Hakuna kitu kinanyima raha kama kuzaliwa peke yako

Hakuna kitu kinanyima raha kama kuzaliwa peke yako

Kuzaliwa na ndugu sio ishu hiyo. Mimi nina ndugu wengi na hata hatuna ushirikiana yaan kila mtu na mambo yake. Muombe Mungu akupe watu sahihi katika maisha yako. Ndugu unawezakuwa nao na hawana faida yeyote
Mnaweza kuwa wengi na ikawa afadhali ya aliezaliwa peke yake, ndugu wengi ni wazuri sana mkiwa wadogo ila mkishakuwa wengi ni mtihani.
 
Wazazi wangu wakati wanaongeza wadogo zangu nilikuwa nachukia, lakini sasa miongoni mwa vitu nikiwaza vinanipa raha ni hawa machalii wangu.

Mungu akikupa neema ya kuwa na familia barikiwa watoto wa kutosha utapata raha kama unavyofikiria.
 
Wengi sanaa wawili! Ndio maana napenda kuolewa na single faza nimkute na watoto tayari ili asiniambie habari za kuzaa watoto 6
Nipo hapa,nna watoto wawili tayari bado wawili na wewe.mimi nataka watano,Mmoja nitajua mwenyewe kwa kumtoa.
 
Hakuna kitu kinaninyima Raha maishani kama kuzaliwa peke angu kwenye tumbo Moja🥺
Najua ni mipango ya mungu ila huwa naumia sana
Natamani ningekuwa na ndugu wa Damu hasa wa kike Wa kushare nae mambo yangu binafsi kwenye shida na raha kwa sababu Kuna mambo ambayo kabla mtu huja-share na mzazi au mwenza wako ni lazima umhusishe ndungu yaki., ila ndo hivo ndugu niliyenae ni mmoja na ni wa kiume (ni mtoto wa baba.
Huwa nawaza pindi mungu akiwachukua wazazi nitaishi vipi?
Namuomba sana mungu ANIPE uzao I hope wanangu watakuwa ndugu zangu🥺
Naandika haya nikiwa na masikitiko makubwa coz Kuna jambo linanitatiza hapa ila ndugu wa ku share nae Sina.
Dah!
Bado una nafasi ya kutafuta ndugu
 
Back
Top Bottom