Hakuna mkoa mzuri wa kuishi kama Mbeya hapa Tanzania

Niliaminigi maneno ya Wanyakyusa nikaenda huko 2009 nilikutana vumbi kama poda kipindi hiki watu wanakula nondo za utosi, saa moja jioni wote ndani ukitaka kwenda hata dukani inabidi uvae helmet kulinda fuvu.
 
Niliaminigi maneno ya wanyakyusa nikaenda uko 2009 nilikutana vumbi kama poda kipindi hichi watu wanakula nondo za utosi saa moja jioni wote ndani ukitaka kwenda hata dukani inabidi uvae helmet kulinda fuvu
Karibu tena Mkuu maendeleo ni hatua vumbi limepungua

 
Ingekuwa Vijana wanaoanza maisha ya Utumishi ingekuwa wanaruhisiwa kuchagua Mkoa, ningewashauri waanze na huo.

Maisha ni Cheap sana Mbeya, mara ya kwanza nafika nakutana na Chips za shilingi 500 ambazo nilishindwa kuzimaliza

Ukiwa na shilingi laki 1 inatosha kula Mwezi Mzima
 
Not that bad
Huu mji umechoka inabidi uvunjwe ujengwe upya. Ni mji mkubwa ila sio mzuri kimpangolio isipokuwa sehemu kadhaa. Mbeya ingepangwa mji ungekuwa mzuri no 1. Geographically ni no 1.

Mwanza itaendelea kuiacha Mbeya daima kwa sababu Mbeya wanaendelea kujenga holela sasa sijii kwa nini Serikali haingilii kati na kuzuia kujenga holela.

Wanyakyusa na ndugu zao wasafwa hawazingatii mpango mji japo ni watu wanaojenga sana pengine kuliko makabila mengi.
 
Mkuu rangi za kutu za bati zisikutishe
 
Msipende sana mikoa yenye chakula kingi, hsina nxunguko wa hela. Mbeya, Songea, Rukwa, Kigoma, Kagera,Kilimanjaro.

Hio mikoa utashiba ila hela za maana hutashika. Mkoa unaopta ndizi 4 kwa mia mbili utatoboa hapo. Ili utoboe hio mikia inakubidi ulime usafirishe mikoa mingine.

Napingana na ushauri wako. Maisha sio chakuka bali ni hela, ukiwa na hela utanunua chochote.. Ili upate elfu 10 itabifi uuze sahani ngapi za chips au chane ngapi za nduzi!
 
Ipo hivi watu wa Mbeya moja ya kitu wanafikiria sana ni kujenga ....... yani wewe ukiwa Mbeya haijalishi una pesa kiasi gani haijalishi unatembelea gari ya bei juu kiasi kuanzia benzi, BMW and the like ...

Kama utakuwa hujajenga nyumba hata ya vyumba viwili (hauna nyumba ) basi mbele ya wanambeya huna cha kuwaambia wewe ni masikini kama masikini wengine.

Sasa basi ili kila mwanambeya kukwepa hii aibu basi atajitahidi kujenga kajumba kokote kale hata eneo lisilotakiwa ili kukwepa kudharaulika matokeo yake ndyo huo ujenzi wa olela unaouona hapo Mbeya.
 
Mkoa wa Mbeya ni namba 3 Kwa pato la Taifa Sasa unasemaje hakuna pesa?

Mbeya ni Mkoa wa pili kuwa na mabasi mengi ya kutoka Dar to Mikoani

Sasa with all that how comes hakuna mzunguko wa pesa? Hizi stori Huwa unahadithiwa na nani bwashee?

 
Hili lina ukweli. Mwanambeya akikuambia amejenga halafu ukakikuta alichokijenga, ni ajabu
 
Naufahamu mkoa vizuri.
Serikali imezembea kwente kipanga huu mji na bafo wanaendekea kugaribu huko milimani wanajenga miji mioya hovyo hovyo.
Mbeya haijawahi pata kiongozi mahiri wa kusimamia mji.
Mbeya ingekuwa kama ulaya.
Hakuna single Kiongozi anaweza badili Mkoa yeye kama yeye,sera za Nchi Haziruhusu Hilo maana hata ukiongeza uzalishaji Bado mapato yatakuwa ni ya Nchi.
 
Mkoa wa Mbeya ni namba 3 Kwa pato la Taifa Sasa unasemaje hakuna pesa?

Mbeya ni Mkoa wa pili kuwa na mabasi mengi ya kutoka Dar to Mikoani

Sasa with all that how comes hakuna mzunguko wa pesa? Hizi stori Huwa unahadithiwa na nani bwashee?
Pesa zingeonekana. Mwanza huitaji kuitetea kila kitu kinajionesha. Kwa nini mbalali haibadiriki kama watu wanahela.
Mbeya ina watu wengj wenye vishughili shughuli.
 
Upo sahihi mkuu, gharama za maisha za huo mkoa ni kitongaaaa...
 
Hakuna single Kiongozi anaweza badili Mkoa yeye kama yeye,sera za Nchi Haziruhusu Hilo maana hata ukiongeza uzalishaji Bado mapato yatakuwa ni ya Nchi.
Hata mipango mji? Mapato ya halmashsuri mengine si yanabaki. Dodoma yajuzi tu wameweza kupanga mji wao na unakua kwa kasi na itaizidi mbeya si muda mrefu.
Mbeya ilitakiwa iwe zaidi ya hapa ilipo, tuongee ukweli.
Mkurugenzi wa dodona kipindi cha Magu alikuwa mkali sana kwenye mipango miji
Mbeya miji mipya inajengwa holela hafi sasa hivi nenda itewe nk ujionee ni shaghala bagala.
 

Kwenye umeme hapana, labda bwawa likiisha, umeme ni tia maji tia maji sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…