Hakuna kitu kinaniuma Kama ndugu zangu wote kuzalia nyumbani

pole hii changamoto ni ya wengi sio wewe tu
 
Hao nao si wana dada zao.
#ifyoudontgetitforgetaboutit
 
Sisi wanaume maranyingi tunajuaga tabia za wadada tunaodate nao kama ni mbaya au nzuri,na tukijua dada flani hajatulia,hatumwambii kua anatabia mbaya,ila tunamtongoza ili tupate huduma,na hatumwambii kua tunataka tulale nae tu,hapana bali akiuliza kama tutamuoa,tunamjibu ndiyo,ili tumle tu,ila moyoni tunajua huyu ni kicheche siyo wa kuoa,muda ukienda,mdada anaacha hata kuchukua tahadhari ya kukwepa mimba,mwisho wa siku anaibeba mimba,mwanaume anakataa kumuoa,anasema ntalea mtoto ila siyo kukuoa.
Wadada wengi ambao hawajaolewa na wana watoto,wanajua makosa ambayo wanayo kitabia,na wengine familia zao zinajua kua watoto wao hawajatulia,hivyo hawalaumu watoto wao kutoolewa.MALEZI JAMANI.
 
Watu wengi hawajui hii kitu....

Unaweza Kuta dada zake wametulia, wanasifa zote za kuwa wake. Na wanapata watu wenye Nia kweli na wao wanakuwa tayari kuwa wake na kuwa mama.....

Ila kaka zao wanachezea dada za watu huko.....Karma inarudi. Hapo Sasa inawakuta dada zake, Hadi wadada wanabaki kujiuliza wanakosea wapi na kosa hawalioni.

Lakini pia...Maji hufuata mkondo historia ya familia ipoje...kama hakuna kuoa oa au kuolewa olewa inakuwa ni changamoto, ni kukaa karibu sana na Mungu kuvunja Hilo suala bila hivyo mambo yataendelea kizazi na kizazi.

Ndio unakuwa watu wanasema familia ile Huwa hawaolewi, au familia ile Huwa hawadumu kwenye ndoa.

Wakati mwingine ni kuangalia kiini Cha tatizo na kuvunja hiyo minyororo inayotufuata.
 
Halafu wee jamaa hauko kwenye ile crew ya kataa ndoa wewe? Sasa hiyo imerudi kwa masista
Huyo Ndio kinara kwenye iyo crew nashangaa leo analalamika dada zake hawaolewi wanazalia nyumbani.
Na katika crew yao kauli mbiu yao usioe tafuta mwanamke piga mimba sepa,leo wahuni wenzake wamemzunguka amepigiwa mimba dada zake
 
Familia anayotoka mwanamke ina mchango mkubwa sana kumpandisha binti soko la kuolewa.

Tazama mabinti wengi wanaotoka familia zilizoelimika.. ama za uchapakazi.

Hao mabinti kuolewa ni fasta sana labda wakatae wenyewe.

Pia wale mabinti wanaokuwaga best student vyuoni.. nao ofa za ndoa wanazipata fasta tu.

Tazama mabinti wale wafanyakazi wa Big 4 auditing firms pwc, kpmg, delloitte , ama ey uone kwa nini wanaolewa fasta. Na wana ofa za ndoa kibao.. sababu kuu ni brain factor
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…