Kinkunti El Perdedo
JF-Expert Member
- Nov 28, 2020
- 5,200
- 12,762
Naked truth [emoji125][emoji125]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Enzi hizo, kula wali kuku mpaka xmasi..
Wali maharage mpaka sabasaba.
Chai maandazi mpaka maulidi.
Ukibahatisha sana breakfast uji na viazi.
Usafiri kwenda dar, unatumia siku 10,
Ukitaka kununua gari mpaka utume maombi taifani na process zinachukua miaka.
Tv ilikua labda uende zanzibar ndo ukaangalie vipindi,,
Nguo zilikua adimu sana, watu walivaa suruali zina viraka, kumiliki baiskeli ilikua sifa kubwa sana, usafiri wa kijiji kwa kijiji ilikua ni kutembea au ukibahatisha ubebwe na tractor la kijiji[emoji23][emoji23][emoji23]
Dunia haina huruma ukifa ndo utapata unachostahiki
Miaka 20 ijayo watu wataona sisi Sasa ivi tulikuwa tunaishi maisha magumu according to your scenerio...maisha magumu it's mind set ya kucompare na mtu Fulani anacho huna...zamani maisha hayakuwa magumu watu waliona kawaida kuandikiana barua na kutuma posta Wala Hakuna watu waliofeel ugumu..sema saiv mna WhatsApp mnaona vya nyuma mnaonana vilikuwa tabu ...hapana ilikuwa normal n life lilikuwa normal Sana tu...
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
maisha ya kuanzia 2000 kwenda juu ndio magumu zaidi, wale waliokimbilia mjini hata kama watalala njaa, kwa sasa wanakula ila hawaifaidiki na raslimali zilizopo kwenye nchi yao, wameongezewa bei za vifurushi vya mawasiliano na tozo kila kona, tutafika mbinguni tumechoka sana
Vitu vizuri ni Haki na halali Kwa wenye nguvu ya Fedha, mamlaka, nguvu ya kiroho(iwe Uchawi au miungu), na wazuri wenzao.
👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿
Mkuu huko sahihi kabisa huoni Jiwe alivyokuwa anatafuna vitu laini kina AK.
Ahsante ndugu mwandishi kwa mtazamo ambao wengi wetu hatuna, Jambo ambalo linatufanya tusiishe kulalamika kila leo, japo upande mwingine tuna haki ya kulalamika sababu twawaona wenzetu wapo juu zaidi yetu, hata hivyo kupanga Ni kuchagua, maana Kuna maamuzi uyafanyayo leo, yatakufikisha mahali fulani au uishi maisha fulani, aidha wewe au vizazi vyako.HAKUNA MAISHA MAGUMU ZAMA HIZI, KILICHOPO WATU WA SASA KUPENDA USAWA.
Kwa Mkono wa, Robert Heriel.
Hakuna maisha rahisi Kama ya Zama hizi. Siku hizi kila kitu kimerahisishwa. Sijazaliwa zamani Sana Ila miaka ya 2000 Kurudi nyuma maisha yalikuwa complicated, yalikuwa magumu jamani.
Sio kwenye chakula, sio kwenye mawasiliano, sio kwenye makazi, sio kwenye usafiri, sio kwenye Huduma za kijamii. Maisha yalikuwa Magumu mno tena Sana.
Kwa watu waliokulia vijijini wataungana na Mimi kuwa Maisha ya sasa hivi ni rahisi yaani laini Kama unakunywa uji tuu.
Zamani ilikuwa ni Bora ukimbilie mjini ukalale njaa mjini kuliko kuishi kijijini ukila ukashiba.
Maisha ya sasa sio magumu Ila kinachoendelea ni Vijana wa Zama hizi Kupenda USAWA usiowezekana.
Ukitaka maisha yawe magumu penda USAWA usiowezekana.
Ati masikini Kama Taikon unataka uishi Sawa na Tajiri MOO! Hapo lazima maisha yawe complicated.
Zamani kunywa chai na sukari ilikuwa mbinde, walikuwa wanakunywa watu wenye pesa au wenye unafuu.
