Hakuna mbunge atakayethubutu kuukosoa utawala wa Rais Samia, kwa sababu kwa kufanya hivyo atahatarisha nafasi yake

Hakuna mbunge atakayethubutu kuukosoa utawala wa Rais Samia, kwa sababu kwa kufanya hivyo atahatarisha nafasi yake

Sio kweli mama samia ana imani na uchamungu...mwendazake ndie alikuwa na tabia hiyo

Kwa taarifa yako huyo mama ukimkosoa washauri wake wanamwambia usikubali kuchezewa, mbona hawakumchezea Magufuli? Kitakachifuata hapo utajua hujui. Magufuli ndio alipandikiza hii mbegu mbaya ya kutotaka kukosolewa, na wengine wote watakaofuata watatumia mbinu hiyo hiyo. Machafuko tu ndio yataturejesha kwenye njia sahihi.
 
Huyu ndio muumini wa uongozi wa kiimla sana kuliko hata waliowaho kuongoza nchi ya Tanzania. Kwanza hapendi kukosolewa sio kwa sababu wakosoaji wanakosea, hapana ni kwa sababu anayekosolewa huwa anahisi kuwa na uduni hivyo wasaidizi wake wanachukua majukumu ya kuwakomoa wahusika bila kuzingatia sheria. Kwa kuwa wale mabingwa wa kuhamasisha kupinga dhuluma walishalambishwa asali suala la kukandamiza haki za binadamu linanyamaziwa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea. Mifano ni mingi sana hata unaowasikia wakisifia sio kwamba wana penda ila matakwa ya wakati wa mtawala aliyeko madarakani ndio shida inapoanzia.

Wabunge hawatetei wananchi wala kukemea ukiukwaji wa haki za wengine hasa wasiokuwa na kipato cha kutosha na kumudu angalau mahitaji muhimu ya binadamu
Hilo bunge nani alilitengeneza

Si walitaka wenyewe

Ova
 
Kwa taarifa huyo mama ukimkosoa washauri wake wanamwambia usikubali kuchezewa, mbona hawakumchezea Magufuli? Kitakachifuata hapo utajua hujui. Magufuli ndio alipandikiza hii mbegu mbaya ya kutotaka kukosolewa, na wengine wote watakaofuata watatumia mbinu hiyo hiyo. Machafuko tu ndio yataturejesha kwenye njia sahihi.
Naona mleta uzi huu hapa anapita kimya kimya
Nmemuliza aliyepita si kuna watu walimkosoa au [emoji1]
Acha tu tunyo9shweeee tu

Ova
 
Huo ndiwo ukweli.

Wawakilishi wa wananchi hususani wabunge wote ni waoga kuukosoa Utawala wa Samia kwa hofu kubwa ya kutokuteuliwa 2025 kuwa wagombea wa nafasi hiyo.

Kama yupo awaye na matarajio hayo ni bora ayafute.

Ifahamike wabunge wote waliopo mle bungeni kwa sasa ni zao na bila kupepesa macho ni wale Hayati Magufuli aliwataka.

Kwa muktadha huo waheshimiwa hao kwa sasa wanaishi kwa matumaini yasiyo tumainika na ili aghalabu wapambanie ndoto zao wengi wao wanaonelea ni bora kutoukosoa Utawala huo wakitarajia huruma ya Mwenyekiti kwenye kura za maoni zijazo.

2025 itakuwa huyo alikuwa mwenzetu-apite na huyo hakuwa upande wetu alipuliwe bila kujali ameongoza kura za wajumbe ama la!.

Allah nijalie niuone mwaka 2025.
Sote tunaelewa kwamba kujipendekeza ndio mtindo wa kisasa. Kwahio kila mwenye nafasi ya kusikika anataka asikike akitoa pambio ila zote ni njaa tu.

Mbona mbunge shabibby anatoa maoni yake vizuri tu. Tatizo wabunge njaa ndio wanaoleta kero bungeni kwa pambio za kijinga.
 
Sio kweli mama samia ana imani na uchamungu...mwendazake ndie alikuwa na tabia hiyo
Mungu akubariki chanzo cha matatizo yote haya ni magufuri,huwezi ukatibu ugonjwa bila kujua chanzo cha ugonjwa,watu wataongea sana ila wakijua kuwa kuna kitu Magu alipanda watatulia tu.
 
Unataka wakosoe Nini labda, Kama Ni vituo vya Afya, zahanati, shule , huduma za maji na umeme zinapelekwa kila Jimbo na kata zote nchini, wabunge wanapewa majibu ya kulizisha waulizapo maswali bungeni kuhusiana na kero katika majimbo yao maana serikali ya mh Rais wetu Ni sikivu Sana,

Sasa wewe unataka waanze kukosoa kwamba serikali inajenga vituo vya Afya vingi Sana? Au unataka wakosoe Nini, waheshimiwa wabunge wetu Kama ilivyokwetu wananchi wameridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais wetu mpendwa, Ndio maana wanaendelea kumuunga mkono na kufanya Naye kazi bega kwa bega katika kutuletea maendeleo sisi wananchi
 
Huo ndiwo ukweli.

Wawakilishi wa wananchi hususani wabunge wote ni waoga kuukosoa Utawala wa Samia kwa hofu kubwa ya kutokuteuliwa 2025 kuwa wagombea wa nafasi hiyo.

Kama yupo awaye na matarajio hayo ni bora ayafute.

Ifahamike wabunge wote waliopo mle bungeni kwa sasa ni zao na bila kupepesa macho ni wale Hayati Magufuli aliwataka.

Kwa muktadha huo waheshimiwa hao kwa sasa wanaishi kwa matumaini yasiyo tumainika na ili aghalabu wapambanie ndoto zao wengi wao wanaonelea ni bora kutoukosoa Utawala huo wakitarajia huruma ya Mwenyekiti kwenye kura za maoni zijazo.

2025 itakuwa huyo alikuwa mwenzetu-apite na huyo hakuwa upande wetu alipuliwe bila kujali ameongoza kura za wajumbe ama la!.

Allah nijalie niuone mwaka 2025.
Ngoja niende zangu Burundi Mie kila Siku Mapya
1661339423618.jpg
 
Back
Top Bottom