Coach Slamah Hamad
JF-Expert Member
- Nov 12, 2014
- 3,810
- 5,043
Kwenye ku wish (nashindwa kusema kutamani maana haileti maana ninayoikusudia)halisia ni (electrical signals) zinazotafsiriwa na ubongo kupitia milango ya fahamu kama vile macho, masikio, pua, ulimi na ngozi.
Uhalisia ni halisia pepe (virtual).
Asili ya mazingira yetu katika kiwango cha quantum inaonesha (subatomic particles) zina tabiaya kuwa mawimbi (waves) unapokuwa huyaangalii (perceive),
lakini hubadilika na kuonekana kama chembe halisi unapoyaangalia unavyotafsiri (perceive).
Fikiria hili:
Ndio na hapana.
Jinsi unavyohisi, unavyotafsiri (perceive), na unavyofikiria — hiyo ndiyo huunda uhalisia wako binafsi kwa wakati uliopo.(reality)
Lakini la, kile unachokitamani (wish) kimejengwa katika mawazo yako, si katika hali halisi ya sasa. Kinaweza kuwa halali kihisia, lakini si uhalisia kwa wakati uliopo.
Naam; huwa inanifikirisha sana, kwamba uhalisia Halisi ni upi?Fikiria hili:
"Nini tofauti kati ya ndoto na uhalisia huu tunaouishi?"
Naam;
huwa inanifikirisha sana, kwamba uhalisia Halisi ni upi?
Uhalisia halisi ni huu tunao experience kwnye maisha ya kila siku physical realty (3D), Lakini hilo halimaanishi kwamba ndoto siyo halisia.uhalisia Halisi ni upi?
fikiria hili:Je? Tunaamka toka ndotoni ama tunaamka kutoka kwenye uhalisia kuingia ndotoni?
Katika quantum level, vitu havipo kama tunavyoviona hadi pale vinapotazamwa — hali inayoonesha kuwa mtazamaji (conscious observer) huunda uhalisia.Kwamba inafaa iangaliwe kinyume:
Tunayoona ndio Maisha halisi ni ndoto huku ndoto ikiwa ndio uhalisia wenyewe?
ni (head chemist) wa ubongo (mind)— ndiye anayechochea mchakato wa kuunda halisia.Kuamini/Believe ni nini?
Kuamini ni msingi wa kila halisia unaotengenezwa na ubongo wako kuwa uhalisia.Kwanini ni muhimu kuamini/kujiamini ili jambo fulani liende lilivyokusudiwa?
So it is safe to say Reality is the outcome of how we feel/perceive/think/wish?
Kwenye ku wish (nashindwa kusema kutamani maana haileti maana ninayoikusudia)
Wish ile ambayo unaweza kuitafsiri Kama Manifesting/Manifestation.
Hii unaizungumzia vipi?
So it is safe to say Reality is the outcome of Manifesting/Manifestation?
Shukran kwa elimu.Swali lako sasa kwa kiswahili nadhani litakuwa hivi
Kwa hiyo, ni sahihi kusema kwamba uhalisia ni matokeo ya kudhihirisha (manifesting)?
ni kweli,
uhalisia ni matokeo ya kile ambacho ni halisia ndani ya akili yako (Mind).
Kupitia bidii, juhudi, na kujitahidi, kile kilichokuwepo ndani kinadhihirika (manifestation) katika maisha yako halisi jinsi unavyotamani yawe.
Hapo peusi zaidi, please elezea zaidi. Ruhusa kutoka kwa Nani?ni (head chemist) wa ubongo (mind)— ndiye anayechochea mchakato wa kuunda halisia.
Kuamini ni msingi wa kila halisia unaotengenezwa na ubongo wako kuwa uhalisia.
Ubongo hauwezi kuunda njia mpya za neva (neural pathways) bila “ruhusa” kutoka kwenye imani ya ndani ya mtu.
Ni kwamba ubongo hauwezi kutambua mazingira ya kuhitaji kujisimamia, hasa kwa kulazimika? Survival mode instincts?Kwa mfano, mtu aliyepata ajali na kupoteza uwezo wa kutembea — kama haamini kuwa anaweza kurudia kutembea, mwili wake haupati mwongozo wa kuanza kujijenga tena,
kwa sababu tayari ubongo wake unafanya kazi ya kutengeneza uhalisia mpya kwamba haiwezekani kutembea tena.
Katika kiwango cha atomu, wazo la "kugusa" (touch) ni udanganyifu.
Atomu nyingi zina nafasi tupu, zikiwa na kiini kizito katikati na wingu la elektroni.
Unapojaribu kugusa kitu, elektroni katika atomu zako na atomu za kitu hicho zinakataa kukaribiana (repel each other)
kwa sababu ya nguvu ya sumakuumeme.(electromagnetic force)
Kwa kuwa zote zina chaji hasi, hazijawahi kugusana moja kwa moja.
Unachokihisi kama kugusa ni msukumo wa kielektroni kati ya atomu zako na atomu za kitu hicho.
Kwa uhalisia, "kugusa" ni mwingiliano wa nguvu zisizoonekana(invisible forces),
si chembechembe kukutana kimwili.
Tunadhani Tunashika, Lakini Kiuhalisia Hatugusi Chochote, hakuna kitu kinachogusana na kingine.
Fikiria hili: hata unapotembea, hukanyagi ardhi kimwili