Nakumbuka Sisi badala ya kunywa chai yenye sukari tulikuwa tunakunyaa Uji WA chumvi.
Na tulikuwa tunaona ni Sawa Kabisa.
Siku hizi ni ngumu siku mbili kupita bila kunywa chai yenye sukari.
Ugumu wa maisha unatokana na kulazimisha maisha. Kutaka kuishi maisha yasiyo level yako.
Unataka kuendesha Gari alafu huna hela ya Mafuta[emoji3][emoji3] Mafuta yakipanda bei unapiga kelele. Jambo lolote lisilo la kiwango chako ukilivagaa lazima upige kelele.
Unapiga kelele Kwa sababu mfumo wa maisha haukutambui Ila wewe ndio ukajitambulisha kuwa unakutambua.
Tunaishi kwenye Zama ambazo asiyefanya kazi anataka aishi Kama mtu anayefanya kazi. Yaani mtu hapokei ujira wowote kwa siku au Kwa mwezi alafu anataka aishi maisha Kama anapokea Kwa mwezi.
Maisha lazima yawe magumu ikiwa hujasoma lakini unataka ulipwe Mshahara mkubwa Kama mtu aliyesoma.
Hujasoma jua wewe ni kibarua, huwezi lipwa mishahara mikubwa. Wewe level yako ni kulipwa mishahara ya chini.
Sasa tatizo linakuja hapa; mtu hajasoma anataka kulipwa Mshahara mkubwa Kama aliyesoma[emoji3][emoji3] hapo lazima maisha yawe magumu Mzee.
Unataka ulipwe mamilioni ya pesa wakati kiwango chako sio hiko. Utabaki kulalamika tuu lakini unachopata ndio haki yako.
Hakuna maisha Magumu ikiwa utaishi maisha ya kiwango chako.
Unaoa mwanamke mzuri wakati huna hadhi ya kuoa mwanamke mzuri[emoji3][emoji3] lazima uhenyeshwe mavi. Lazima maisha yakuwie magumu.
Ni lazima ujue kuwa Maisha ya hapa Duniani hayana USAWA Kwa baadhi ya ishu.
Vitu vizuri ni Haki na halali Kwa wenye nguvu ya Fedha, mamlaka, nguvu ya kiroho(iwe Uchawi au miungu), na wazuri wenzao.
Zamani mtu alioa na kuolewa Kwa kufuata kiwango chake, masikini Kwa masikini, wanyonge Kwa wanyonge, wachawi Kwa wachawi, wazuri Kwa wazuri, wenye Fedha Kwa wenye Fedha, wafupi Kwa wafupi.
Na endapo itatokea ukaoa mtu msiyefanana basi lazima utoe kitu kinacholingana na alichonacho mtu huyo.
Kwamfano mwanaume mfupi ili aoe mwanamke mrefu na mzuri yampasa awe na sifa ya ziada Kama kuwa na pesa au mchawi au mbabe Sana, au Mtawala.
Ugumu wa maisha umeletwa na unafiki unaoendelea Duniani kuwa watu wote ni Sawa Jambo ambalo sio kweli.
Tupo Sawa kwenye some issues lakini tuna utofauti mkubwa kwenye ishu zingine.
Mtu anakuambia anayohaki ya kuishi mjini lakini akiambiwa ajenge nyumba inayoendana na mahali husika anaanza kupiga kelele; ooh! Gharama za ujenzi ni kubwa, ooh sijui mafundi wanabei kubwa[emoji3][emoji3] sasa si uende kijijini ambapo mafundi ni bei cheer!
Maisha hayarudi nyuma Hilo lazima likae akilini.
Maisha yanakua Kama wewe unavyokua.
Bei lazima zipande, zikue ili kuwafanya wasiostahili kuondoka kwenye mfumo.
Kama vile muda unavyoenda ili kutuzeesha Sisi viumbe ili tufe tuondoke kwenye mfumo wa maisha wake viumbe wengine.
