Hakuna kitu tunachogusa, kushika wala kukanyaga – kugusa ni udanganyifu wa akili

vitu havijaundwa na pure atoms.
ni wapi nimesema kuwa Mwili umeundwa na pure atoms.?
kwa mfano mwili wangu umeundwa na molecules ama compounds ambazo hazina chaji yoyote
siyo mwili wako tu umeundwa na molecules (Molekuli) ama compounds ni mwili wa binadamu na myama yoyote yule


ni kweli kabisa — hakuna ubishi kwamba mwili wa binadamu umeundwa na molekuli (molecules) na (compounds) kama maji (H₂O), protini, mafuta, n.k.

Lakini hoja yangu haipingani na hiyo. Badala yake, hoja yangu inatokana na ukweli wa kisayansi kwamba hata hayo molecules, compounds, au hata seli zetu — MWISHO WA SIKU — zote zimeundwa na atomi.

Sasa turudi kwenye msingi wa mjadala wangu


Kulingana na fizikia ya kisasa (Quantum Physics), haswa maelezo yaliyotolewa na makala ya Futurism yenye kichwa “Why Physics Says You Can Never Actually Touch Anything”

Kwa hiyo, mhogoz
hata kama molekuli (Molecule) hazina chaji kamili, bado elektroni ndani ya molekuli (Molecule) hizo haziwezi kuruhusu kugusana moja kwa moja.

Tunachokihisi kama “kugusa” ni tafsiri ya ubongo kutokana na msisimko wa neva, siyo mgusano halisi wa vitu.

Kwa ufupi:​

  • Molekyuli = kundi la atomi
  • Atomi = zina elektroni
  • Elektroni = hazigusani moja kwa moja (zinajikwepa kwa nguvu ya sumakuumeme na kanuni ya quantum)
 
Kwa logic hii atom zako nazo hazigusani na wewe haupo.
 
Bora ungeandika kidhungu labda ningeelewa😴
 
Kwa logic hii atom zako nazo hazigusani na wewe haupo.

Ndiyo, kwa maana ya kina — we do not exist, Sisi ni viumbe wa kiroho tunaopitia uzoefu wa kibinadamu.

Kila kitu tunachokiona, kugusa, au kuhisi ni tafsiri ya akili yetu juu ya mitikisiko ya nishati (energy vibrations).

Katika kiwango cha atomiki, hakuna kitu kinachogusana na kingine.
Atomi zinaonekana kuwa na umbo imara, lakini kiukweli asilimia 99.999999% ya atomu ni tupu.

Kile tunachokiita 'Matter' au 'vitu' ni (electromagnetic fields) held together by fundamental forces of nature
Hii ndiyo maana physicists say: “matter is an illusion.
 
Somo lako latufunza jambo lipi ndugu mwandishi
 
Somo lako latufunza jambo lipi ndugu mwandishi
Somo ni:
Ubongo wako ndiyo unaotengeneza hisia za kugusa au kushika kitu — lakini kiuhalisia, kulingana na asili ya mazingira yetu (nature of our reality), hakuna mguso wa kweli unaotokea. Hakuna kitu kinachogusana kabisa.


Kwa ufupi:
  • Ubongo = Mtafsiri wa uhalisia (interpreter of reality)
  • Na Wewe ≠ (siyo) Ubongo
 
1. Katika ngazi ya kimwili; mguso wa unyayo na ardhi ni kitu halisi
ndiyo, tunahisi kama tunagusa, tunatembea, tunakanyaga… Huo mguso unahisiwa kwa sababu ya ishara zinazotumwa na mishipa ya fahamu hadi kwenye ubongo, na hapo ndipo tafsiri ya "mguso halisi" huzaliwa.

2. Katika ngazi ya atom; mguso huo ndo hutafsirika ni udanganyifu
hakuna kitu kinachogusana. Elektroni kwenye unyayo wako na zile kwenye sakafu ya ardhi zinakinzana (repel each other) kwa kutumia nguvu ya umeme (electromagnetic force), hivyo hazikai pamoja au kugusana hata kidogo.
 
Umeshasema kwenye kiwango cha atom (yaani at atomic level)

Sasa nikuulize je wewe ni atom au ni mkusanyiko wa billions of atoms ?

Ndiyo, mimi si atom moja — mimi ni mkusanyiko wa mabilioni ya atomi. Lakini jambo muhimu hapa ni hili: ukiuchambua mkusanyiko huu hadi ngazi ya msingi zaidi (atomic level),
bado sheria zile zile za kutogusana zipo.

Hakuna sehemu yoyote ya huo mkusanyiko inayogusana na nyingine kimwili.

Kwa hiyo, hata kama sisi ni "mkusanyiko wa atomi", bado msingi wa uhalisia wetu umejengwa juu ya kanuni za electromagnetic repulsion — ambazo ndizo zinazofanya ionekane kana kwamba kuna mguso, ilhali kiuhalisia hakuna.

Hivyo, hoja yangu inabaki palepale: kile tunachokiita "kugusa" ni tafsiri ya ubongo wetu, si mguso wa kweli katika kiwango cha atomu.
 
hakuna kitu kinachogusana. Elektroni kwenye unyayo wako na zile kwenye sakafu ya ardhi zinakinzana (repel each other) kwa kutumia nguvu ya umeme (electromagnetic force), hivyo hazikai pamoja au kugusana hata kidogo.
Of course 😊
 
Kwamba uchukue magnet north pole na nyingine south pole itatokea repulsion at their surfaces

Au wewe udumbukie kwenye concentrated sulfuric acid utahisi tu mgusano sababu ya repulsion ?

By the way if that is the case kwanini ukifunga break kwa kasi ngozi ya miguu inachubuka sababu ya friction kama hakuna mguso wowote ?

Nadhani mkuu unachanganya concepts
 
Ok,kuna mwanasaikolojia nilimsikia katika chombo cha habari kimoja,mwanadamu ni software,huu mwili wa nyama ni kasha tu,mtu yu ndani yake,haonekani,na kinachokufa ni huu mwili si mtu,mtu ni yule tumtambuae kwa alama ambazo aliacha,.nadhani hii yalandana na usemacho.
 
Daah nipo nawaza inamana nikiwa na mama chanja atoms za nanihii yake hazigusani kabisa na atomu za nanihii yangu...sasa inakuwaje wazungu wanatoka na raha naskia na kutunga mtoto?? Au ni illusion tu
 
kwa maneno yako ni kama unataka kusema unavooga maji hayagusi mwili. au ukimwaga maji kwenye unga hauloi maana chembechembe hazigusani, si ndio?? sasa kwanini sukari na chumvi vunayeyuka kwenye maji? Ukinijibu hapo na kueleweka nitakua mwanafunzi wako kuanzia leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…