Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
HAKUNA MAISHA MAGUMU ZAMA HIZI, KILICHOPO WATU WA SASA KUPENDA USAWA.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel.
Hakuna maisha rahisi Kama ya Zama hizi. Siku hizi kila kitu kimerahisishwa. Sijazaliwa zamani Sana Ila miaka ya 2000 Kurudi nyuma maisha yalikuwa complicated, yalikuwa magumu jamani.
Sio kwenye chakula, sio kwenye mawasiliano, sio kwenye makazi, sio kwenye usafiri, sio kwenye Huduma za kijamii. Maisha yalikuwa Magumu mno tena Sana.
Kwa watu waliokulia vijijini wataungana na Mimi kuwa Maisha ya sasa hivi ni rahisi yaani laini Kama unakunywa uji tuu.
Zamani ilikuwa ni Bora ukimbilie mjini ukalale njaa mjini kuliko kuishi kijijini ukila ukashiba.
Maisha ya sasa sio magumu Ila kinachoendelea ni Vijana wa Zama hizi Kupenda USAWA usiowezekana.
Ukitaka maisha yawe magumu penda USAWA usiowezekana.
Ati masikini Kama Taikon unataka uishi Sawa na Tajiri MOO! Hapo lazima maisha yawe complicated.
Zamani kunywa chai na sukari ilikuwa mbinde, walikuwa wanakunywa watu wenye pesa au wenye unafuu.
Nakumbuka Sisi badala ya kunywa chai yenye sukari tulikuwa tunakunyaa Uji WA chumvi.
Na tulikuwa tunaona ni Sawa Kabisa.
Siku hizi ni ngumu siku mbili kupita bila kunywa chai yenye sukari.
Ugumu wa maisha unatokana na kulazimisha maisha. Kutaka kuishi maisha yasiyo level yako.
Unataka kuendesha Gari alafu huna hela ya Mafuta😀😀 Mafuta yakipanda bei unapiga kelele. Jambo lolote lisilo la kiwango chako ukilivagaa lazima upige kelele.
Unapiga kelele Kwa sababu mfumo wa maisha haukutambui Ila wewe ndio ukajitambulisha kuwa unakutambua.
Tunaishi kwenye Zama ambazo asiyefanya kazi anataka aishi Kama mtu anayefanya kazi. Yaani mtu hapokei ujira wowote kwa siku au Kwa mwezi alafu anataka aishi maisha Kama anapokea Kwa mwezi.
Maisha lazima yawe magumu ikiwa hujasoma lakini unataka ulipwe Mshahara mkubwa Kama mtu aliyesoma.
Hujasoma jua wewe ni kibarua, huwezi lipwa mishahara mikubwa. Wewe level yako ni kulipwa mishahara ya chini.
Sasa tatizo linakuja hapa; mtu hajasoma anataka kulipwa Mshahara mkubwa Kama aliyesoma😀😀 hapo lazima maisha yawe magumu Mzee.
Unataka ulipwe mamilioni ya pesa wakati kiwango chako sio hiko. Utabaki kulalamika tuu lakini unachopata ndio haki yako.
Hakuna maisha Magumu ikiwa utaishi maisha ya kiwango chako.
Unaoa mwanamke mzuri wakati huna hadhi ya kuoa mwanamke mzuri😀😀 lazima uhenyeshwe mavi. Lazima maisha yakuwie magumu.
Ni lazima ujue kuwa Maisha ya hapa Duniani hayana USAWA Kwa baadhi ya ishu.
Vitu vizuri ni Haki na halali Kwa wenye nguvu ya Fedha, mamlaka, nguvu ya kiroho(iwe Uchawi au miungu), na wazuri wenzao.
Zamani mtu alioa na kuolewa Kwa kufuata kiwango chake, masikini Kwa masikini, wanyonge Kwa wanyonge, wachawi Kwa wachawi, wazuri Kwa wazuri, wenye Fedha Kwa wenye Fedha, wafupi Kwa wafupi.
Na endapo itatokea ukaoa mtu msiyefanana basi lazima utoe kitu kinacholingana na alichonacho mtu huyo.
