Yaani unaamka halafu hauna mishe zozote au mishe ulikuwa nazo zinegoma aisee inapain sana.
Nilipitia hii hali basi bwana nilipopanga chumba unaona vyumba vya majirani zako Wanaamka Mapema wanaenda mishe kurudi jioni Mimi nipo tu
Hii hali ilinitesa sana kutokuwa na mishe full no respect mtaani yaani unaona kabisa hapa hii kwakuwa sina mishe
Basi bwana, nikaona nisiwe boya nikaanza nami kuamka mapema naoga na vaa vizuri naondoka kumbuka sina kazi yoyote hapo naenda mjini
Naenda zangu mjini kuzurura kumbuka kama hauna mishe jua linachelewa kuzama hatari
Mimepiga hiyo kitu kama miezi mitatu heshima nilipokuwa nakaa ikarejea kidogo, mabinti walikuwa wengi hapo napoishi wakawa wananiambia eeh sikuizi umepata mishe hongera Mimi najibu si unajua tena, kumbe wangejua nazurura tu mjini huko
Nifupishe, katika kuzurura kwangu nikapata Dili hilo Dili ikanipa Hela kidogo hiyo Hela nikaona fursa huko huko mjini nikatembea nayo
Tutoke maghetoni vijana Dunia Haina huruma na mtu asiyekuwa na shughuli ya kumwingizia kipato
Kama ushapitia hali hii pita hapa toa experience yako ilikuwaje
Mungu awapiganie Wote wanaoamka Asubuh halafu sehemu ya kwenda hawana wapate mishe🙏🏿🙏🏿🙏🏿