Hakuna maisha magumu Zama hizi; kilichopo ni watu kutaka usawa



Alafu kuna mtu anasema maisha magumu hizi ni Akili au matope😀😀😀
 


Husikii watu wakisema maisha ni magumu??

Ndio najaribu kuwaambia maisha ya sasa ni rahisi Kama unakunywa uji tuu.
 


Mbona maisha ni rahisi Sana.

Kama unaona vifurushi ni ghali tumia mfumo wa zamani tulioutumia WA kutuma barua alafu utaelewa ugumu uko wapi.

Ukiona kitu ni kigumu ujue huna hadhi ya kukitumia au hujafikia level ya kukitumia.

Shida binadamu wa Zama hizi wanapenda bwerere
 


😀😀😀😀

Mimi siko huko Mkuu
 
Ahsante ndugu mwandishi kwa mtazamo ambao wengi wetu hatuna, Jambo ambalo linatufanya tusiishe kulalamika kila leo, japo upande mwingine tuna haki ya kulalamika sababu twawaona wenzetu wapo juu zaidi yetu, hata hivyo kupanga Ni kuchagua, maana Kuna maamuzi uyafanyayo leo, yatakufikisha mahali fulani au uishi maisha fulani, aidha wewe au vizazi vyako.
Kama ulivyosema mwandishi, maisha siku hizi yamerahisika Sana, naungana na wewe.
Hapo zamani maisha yalikuwa magumu Sana, na yamekuwa yakirahisika kadri miaka inavyosonga mbele.
Imagine miaka fulani huko nyuma:-
1. Zaidi ya asilimia tisini ya safari zako utatembea kwa miguu hata Kama Ni zaidi ya kilometa kumi,
2.Unaweza ukasafiri Tena kwa miguu kutoka tegeta Hadi makumbusho kwa ajili tu ya kununua kiberiti cha kuwashia Moto, au mafuta kwa ajili ya taa usiku au vyote..
3.Unaweza kusafiri na kilo zaidi ya arobaini za mahindi , ukiwa umebeba kichwani umbali sawa na kutoka bunju Hadi kariakoo , kwa ajili ya kwenda kusaga ili upate unga wa kula, na huko ukakuta foleni ya watu wanaosubiri kusaga wasiopungua Mia moja, ukakaa kwenye foleni zaidi ya masaa sita ndipo ukafanikiwa kusaga.
4.Ukimkumbuka ndugu, jamaa au rafiki yako, hakuna masasiliano Kama leo, unafunga tu safari kwenda kumbahatisha, ukiwa na bahati mbaya unaweza kufika ukaambiwa, mmepishana, kaandoka leo kwenda mkoa fulani, atarudi baada ya mwezi mmoja , na bila Shaka Ni ile safari ambayo ukiondoka alfajiri unafika adhuhuri, hivyo unalazimika kulala ndipo uanze safari ya kurudi kwako.
5.Wanafunzi wengi walisoma usiku kwa kutumia mianga hafifu Kama kibatari na chemli, wengi wao wakikosa uwezo wa kusoma muda mrefu, baadhi yao wakikomaa mpaka kupata matatizo ya macho.

Kwa kifupi maisha yalikuwa magumu Sana, hasa kutokana na uhaba au uduni wa huduma za kijamii Kama usafiri,masasiliano, maduka ya mahitaji hata madogo ya nyumbani, nyumba za ibaada, masoko,mashule,mahospitali, umeme, maji, nk.
Pamoja na hayo, bado wenzetu walioishi maisha hayo katika miaka hiyo, ndiyo wanaoongoza kwa kusifia kwamba maisha ya zamani yalikuwa rahisi kuliko haya ya siku hizi.
Ukweli Ni kwamba, urahiai wa maisha katika miaka hiyo ulikuwepo katika upatikanaji wa malighafi Kama chakula, na pengine hi ilitokana na kutojua thamani ya hi malighafi , hujasikia story ya wasukuma kutumia dhahabu Kama kete za kuchezea bao?
Vinginevyo maisha yalikuwa magumu Sana.
Ndugu Hawa waliridhika uduni wa maisha waliyoishi, hawakuwa za maisha Bora, ili mradi chakula kinapatikana, pengine kwa sababu hakukuwa na standard .
Elimu imeleta standard fulani za maisha ambazo kila mtu anatamani azifikie.
Katika mapambano ya mwanadamu kutaka kufikia au kumantain standard fulani zilizopo au alizojiwekea, hukutana na ugumu na vikwazo mbalimbali.
Hapa ndipo anapotafsiri kwamba "maisha yamekuwa magumu.."
 


Sio lazima kuishi ndani ya nyumba😀😀😀 Level yake niya wahadzabe na watindiga au Wa-bushmen😀😀

Mbona Fresh tuu
 


Mkuu Nashukuru Sana Kwa maelezo yako yaliyonyooka.
 
Watu wamejua haki zao za msingi, na vijana wengi wasasa wamejitambua kwakudai haki. Bahatimbaya wakubwa hawataki kukubali kwamba zama zimebadilika na kizazi cha leo kimejitambua kwa msaada wa utandawazi.
 
Upo sahihi mzee 100% kwenye heading.. ngoja nizame kwenye Content niperuzi sasa
...... ........ .....

Nimejiridhisha Content iko vizuri pia kwa kiwango kikubwa kama sio chote..
Hongera sana Taikon..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…