Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Habari za watu kuchanjwa na wachawi usiku zinaaminika sana nchi hii. Lakini ukweli ni kuwa hakuna wachawi wa kuchanja watu chale. Zile Inazoitwa chale za wachawi huwa ni matokeo ya kukwaruzwa na mchanga usiku baada ya kulalia kitanda kichafu.
Mchanga ni mgumu na una ncha kali kama za wembe, na pengine zaidi. Glasi zenyewe hutengenezwa kutokana na mchanga. Na hata kazi kubwa ya screwnprotectors za simu ni kuzuia kioo kisikwaruzwe na mchanga.
Sasa mtu akilalia kitanda kichafu, chenye mchanga. Katika kujigeuzageuza usiku lazima "umchale." Asubuhi akiamka bila kuelewa kilichotokea, anasingizia wachawi.