Hakuna marefu yasiyo na mwisho, ila nitawakumbuka daima

Intel Nina maneno machache kwako.
Kuna faida kubwa sana katika kifo. Lakini hakuna faida kabisa katika kujiua. Watu wengi wanapatwa na madhira zaidi ya hayo uliyonayo, lakini wanakaa yanapita. Unapopata tatizo usisimame, kaa chini lipite. Kukaa kutakupa balance, kusimama kutakuyumbisha na mwisho utaanguka. Kukaa kutakupa tafakuri, kusimama kutakupa kiwewe na mwisho utaweweseka.
Hutakiwi kufa kizembe.
 
Tuwasiliane PM, nitumie namba yako ya simu tuweze kuongea zaidi.
 
Duuuh pole Sana! hayo unayopitia,wengi tumepitia. alikini ashukuliwe Mungu alituokoa kutoka mikononi mwa watesi wetu!! Sasa tunamtukuza Jehovah Kwa matendo makuu aliyotutendea!! ametupa sababu ya kujidai!ametuheshimisha! tumefanyika baraka!! nitafute pm nikupe mbinu za kuishinda hayo.
 
Mwamini Mungu tu atakuvusha. Akili yako inapofika mwisho mweleze Mungu na uamini kwamba bado anakupenda na atafungua milango ya Baraka kwako. Kama aliweza kukausha Bahari ya Shamu na wana wa Israel wakavuka salama na kuwaangamiza adui zake basi Amini ya kwamba hata kwako atatenda Jambo. Kwani amekuokoa na mangapi tangu uzaliwe hadi leo? Je Ni wangapi hawajaamka hai leo na wewe ungali hai? Yote Kwa imani mkabidhi Mungu atakuokoa.
 
Huyu aliyetoa malalamiko hapa nimepita kule sasa hivi anagombana na jamaa aliyeanzisha uzi wa kuhama makazi. Sasa jiulize je huyu kijana ni mzima au bangi?
Mkuu mi nimemuuliza tu, ila inaonyesha labda ye kahisi vibaya. Afu kuhusu bangi, MUNGU anajua ka nishawai hata kuigusa
 
Kaka, shida nini? Tueleze pengine msaada utapatikana mzee.
 
Mungu atakuvusha katika kipindi kigumu unachopitia haijalishi ni magumu gani lakini ukiwa na moyo wa kuamini daima kuna njia. Giza likizidi sana kunakaribia kupambazuka mkuu kaza moyo nina imani michango ya members huku itakuwa imekusaidia na kukupa moyo.

Mimi trudie na kipenzi Chizi Maarifa ambae kanitoroka mwezi mzima sasa sijui alipo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] tunakuombea afueni na pia naamini tutazidi kuwa pamoja humu kwa kipindi kirefu sana. Na akirudi tuu tujitahidi asiende kwenye kampeni ya Kataa ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…