Hakuna kitu tunachogusa, kushika wala kukanyaga – kugusa ni udanganyifu wa akili

Daah nipo nawaza inamana nikiwa na mama chanja atoms za nanihii yake hazigusani kabisa na atomu za nanihii yangu...sasa inakuwaje wazungu wanatoka na raha naskia na kutunga mtoto?? Au ni illusion tu
• KATIKA NGAZI YA TISHU: Unachohisi (experience) ni uhalisia, unapojamiina vichochezi huzalishwa (eg: dopamine) na taarifa husafarishwa na neva (receptors) kwenye ubongo kwa tafsiri, hivyo raha unayopata ni halisi, sawa tu na mtu anayejichua au aliyeungua, si kwamba ni udanganyifu, hisia tunazo-experince zinazohusisha vitu vikubwa zaidi (mfano: mifumo, viungo, homoni nakadhalika) ni halisi

• KATIKA NGAZI YA ATOMU: Hakuna hisi wala fahamu, kukosekana kwa tambuzi katika ngazi hii kunafanya vitendo tunavyo-experience katika ngazi ya tishu (mfumo) vitafsiriwe kuwa ni udanganyifu licha ya michakato kuanzia katika ngazi ndogo sana, hivyo unapoungua/unapojamiiana atomu huwa hazi-experience chochote - atomu kama atomu haina mfumo wa neva, hivyo hakuna kitakachotafsiriwa, isipokuwa zikiwa nyingi mno kiasi cha kuunda molekuli -> tissue (umbo kubwa)
 
ENERGY IS REAL...EVERY THINGS IS ENERGY...EVEN MATTERS
 
Sasa why mada isiende kwenye huo mtiririko badala ya kujaribu kuikatisha kwa kuikosoa na sio kujazia/kuendeleza/kuichambua?

Leteni elimu…
 
Hii concept huo sikubaliani nayo. Reality ni reality, mfano nikikukata kidole nikakitoa haijalishi uta perceive kidole bado kipo au hakipo ila in reality kidole hakipo
Sawa lakini, hujawahi kupata ndoto ambayo kwa kiasi fulani mpaka leo unahisi Kama vile ilikua “halisi/real” kabisa?

Sasa ni kipi kinatenganisha ulimwengu unauona “ndotoni “ na huo unaouona ni uhalisia?

Ipi hapa ni ndoto? Uliyoamka kutoka ama uliyoamka kuingia?

Uhalisia/Reality ni nini?
 
Hapana, kwa nilivyoelewa hivyo vyote ulivyosema vinatokea kwenye ulimwengu ambao uko controlled na consciousness (main & sub),

Lakini kwa mujibu wa hii mada; at the Creator’s realm hakuna chochote zaidi ya experience tu.

Mada inatutoa nje ya box kabisa, inatupa nafasi ya kuangalia ndani yake kutokea popote kwa sababu hakuna limit katika UWEPO wetu.
 
Tafuta mahali kuna jiwe kubwa, kslibamize kwa gari ukiwa speed 180 . Then tuletee majibu
 
Wakuwahishe hospitali, huenda ukapona
 
Sawa the brains can play tricks on you kwenye ndoto au hallucination lakini hiyo haifanyi kuwa ndo uhalisia wote, hatuwezi wote kuwa tuna experience same hallucination alafu tunaita reality, kuna theory moja "egg theory" sijui itakuwa ndo hyo au nachanganya kwamba duniani upo wewe tu na wenginge wote unaowaona ni construct ya imagination yako, sasa nani ambaye ni imagination ni mimi au wewe au yule, haina maana. Mimi ndo maana idea yoyote inayosema sijui kila kitu ni illusion au sijui tunaishi kwenye holographic universe huwa sikubaliani nayo. Lakini huo ni mtazamo wangu tu kutokana na ninachojifunza na experince nliyonayo
 
Aliyekwambia kugusana ni mpaka atom zigusane ni nani ?
Sijawahi kusema kwamba lazima atom ziguse moja kwa moja ndiyo pawe na mgusano.
Nimeeleza kwamba kile tunachokiita “mgusano” ni tafsiri ya macroscopic ya interaction za nguvu katika kiwango cha atomiki, hususan electron repulsion — na hii ni msingi wa “touch” katika physics ya kisasa.


Kwamba sharing of electrons sio mgusano
Sharing of electrons ni sehemu ya chemical bonding, sio physical touch.

Ni interaction ya interaction of energy and force kati ya atomi mbili zinazoshiriki electrons kuunda molekuli.
Hii ni tofauti na “touch” inayohusisha electron repulsion badala ya kuunganika kwa orbital kama inavyotokea kwenye covalent bonds.


alafu huwezi ukaleta rules at atomic level (quantum reality) kwenye molecular level; thing behave differently
Si kwamba naleta quantum rules moja kwa moja kwenye molecular level, ila ukweli ni kwamba molecular behavior inatokana na atomic behavior, nayo inategemea quantum rules.

Mfano mzuri: molecular bonding kama covalent au ionic bonding zinategemea electronic structure — ambayo inafafanuliwa na quantum mechanics (k.m. electron orbitals na energy levels).


Kwahio wewe unafunction na dunia inafunction at an atomic level ?; are the rules the same ? Can you even know where an atom is at any given time
Tunachokiona na kukitenda kwa kiwango cha juu (macroscopic) ni matokeo ya interactions za kiwango cha chini zaidi (atomic).

