Hakuna kauli nyingine za kuombeleza kifo kwa Waswahili zaidi ya hizi

Hakuna kauli nyingine za kuombeleza kifo kwa Waswahili zaidi ya hizi

Kauli za kupeana moyo, kifo ni kitu kizito kuliko vyote kwa maisha ya viumbe wote. Bila kuufariji moyo huwezi kuhimili.
Sema hata tutamkumbuka daima, hatasahaulika mioyoni mwetu, a life well lived...
 
Hadi kauli za vifo zinaleta utata aaah sasa mnataka tufanyeje jama au tutaanza kupiga vigelegele
Wengine wanajiongeza siku hizi wanasema "umejua kutuliza"
 
Namba 5 huwa Nyuma yake mbele yetu mkuu sio ulivyoandika.

Maana yake ni kama mko kwenye foleni, nyuma ya mtu wa mbele yako ni mbele yako wewe, ni kama wote safari yetu moja
Anha, hiyo kauli ni rahisi kujichanganya kama ile ya "mfupa hauna ulimi"
 
Sema hata tutamkumbuka daima, hatasahaulika mioyoni mwetu, a life well lived...
Zote ni kauli za kuufariji moyo, maumivu yanayokuwepo baada ya kumpoteza mtu wa karibu hayawezi kuelezeka.
 
Kila mara mtu anapofariki Waswahili huwa hawakosi hii misemo,

1. Maisha ni fumbo,
2. Tumeumbiwa kifo,
3. Kifo ni kitendawili
4. Tunatembea na kifo
5. Mbele yake nyuma yetu( hii hata huwa sielewei inamaanisha nini)

Mtu anapokufa unatakiwa kusikitikia marehemu na waliobaki, sio kujisikitikia wewe mwenyewe na kuanza kujipa matumaini ya kifo chako.
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.
 
Kila mara mtu anapofariki Waswahili huwa hawakosi hii misemo,

1. Maisha ni fumbo,
2. Tumeumbiwa kifo,
3. Kifo ni kitendawili
4. Tunatembea na kifo
5. Mbele yake nyuma yetu( hii hata huwa sielewei inamaanisha nini)

Mtu anapokufa unatakiwa kusikitikia marehemu na waliobaki, sio kujisikitikia wewe mwenyewe na kuanza kujipa matumaini ya kifo chako.
Ongezea.

Bwana ametoa, bwana ametwaa.

Tulimpenda, ila Mungu amempenda zaidi.

Kila nafsi itaonja mauti.
 
Hii angalau ni sawa kwa maana ya kwamba unamsikitikia marehemu na kumtakia pumziko hasa kama una imani ya kidini.
Hii ndiyo mbaya mbovu kuliko zote. As a matter of fact, hizo zingine hazina tatizo lolote.

Niko tayari kumleta Peter Kibatala awe wakili wangu.
 
Back
Top Bottom