Vijana wengi hupenda vitu vizuri bila kujua kuwa kuna wenye haki ya vitu vizuri.
Sio kila kitu kizuri ni Haki ya kila mtu.
Nimesema vitu vizuri ni Haki na halali ya wenye nguvu na wenye akili za juu.
Ooh! Nataka mwanaume handsome boy au mwenye pesa wakati wewe mwenyewe huna hili wala lile. Nature itakuondoa, itakunyanyasa Kwa sababu sio halali yako kuwa na Mwanaume mzuri au mwenye pesa.
Ukiona mwanamke mrembo mwenye umbo zuri linalokuvutia unafikiri ni Haki yako[emoji3].
Tuacheni hizi ndugu zangu.
Ukiona maisha magumu jua kuna sehemu kubwa umeingilia mfumo usiokutambua. Usiohaki yako, usiohalali yako.
Unakuta mtu anasomesha watoto mamilioni ya pesa wakati uwezo wake ni malaki ya pesa. Huyu lazima apige mayowe Kwa maana mfumo wa mamilioni haumtambui. Unamuona Kama mhamiaji haramu hivyo unakuchukulia hatua Kali za kinidhamu.
Sio lazima mtoto umpeleke shule za gharama, mpeleke shule za kawaida alizosomea Taikon wa Fasihi, mbona Sisi tulisoma na tunakinukisha tuu vyema. Mbona hao waliosomea shule kubwa tumewakalisha mara kibao kila tunapokutana kwenye mitihani ya mwisho. Huko Chuoni mbona tumewapelekesha hao waliosomea kwenye mashule ya mamilioni.
Na hata kingereza tunawaburuza tuu.
Ishu kubwa unapaswa umfundishe mtoto kujitambua ili aweze kujiamini na ku-fit mazingira yoyote.
Hakuna maisha magumu isipokuwa kinachoendelea ni watu kutaka USAWA wawe wanafanana.
Ati viongozi wanalipwa mishahara vizuri au watoto wa viongozi wanapeana na kurithishanaa uongozi, ulitaka wakupe wewe wakati wao wakihangaika kuipigania nchi ipate uhuru, wewe Babu yako alijitia yoga na kukaa nyuma nyuma tena pengine alikuwa anawaona viherehere.
Usipende kujilinganisha, usipende USAWA usiowezekana.
Mwenzako kanunua Gari na wewe unainunua Gari wakati huna uwezo wa kuliwekea Mafuta.
Mafuta yakipanda unapiga yowee! Pumbavu.
Narudia ukiona maisha magumu basi jua kuna sehemu unalazimisha mfumo usiokutambua na usiohaki yako.
Sio lazima uishi nyumba nzuri, sio lazima ukae mjini, sio lazima uwe na Gari, sio lazima uwe na Mke Mzuri.
Wewe angalia mfumo wako unakusapoti kwenye Jambo gani.
Acha nipumzike, Hali ya hewa hainisapoti kuandika, mfumo umenikataa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna mwaka nilienda Mkuranga tu Apo,
Tulikua tunatafta chumba Cha kupanga,
Kuna nyumba tulikuta chumba Ni elfu 3 kwa mwezi,
Na aliyekua anaishi hapo,
Alipewa notsi ya kuhama kwa kushindwa kulipa Kodi ya miezi 3 mfululizo, yaani shilling elfu 9 tu.
Aya maisha KILA MTU anaishi kwa LEVEL YAKE
Ahsante ndugu mwandishi kwa mtazamo ambao wengi wetu hatuna, Jambo ambalo linatufanya tusiishe kulalamika kila leo, japo upande mwingine tuna haki ya kulalamika sababu twawaona wenzetu wapo juu zaidi yetu, hata hivyo kupanga Ni kuchagua, maana Kuna maamuzi uyafanyayo leo, yatakufikisha mahali fulani au uishi maisha fulani, aidha wewe au vizazi vyako.
Kama ulivyosema mwandishi, maisha siku hizi yamerahisika Sana, naungana na wewe.