Dunia haifanyi kazi kwa kanuni zile zile kila level, lakini kila level inajengwa juu ya nyingine.

Sisi hatujui location sahihi ya atomu moja kwa moja (Heisenberg uncertainty principle),
lakini hatuhitaji kujua hivyo ili kuelewa behavior ya mfumo mzima (emergent properties).



Sileti kwa kuchanganya — na wala siyo makosa kuhusisha.
Molecular reactions zinatokea kwa sababu ya electron exchange au redistribution, jambo linalotegemea atomic structure.
Na atomic structure linategemea quantum behavior ya electrons. Hivyo, kueleza mabadiliko ya molekuli bila kutambua msingi wa atomic na quantum ni kuacha maelezo nusu.
 

Unapokaa kwenye kiti:
  • Haumaanishi atom zako zimegusana na za kiti.
  • Kinachotokea ni kwamba electrons katika atom zako zinakutana na electrons za kiti, na kwa kuwa zote zina chaji hasi, zinakataa (repel).
Hii ndiyo inatufanya tusizame kwenye viti — si kwa sababu kuna mgusano wa moja kwa moja, bali ni kwa sababu ya electromagnetic repulsion.
 
Alaaaa hahahahahaha aahhhh yaaan Mwanangu utafiti wako unaandiksa mistari mitano tu Tena Ndani ya JF

Hapa nimeshika simu yangu, Niko natype ,kumbe ni Hisia zangu tu ila sijashika simu🤣🤣🤣
 

halisia ni kile tunachokipitia (experiencing) kupitia fahamu zetu.

Ndoto inapotokea, ubongo huunda mazingira ya hisia, maumivu, furaha, hofu — kila kitu felt real. "halisi."

Vivyo hivyo, hata hali ya kuamka ni tafsiri ya data inayopokewa na ubongo kupitia milango ya fahamu (macho, ngozi, masikio n.k.).

Kama hivyo basi,
halisia ni (electrical signals) tu zinazotafsiriwa na ubongo wako
 
Sasa why mada isiende kwenye huo mtiririko badala ya kujaribu kuikatisha kwa kuikosoa na sio kujazia/kuendeleza/kuichambua?

Leteni elimu…
Angepeleka mada hivyo wala nisingesema nilivyosema (kumuuliza je wewe ni atom ?) sababu at atomic level things behave differently na huwezi uka apply same rules at molecular levels; kwahio mimi nimejaribu kumrekebisha asichanganye concepts....
 
Nope ninachoongelea hapa ni kitu ambacho huyu jamaa amegusia kwamba katika atomic level (na hapa tukiongelea atom naomba upate vision ya kitu kidogo sana ambacho mostly ni empty space in so far as ukiweka atoms zote za dunia ukiondoa ile empty space huenda zisiwe kubwa zaidi ya punje ya mchanga); Sasa behaviour ya hizi atom uzilete na kusema kwamba kiumbe ambacho ni billions of atoms kita behave the same..., kitu ambacho ni misleading na tunaelewa kabisa things behave differently in quantum mechanics

Kwahio siku ukileta mada inayosema hivyo specifically unavyosema wewe niite ili tuone merits and demerits of what you are saying
 
Hapa nadhani umeleta content without context


Na kwa ufupi ni kwamba at Atomic Level At the atomic level, matter exhibits behaviors distinct from our everyday experiences due to the principles of quantum mechanics. This includes the wave-particle duality of matter, where particles like electrons can also behave as waves, and the inherent uncertainty in their properties. Furthermore, the act of observation can influence the behavior of these particles, leading to phenomena like quantum entanglement.

By the way kama ni kweli usemayo basi dunia hii vitu vingekuwa havina wear and tear sababu friction ingekuwa haipo..., and what is touch ? hata kama ni nguvu magnetically bado hio ni touch hata kama ni upepo unakusukuma hio bado ni touch; na vilevile atoms do collide (soma what happens when atoms collide)
 
So it is safe to say Reality is the outcome of how we feel/perceive/think/wish?
 
Nini ni halisi? (real)
halisia ni (electrical signals) zinazotafsiriwa na ubongo kupitia milango ya fahamu kama vile macho, masikio, pua, ulimi na ngozi.


Uhalisia ni nini? (reality)
Uhalisia ni halisia pepe (virtual).

Asili ya mazingira yetu katika kiwango cha quantum inaonesha (subatomic particles) zina tabiaya kuwa mawimbi (waves) unapokuwa huyaangalii (perceive),
lakini hubadilika na kuonekana kama chembe halisi unapoyaangalia unavyotafsiri (perceive).

Fikiria hili: Mti ukianguka msituni na hakuna anayeusikia, je, unatoa sauti?


So it is safe to say Reality is the outcome of how we feel/perceive/think/wish?
"ni salama au vizuri kusema kwamba uhalisia ni matokeo ya jinsi tunavyohisi, (perceive), tunavyofikiria, na tunavyotamani?"

Ndio na hapana.
Jinsi unavyohisi, unavyotafsiri (perceive), na unavyofikiria — hiyo ndiyo huunda uhalisia wako binafsi kwa wakati uliopo.(reality)

Lakini la, kile unachokitamani (wish) kimejengwa katika mawazo yako, si katika hali halisi ya sasa. Kinaweza kuwa halali kihisia, lakini si uhalisia kwa wakati uliopo.

Fikiria hili: Nini tofauti kati ya ndoto na uhalisia huu tunaouishi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…