Kwamfano mwanaume mfupi ili aoe mwanamke mrefu na mzuri yampasa awe na sifa ya ziada Kama kuwa na pesa au mchawi au mbabe Sana, au Mtawala.
Ugumu wa maisha umeletwa na unafiki unaoendelea Duniani kuwa watu wote ni Sawa Jambo ambalo sio kweli.
Tupo Sawa kwenye some issues lakini tuna utofauti mkubwa kwenye ishu zingine.
Mtu anakuambia anayohaki ya kuishi mjini lakini akiambiwa ajenge nyumba inayoendana na mahali husika anaanza kupiga kelele; ooh! Gharama za ujenzi ni kubwa, ooh sijui mafundi wanabei kubwa😀😀 sasa si uende kijijini ambapo mafundi ni bei cheer!
Maisha hayarudi nyuma Hilo lazima likae akilini.
Maisha yanakua Kama wewe unavyokua.
Bei lazima zipande, zikue ili kuwafanya wasiostahili kuondoka kwenye mfumo.
Kama vile muda unavyoenda ili kutuzeesha Sisi viumbe ili tufe tuondoke kwenye mfumo wa maisha wake viumbe wengine.
Vijana wengi hupenda vitu vizuri bila kujua kuwa kuna wenye haki ya vitu vizuri.
Sio kila kitu kizuri ni Haki ya kila mtu.
Nimesema vitu vizuri ni Haki na halali ya wenye nguvu na wenye akili za juu.
Ooh! Nataka mwanaume handsome boy au mwenye pesa wakati wewe mwenyewe huna hili wala lile. Nature itakuondoa, itakunyanyasa Kwa sababu sio halali yako kuwa na Mwanaume mzuri au mwenye pesa.
Ukiona mwanamke mrembo mwenye umbo zuri linalokuvutia unafikiri ni Haki yako😀.
Tuacheni hizi ndugu zangu.
Ukiona maisha magumu jua kuna sehemu kubwa umeingilia mfumo usiokutambua. Usiohaki yako, usiohalali yako.
Unakuta mtu anasomesha watoto mamilioni ya pesa wakati uwezo wake ni malaki ya pesa. Huyu lazima apige mayowe Kwa maana mfumo wa mamilioni haumtambui. Unamuona Kama mhamiaji haramu hivyo unakuchukulia hatua Kali za kinidhamu.
Sio lazima mtoto umpeleke shule za gharama, mpeleke shule za kawaida alizosomea Taikon wa Fasihi, mbona Sisi tulisoma na tunakinukisha tuu vyema. Mbona hao waliosomea shule kubwa tumewakalisha mara kibao kila tunapokutana kwenye mitihani ya mwisho. Huko Chuoni mbona tumewapelekesha hao waliosomea kwenye mashule ya mamilioni.
Na hata kingereza tunawaburuza tuu.
Ishu kubwa unapaswa umfundishe mtoto kujitambua ili aweze kujiamini na ku-fit mazingira yoyote.
Hakuna maisha magumu isipokuwa kinachoendelea ni watu kutaka USAWA wawe wanafanana.
Ati viongozi wanalipwa mishahara vizuri au watoto wa viongozi wanapeana na kurithishanaa uongozi, ulitaka wakupe wewe wakati wao wakihangaika kuipigania nchi ipate uhuru, wewe Babu yako alijitia yoga na kukaa nyuma nyuma tena pengine alikuwa anawaona viherehere.
Usipende kujilinganisha, usipende USAWA usiowezekana.
Mwenzako kanunua Gari na wewe unainunua Gari wakati huna uwezo wa kuliwekea Mafuta.
Mafuta yakipanda unapiga yowee! Pumbavu.
Narudia ukiona maisha magumu basi jua kuna sehemu unalazimisha mfumo usiokutambua na usiohaki yako.
Sio lazima uishi nyumba nzuri, sio lazima ukae mjini, sio lazima uwe na Gari, sio lazima uwe na Mke Mzuri.
Wewe angalia mfumo wako unakusapoti kwenye Jambo gani.
Acha nipumzike, Hali ya hewa hainisapoti kuandika, mfumo umenikataa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam