Nitaongelea kwa habari ya binadamu kwanza kabla ya viumbe vingine.
Unaposema mtu, mtu ni nafsi iliyo hai ambayo imehuishwa na roho, roho inayokaa kwenye nyumba inaitwa mwili, so mtu ni mtu either yupo kwenye mwili or nje ya mwili wake, Na roho ilitoka kwa Mungu anayeishi Milele.
Sema mafundisho mengi makanisani watu wameaminishwa wao ni damu na nyama yaani mwili upatikanao na mauti ambao ki uhalisia ndio mavumbi ambayo hurudi ardhini ndio sababu baba yetu wa kwanza kuitwa Adam kwa kumaanisha udongo/mavumbi (Adama in Hebrew).
Na ndio maana hatuwezi kumpendeza Mungu ikiwa tutakuwa watu wa mwili kwa kuwa Mungu mwenyewe ni roho ila isiyo na mwili wa damu na nyama (sijasema isiyo na umbo) hivyo anaabudiwa na kupendezwa katika roho na kweli tu.
Na kwa sababu ya mchanganyo kutoka kwa mafundisho mbalimbali watu wameshindwa kutambua Identity yao kuwa they are not flesh
Ndio maana utashangaa kwanini watumishi wa Shetani wanaujuzi mwingi wa mambo ya rohoni kuliko wanaoamini Mungu ni kwa sababu wanatambua mtu sio damu na nyama ni roho au nafsi iliyohuishwa inayoishi kwenye mwili wa udongo, najua watu wenye elimu ya falakhi wanaelewa vizuri zaidi nini namaanisha kuliko wale Wanaomwamini Mungu kwa sababu kwao ni kitu kigeni kufunuliwa lakini hapa ndio kwenye siri zote za rohoni na nguvu zisizo na ukomo za uhai.
Ndio maana yesu alimjibu shetani mtu hataishi kwa mkate tu ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu maana yake ni kwamba chakula cha mtu halisi wa ndani ambaye ndio wewe (nafsi hai, roho) sio mkate wala kande wala ugali ni maelekezo ya roho ile iliyokuumba (Mungu) ndio chakula chako, hapa lengo la shetani ilikuwa ni kutaka kumuaminisha Yesu kuwa yeye ni mwili hivyo asipokula atakufa, kitu ambacho ni kweli mwili usipolishwa mkate (chakula cha kimwili) unakufa, lakini Yesu alijitambua yeye sio mwili na hafi kwa kukosa mkate labda maneno ya Mungu ambayo ndio maelekezo ya jinsi itupasavyo kuishi
Note: Kilichozaliwa na mwili ni mwili na kilichozaliwa na roho ni roho, Mwili hauzai roho, wala roho haizai mwili.
Mwili hurudi mavumbi roho humrudia yeye aliyeitoa.