Hakuna mbunge atakayethubutu kuukosoa utawala wa Rais Samia, kwa sababu kwa kufanya hivyo atahatarisha nafasi yake

Sio kweli mama samia ana imani na uchamungu...mwendazake ndie alikuwa na tabia hiyo

Kwa taarifa yako huyo mama ukimkosoa washauri wake wanamwambia usikubali kuchezewa, mbona hawakumchezea Magufuli? Kitakachifuata hapo utajua hujui. Magufuli ndio alipandikiza hii mbegu mbaya ya kutotaka kukosolewa, na wengine wote watakaofuata watatumia mbinu hiyo hiyo. Machafuko tu ndio yataturejesha kwenye njia sahihi.
 
Hilo bunge nani alilitengeneza

Si walitaka wenyewe

Ova
 
Naona mleta uzi huu hapa anapita kimya kimya
Nmemuliza aliyepita si kuna watu walimkosoa au [emoji1]
Acha tu tunyo9shweeee tu

Ova
 
Sote tunaelewa kwamba kujipendekeza ndio mtindo wa kisasa. Kwahio kila mwenye nafasi ya kusikika anataka asikike akitoa pambio ila zote ni njaa tu.

Mbona mbunge shabibby anatoa maoni yake vizuri tu. Tatizo wabunge njaa ndio wanaoleta kero bungeni kwa pambio za kijinga.
 
Sio kweli mama samia ana imani na uchamungu...mwendazake ndie alikuwa na tabia hiyo
Mungu akubariki chanzo cha matatizo yote haya ni magufuri,huwezi ukatibu ugonjwa bila kujua chanzo cha ugonjwa,watu wataongea sana ila wakijua kuwa kuna kitu Magu alipanda watatulia tu.
 
Unataka wakosoe Nini labda, Kama Ni vituo vya Afya, zahanati, shule , huduma za maji na umeme zinapelekwa kila Jimbo na kata zote nchini, wabunge wanapewa majibu ya kulizisha waulizapo maswali bungeni kuhusiana na kero katika majimbo yao maana serikali ya mh Rais wetu Ni sikivu Sana,

Sasa wewe unataka waanze kukosoa kwamba serikali inajenga vituo vya Afya vingi Sana? Au unataka wakosoe Nini, waheshimiwa wabunge wetu Kama ilivyokwetu wananchi wameridhishwa na utendaji kazi wa mh Rais wetu mpendwa, Ndio maana wanaendelea kumuunga mkono na kufanya Naye kazi bega kwa bega katika kutuletea maendeleo sisi wananchi
 
Ngoja niende zangu Burundi Mie kila Siku Mapya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…