Mkuu ujenzi wa tofali za kuchoma kwa Mbeya mjini umekuja baadaye sana, mimi mwenyewe nimeishi sana tu kwenye hizo nyumba za tofali tope...
Nonde, Simike,Sinde, Nzovwe, Mbalizi, Makunguru, Ilomba, Uyole na hata miji mipya kama Nsalaga huku kote nyumba zilizopo ni za matofali ya matope yale...
Kuna miaka serikali ya mkoa ilipitisha amri ya ujenzi wa tofali za kuchoma, ndio walau afadhali watu wakaanza choma matanuru ya tofali na kwa waliokuwa na nyumba tayari, wakaambiwa wapige "lipu"...
Haziwezi vunjika kwa sababu zinajengwa vizuri, isipokuwa zinaharibu muonekano wa mji kwa namna zilivyo...Hazivutii machoni...