Hapo zamani maisha yalikuwa magumu Sana, na yamekuwa yakirahisika kadri miaka inavyosonga mbele.
Imagine miaka fulani huko nyuma:-
1. Zaidi ya asilimia tisini ya safari zako utatembea kwa miguu hata Kama Ni zaidi ya kilometa kumi,
2.Unaweza ukasafiri Tena kwa miguu kutoka tegeta Hadi makumbusho kwa ajili tu ya kununua kiberiti cha kuwashia Moto, au mafuta kwa ajili ya taa usiku au vyote..
3.Unaweza kusafiri na kilo zaidi ya arobaini za mahindi , ukiwa umebeba kichwani umbali sawa na kutoka bunju Hadi kariakoo , kwa ajili ya kwenda kusaga ili upate unga wa kula, na huko ukakuta foleni ya watu wanaosubiri kusaga wasiopungua Mia moja, ukakaa kwenye foleni zaidi ya masaa sita ndipo ukafanikiwa kusaga.
4.Ukimkumbuka ndugu, jamaa au rafiki yako, hakuna masasiliano Kama leo, unafunga tu safari kwenda kumbahatisha, ukiwa na bahati mbaya unaweza kufika ukaambiwa, mmepishana, kaandoka leo kwenda mkoa fulani, atarudi baada ya mwezi mmoja , na bila Shaka Ni ile safari ambayo ukiondoka alfajiri unafika adhuhuri, hivyo unalazimika kulala ndipo uanze safari ya kurudi kwako.
5.Wanafunzi wengi walisoma usiku kwa kutumia mianga hafifu Kama kibatari na chemli, wengi wao wakikosa uwezo wa kusoma muda mrefu, baadhi yao wakikomaa mpaka kupata matatizo ya macho.
Kwa kifupi maisha yalikuwa magumu Sana, hasa kutokana na uhaba au uduni wa huduma za kijamii Kama usafiri,masasiliano, maduka ya mahitaji hata madogo ya nyumbani, nyumba za ibaada, masoko,mashule,mahospitali, umeme, maji, nk.
Pamoja na hayo, bado wenzetu walioishi maisha hayo katika miaka hiyo, ndiyo wanaoongoza kwa kusifia kwamba maisha ya zamani yalikuwa rahisi kuliko haya ya siku hizi.
Ukweli Ni kwamba, urahiai wa maisha katika miaka hiyo ulikuwepo katika upatikanaji wa malighafi Kama chakula, na pengine hi ilitokana na kutojua thamani ya hi malighafi , hujasikia story ya wasukuma kutumia dhahabu Kama kete za kuchezea bao?
Vinginevyo maisha yalikuwa magumu Sana.
Ndugu Hawa waliridhika uduni wa maisha waliyoishi, hawakuwa za maisha Bora, ili mradi chakula kinapatikana, pengine kwa sababu hakukuwa na standard .
Elimu imeleta standard fulani za maisha ambazo kila mtu anatamani azifikie.
Katika mapambano ya mwanadamu kutaka kufikia au kumantain standard fulani zilizopo au alizojiwekea, hukutana na ugumu na vikwazo mbalimbali.
Hapa ndipo anapotafsiri kwamba "maisha yamekuwa magumu.."
Watu wamejua haki zao za msingi, na vijana wengi wasasa wamejitambua kwakudai haki. Bahatimbaya wakubwa hawataki kukubali kwamba zama zimebadilika na kizazi cha leo kimejitambua kwa msaada wa utandawazi.
Kwa mtazamo wangu, naona vijana wengi wanakua na ugumu wa maisha kwasababu ya hofu na kutokuthubutu.Vijana wangejitambua wasingeyaona maisha ni magumu
Kwa mtazamo wangu, naona vijana wengi wanakua na ugumu wa maisha kwasababu ya hofu na kutokuthubutu.
Upo sahihi mzee 100% kwenye heading.. ngoja nizame kwenye Content niperuzi sasa
...... ........ .....
Nimejiridhisha Content iko vizuri pia kwa kiwango kikubwa kama sio chote..
Hongera sana Taikon..