiyo wakubwa wa dunia (The Known World). Ila kumbe kama ambavyo mchwa huwa anaanza kula mbao kwa ndani, ndivyo matatizo ya Rumi yalivyokuwa bila wao kuyaona. Marekani inapitia kipindi kigumu mno katika historia yake ya miaka zaidi ya 250. Marekani kama dola kubwa duniani (An Imperial State) ambalo limeshawishi dunia tokea mwaka 1945, limakuwa na nguvu kuu nne:

a) Umoja wa kitaifa (National Cohesion)
b) Nguvu ya kijeshi (Military Power)
c) Nguvu kubwa ya ushawishi (Soft Power/Cultural Influence and Propaganda)
d) Nguvu kubwa ya kiuchumi

Tofauti na madola ya zamani ambayo yamekuwepo kipindi ambacho dunia haijawa na mfumo wa fedha wa pamoja (International Monetary System), Marekani ametumia nguvu yake kiuchumi hasa dola kama moja ya silaha hatari za kuzorotesha maaduia zake. Zamani kabla ya mfumo wa fedha wa pamoja (International Monetary System) mataifa yalikuwa yanatumia mbinu kama Protectionism na Sanctions kama silaha za kiuchumi.

Mwaka 1588 wakati Malkia Elizabeth wa Uingereza amegoma kulamba miguu ya Papa wa Rumi, Vatican ilituma vikosi vya mamia ya meli kumsulubisha ila vikashindwa. Njia viliyotumia ni kuweka vikwazo kwamba mataifa yote ya Kiroma hayatakiwi kufanya biashara na taifa la Kiprotestanti la Uingereza. Pona pona ya Uingereza ilikuja baada ya Sultan Murad III wa Uturuki (Ottoman Empire) kuruhusu Uingereza ifanya biashara kwenye himaya yake.

====================================================================================
SASA BASI kule Iran Marekani alikuwa na nyenzo kuu mbili za kusulubisha Maayatollah na Mamullah. Nguvu ya kijeshi (Military Power) na Nguvu ya Kiuchumi (Economic Power). Mwaka 2011 Raisi Obama alitumia nguvu ya uchumi kulazimisha Iran ije kwenye meza ya mazungumzo mwaka 2014 na kusaini mkataba wa nyuklia (The Iran Nuclear Deal), ambapo mabenki ya Iran yalitolewa kwenye mfumo wa SWIFT na nchi kuwekewa vikwazo vya kutisha.

Kipindi hiki Marekani katumia mbinu zote na bado ameshindwa kuwang'oa Maayatollah na Mamullah wa Iran. Wataalamu wengi wanasema Marekani ameigeuza Iran kuwa taifa lenye kisirani na huenda likaamua kutengeneza kweli silaha za kinyuklia, jambo ambalo litakuwa na hatari zaidi.

===================================================================================
MABAZAZI na MADUNYA kwa kukosa maarifa hawataki kuamini kwamba Marekani imeshindwa nchini Iran mbali. Mbinu zote, kuanzia vikwazo vya kiuchumi (Sanctions), Mauaji (Targeted Assassinations) na Uvamizi Mkubwa wa Kijeshi (Overwhelming Invasion) vimefeli kabisa. Ukisoma historia jambo kama hili limeyakuta madola mengi mno.

MIFANO YA KIHISTORIA:

1. Roman-Parthian War (The Carrhae Disaster)

Mwaka 53 B.C, Bilionea wa Kirumi Marcus Crassus ambaye alikuwa tajiri mkubwa Rumi alivamia Uajemi (Parthia) ambako leo hii ni Iran akiwa na wanajeshi zaidi ya 40,000 ambao ni wazoefu wa vita (Military Veterans). Warumi ndiyo walikuwa na jeshi bora kipindi hicho. Basi Bilionea Crassus kutaka sifa akavamia Parthia. Kule akakutana na wanajeshi 10,000 ambao walikuwa wamezidiwa idadi na Warumi.

Kiongozi wa jeshi la Kiajemi, Surena akifahamu fika kwamba hawezi kupambana na Rumi kwenye vita ya wazi (Pitched Battle) aliamua kutumia mbinu mbadala (Asymmetric Warfare) kusababisha hasara kubwa kwa Rumi. Alitumia milima ya Iran kama silaha, ambapo alisubiri wanajeshi wa kirumi waingine katikati kwenye korongo, halafu wao wakawazunguka pande zote.

Surena akatengeneza ukuta wa duara ambao ulizungukwa na wapiga upinde, ambao walianza kufyatia mishale bila kupumzika kwa masaa. Nje ya huu ukuta wa kwanza ukatengenezwa ukuta wa pili wa mikakati (Logistics and Supply) ambapo walikuwa wanaleta mishale mipya.

Warumi mara ya kwanza waliweka ngao zao kuzuia mishale wakidhani waajemi wataacha baada ya muda. Bahati mbaya waajemi wakawa wanafyatua mishale masaa bila kusimama wakisababisha hadi angala linakuwa jeusi kwa wingu la mishale. Mwishowe ngao za waajeshi zikaanza kuvunjika na wenyewe baada ya kuona hivyo morali ikaisha, mishale ikaanza kuwachoma wakaanza kufa kwa maelfu.

Ile wanataka kukimbia wakazungukwa na jeshi la wapanda farasi wa kiajemi waliokuwa wamevaa vyuma (Cataphracts) ambao walianza kuchinja warumi waliochoka. Crassus alikamatwa na Surena akayeyusha dhahabu ya moto na kumwangushia kichwani. Roma na ubabe wake alinyooshwa.

2. First Battle of Dongola

Mwaka 642, wavaa kobazi wametoka huko Mashariki ya kati wamewachakaza Warumi na Waajemi vibaya mno na kugeuka kuwa dola lenye nguvu duniani kwa wakati huo (The Rashidun Caliphate), wakajichanganya na kusema wavamia ufalme wa Kikristo uliopo Sudan uitwao Mekuria.

Ile kuvamia wakakutana na jangwa na binadamu wataalamu mno wa kufyatua upinde. Waarabu wakaanza kufa, ikafika mahali wasudani wakawa wanawauliza "Mnataka kupige mshale wapi ?" kama kejeli, Mwarabu mmoja akajibu na kuonesha alama ya jicho akiwa mbali akidhani hawezi fikiwa. Msudani alifyatua mshale na ukamfikia palepale jichoni.

Hii ndiyo ilikuwa vita ya kwanza dola kubwa la kiislamu, lenye maelfu ya askari kushindwa na ufalme mdogo ambao hauna askari wengi. Lilikuwa somo gumu kwa waarabu na wakaamua kugeuza njia kulekea huko Morocco na Tunisia.

=======================================================================
Mifano iko mingi mno, ambayo MADUNYA na MABAZAZI wakiisoma wataelewa, lakini kwasababu watanzania wengi ni wazee wa kupita njia rahisi (Short-Cut) sidhani kama hata watajisumbua zaidi ya kumuuliza Grok na ChatGPT.

ENIWEI ntaendelea...
​
Safi sana
 
Back
Top Bottom