Hakuna kosa wala dhambi kumkumbuka Magufuli, aliiweza nchi, kwa sasa kuwa na uhakika wa mambo ya kesho, haijulikani

Hakuna kosa wala dhambi kumkumbuka Magufuli, aliiweza nchi, kwa sasa kuwa na uhakika wa mambo ya kesho, haijulikani

Miaka aliyotawala ni michache sana na Angalau aliweza kujenga hicho alichokijenga. !
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni !
Msema kweli mpenzi wa Mungu .
Lakini pia alikuwa na mapungufu yake kama binadamu !🙏🙏
Ni nani aliyekaa miaka mingi na hakufanya kitu? Nitajie Rais yeyote kati Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwette.

Kama umezaliwa baada ya 1990s nitakuelewa. Ila kama umezaliwa 1980s and before utakuwa na mtindoo wa ubongo
 
Asingekufa mwamba lami ingekuwa imefika hapa kwetu na kupita kwenda huko kituo cha treni mpya.

Japo uliniumiza mahali ila ninakukumbuka

Rest very Easy Mwamba
 
Asingekufa mwamba lami ingekuwa imefika hapa kwetu na kupita kwenda huko kituo cha treni mpya.

Japo uliniumiza mahali ila ninakukumbuka

Rest very Easy Mwamba
Mkuu, wewe leo umekuwaje chief, ni wewe mwenyewe kweli au wezi wa I'd wamekufanyia uhuni?
 
Ni nani aliyekaa miaka mingi na hakufanya kitu? Nitajie Rais yeyote kati Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwette.

Kama umezaliwa baada ya 1990s nitakuelewa. Ila kama umezaliwa 1980s and before utakuwa na mtindoo wa ubongo
Mwenye macho haambiwi tazama !
Huo ni mtazamo wangu tu ! 🙏🙏
Mimi nimezaliwa 1951 🙏🙏
 
Inashangaza watu wanaponda utawala wa Magufuli, na wakiona huu wa sasa ni bora zaidi. Unafiki.
 
Ni ujinga kulazimishwa eti tusikumbuke uzuri wa ilivyokuwa awamu ya Magufuli

Ni ujinga kuendelea kutiana moyo kwamba, eti tupo pazuri na tunaelekea pazuri zaidi

hivi, Magufuli alitumia miujiza gani kwenye suala la Umeme na mgao kutokuwepo?

Yeye alifanyeje kumeneji suala la mlipuko wa bei za vyakula mbali na kuwa kwenye janga la Korona dunia nzima?

Alitumia mbinu gani kufanya nishati ya mafuta isipande na nauli kuwa juu, licha kwamba kipindi cha Korona meli nyingi zilipaki?

Sukari nayo imeshindikana sasa kushuka licha ya kuwa na kiwanda cha Bagamoyo sugar na kikubwa kulikoni vyote East Africa, sukari kg 4000 mpaka 4500, kweli???

Tunatafutana nini hapo?

kila mtu anayetokea mikoa ya mbali atakubaliana nami kwamba, kwa sasa suala na safari kutoka mkoa hadi mkoa, ni kama adhabu ya ndogo ya jehanamu

Kutoka kuwa na nauli ya tsh 70,000 kwenda Bukoba hadi 100,000+

Kutoka nauli ya 300 jijini Dar hadi 900 na 1100??

Halafu kuna mpuuzi mmoja anaendelea kusema ni sawa?

Kutoka kuwa na matibabu ziro kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 0 hadi 5, leo ni pesa??

Kutoka kuwa na umeme 27,000 wa REA hadi kutojulikana kama kuna REA au hakuna, maana bei ni ileile 310,000, bado kuna mjinga anaona ni sawa?

Tusikumkumbuke Magufuli kwa sababu ya wajinga wachache aliowatimua kazini?

Kwa sababu tu aliwadhibiti waliokuwa wanajilipa mapesa kupitia watumishi hewa?

Hao ndio watufanye tusisemee mazuri hayo kwa sababu ya matusi yao mitandaoni?

Mnataka tuwasifu kwenye lipi sasa ikiwa kila kitu kimepanda bei?

Watu hawalazimishwi kusifia, wafanyie mambo mazuri wakusifu, kwa sasa tusifu nini na tumsifie nani na kwa lipi?

2025 nayo ile palee, kila kitu kimegoma kurudi mahali pake,, mtatuambia nini wapiga kura sisi?

Tisheti na kanga?

Na bahati mbaya hata makanisani na misikitini huwa mnakwenda kumzuga padri, Asikofu na shekhe ili hali mkijua njia yenu ni ovu kuliko waovu wote, mnasubiri muibe kura 😂 na mjitangaze mmeshinda kwa kishindo!!

Mnakula mema ya nchi mkiendelea kuwahadaa wananchi walala hoi kwamba mnawatengenezea maisha bora? Njia zenyewe ndio hizo za kupandisha gharama kwenye kila bidhaa??

Mungu ilinde Tanzania kwa mkono wako wa chuma!

Uwabariki viongozi wetu waçhache wanaomaanisha kuwatumikia wananchi
mhhhh....
 
Back
Top Bottom