Mwaka 1979, KGB-Vympel walivamia THE TAJBEG PALACE na kumuua Raisi Hafizullah Amin na watu wake. KGB ikiongozwa na Myahudi Bwana Yuri Andropov ilisifiwa duniani kote kwa kufanya oparesheni ya kijasusi ya kisasa kabisa, lakini huu ulikuwa ni mwanzo mkali wa maumivu yao. Waliua viongozi na kulipua nchi kwa miaka 15 mfululizo bila mafanikio yoyote yale, na mwishowe wakanyoosha mikono juu.
Vladmir Putin alijaribu kufanya Oparesheni kama hii mwanzo kabisa mwa vita ya Ukraine kwa kutaka kuteka Airport na majengo ya serikali bila mafanikio. Wengi walitegemea kwamba kinachofuata ni kumuua Zelensky na serikali yake, lakini hakufanya hivyo kwasababu ana uzoefu wa kilichotokea Afghanistan baada ya kumuaa Hafizzulah Amin.
Marekani na Israel wamefanya makosa makubwa kwa kuzichanga karata zao vibaya nchini Iran. Kwenye sayansi ya siasa kuna mataifa ya kisasa (Modern Nation States) kama Tanzania, Marekani na Uingereza na kuna mataifa ya kizamani (Civilizational States) kama Uchina, Israel, India na Iran, ambayo yanatofautiana vibaya mno katika kujiendesha. Usipolifahamu hili utapata matatizo makubwa katika kuelewa jinsi dunia inaenda hivi ilivyo leo hii.
Mataifa ya Kisasa(Modern Nation States), yalianza mwaka 1648 baada ya Mkataba wa Westphalia (Treaty of Westphalia) na yapo kitaasisi, ambapo ili yaweze kuwepo hali ni lazima yetegemee kuanzishwa kisheria (Constitutional Establishment) na kitaasisi, kwamba lazima serikali iwepo (Intact Governing Institutions). Mfano, Tanganyika limekuwa taifa mwaka 1961 baada ya kuanzishwa kisheria, baada ya TANU kurithi taasisi za kikoloni na kutangaza uhuru. Mataifa kama haya yanategemea mno serikali na katiba.
Mataifa ya kale (Civilizational States), yameanza kabla hata ya Westphalia 1648, na yamekuwa yakiongozwa na kushikiliwa na vitu kama Tamaduni, Imani na Utambulisho ambao huanzia kwenye ngazi za familia, koo, kabila, jamii hadi nchi. Mataifa kama Uchina, India, Iran na Israel nguvu yake haipo kwenye taasisi za kisheria za kiutawala kama kwetu sisi, wao sehemu kubwa ya nguvu zao huanzia kwenye taasisi za chini kabisa kama Familia, ambapo kabla ya nchi kutunga na kusimamia sheria, familia ndiyo ina wajibu mkubwa wa kufanya hivyo.
Ndiyo maana wenzetu kama Wachina, Wayahudi, Wahindi na Waajemi wanaogopa kufanya makosa kwa madhara ambayo yanaweza kuikuta familia kuliko yale ambayo serikali inaweza kuyaleta. Wachina na Wahindi hili wanaliita FILIAL PIETY, na ni sheria ambayo ipo kwenye tamaduni zinazofuata mfumo wa Kibudha na Kikonfushasi. Kule Japan mtu akifanya kosa la kudhalilisha familia kuficha aibu anaenda kujiua (SEPUKU). Hili limefanya hizi jamii ziweze kuwa kongwe na kufanikiwa kuishi dunia kwa miaka zaidi ya 4000.
Wayahudi walitawanywa duniani kote, lakini huu mfumo ndiyo uliwafanya wasipoteze utambulishon wao. Utawala wa Myahudi unaanzia katika ngazi ya kifamilia, ule utawala wa serikali unakuja baadaye ili kusaidia jamii nzima katika mambo ambayo wanakubaliana (Collective Goods). Sisi hapa utawala wa nchi unaanzia kwenye ngazi ya serikali kushuka chini. Kila kitu mnaamuliwa na serikali.
Nikupe mfano hai kabisa wa kihistoria dola la Zhou (Zhou Dynasty) lilitawala Uchina kwa miaka zaidi ya 800, ila baadaye likaanguka na kumegeka vipande vya mataifa saba yalikuwa yakipigana vita vikali kwa miaka takribani 200 (The Warring States Period) kutaka kuliunganisha taifa. Kipindi hakukuwa na Central Authority, bali mataifa yaligawanyika kijamiii ambapo wengi walikuwa ni ndugu wa jamii moja. Tofauti na mataifa mengi ya duniani ambapo yakianguka lazima itokee taharuki na giza kama ilivyokuwa kwa Dola la Mrumi, Uchina kipindi hiki yaliyokea maendeleo makubwa ya kisayansi na kijamii kuliko hata ambavyo Uchina lilikuwa taifa moja.
Kitabu cha Art of War kiliandikwa kipindi hiki. Utaalamu wa uhunzi wa kufua chumu ulikomaa kipindi hiki, na mengineyo mengi-mengi ambayo mpaka leo dunia inafaidika nayo. Ikumbukwe Uchina, Israel na Iran wamepitia vipindi vya ombwe la uongozi (Anarchy) bila nchi kuwa na mtawala na jamii zikaendelea na maisha yao mpaka leo hii.
=======================================================================
Hakuna jambo la hatari hapa duniani kama kuingia kwenye vita na mtu usiyemfahamu vizuri.......
ENIWEI sijui kama utanielewa...
A Modern Nation State vs A Civilizational State