Hakuna mchawi anayechanja chale watu usiku, acheni kulalia vitanda vichafu.

Jamii zote duniani zimepitia hizi imani za kichawi. Ni mambo yasiyofanya chochote. Lakini kwa vile watu walikuwa wakiyafanya, ndiyo maana yameandikwa.
 
Mmae leo nakupiga chale kwenye kalio uamke nazo kesho halafu ulete thread kesho
 
Ufu 22:15

Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.
Wachawi na waabudu sanamu hawana tofauti. Pilika zao hazizai matunda yoyote. Unaamini mtu anaweza zindikwa risasi isimpenye?
 
Yaani unaelezea mpaka raha bila magumashi🙏🔥🔥
 
We ni kichwa sana👽👽
 
Mm nilikuwa siamini mambo ya kishirikina ila yaliyo nitokea Mwaka Juzi nikiwa Moshi niliamini uchawi upo Hadi Leo Huwa nashindwa kuelewa Kila nikikumbuka sinywi pombe Wala kuvuta bangi ila niliyo yaona Bado Huwa nikikumbuka naweweseka
 
Jamii zote duniani zimepitia hizi imani za kichawi. Ni mambo yasiyofanya chochote. Lakini kwa vile watu walikuwa wakiyafanya, ndiyo maana yameandikwa.
Sijakuelewa?
Kwa kua watu waliyafanya ndio maana yameandikwa kwa hiyo yapo au hayapo?

Kuna kifungu kinasema mchawi auliwe katika biblia hapo imekaaje?
 
Wachawi na waabudu sanamu hawana tofauti. Pilika zao hazizai matunda yoyote. Unaamini mtu anaweza zindikwa risasi isimpenye?
Wewe unaamini katika vitabu vya dini?
Labda tuanzie hapo ndio tutajua hasa msimamo wako,
 
Aisee kumbe wana mbinu kali hivi [emoji1787]
Mtoa mada aje ajitetee hapa
 
Sijakuelewa?
Kwa kua watu waliyafanya ndio maana yameandikwa kwa hiyo yapo au hayapo?

Kuna kifungu kinasema mchawi auliwe katika biblia hapo imekaaje?
Hata walioabudu Baali waliuwawa, Lakini ibada yao ilikuwa na matokeo yoyote? So aliyefanya uchawi aliuwawa lakini uchawi wake haukuwa kitu chochote. Ni ujinga tu. Leo hii watanzania wengi wanaamini nyongo ya mamba ni sumu. Lakini si kweli hata kidogo. Ndivyo imani juu ya uchawi ipo hivyo. Inatokana na ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…