Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Onyesha hivyo vipande vipande

Dismembered - kukatwa vipande vipande
1000030729.png
 
Matukio mengi ya mauji hufanyika sirini lakini huja kuwa dhahiri tena kwenye mwanga mkali

Wazungu wanasema " no perfect murder"
Murder ikitendeka na isijulikane labda vyombo vya uchunguzi visiamuwe kuingia kazini

Ukitenda jinai ya murder Kuna uhakika asilimia 💯 utajulikana na ushahidi utakutia hatiani
Jiweke mbali na jinai hii

Kesi na upelelezi vinaweza chukua hata miaka 30 lakini amini wapelezi watakutia hatia na uovu utawekwa wazi

Hapa nitatoa baadhi ya hujuma maarufu hapa Tanzania

1. Mauaji ya Milembe Suleimani
Hawa wauaji walikuwa smart, jinsi walivyo mlaghai hadi kumpeleka site,
Kuzuia mawasiliano, kuficha simu na vifaa au silaha
Lakini wakasahau chupa ya fanta, na wapelelezi walivoikuta wakachukua vinasaba na kugundulika kuwa aliishika mmoja wa mtuhumiwa na kilichofuata mambo yalikuwa kwenye mwanga wa jua kali

2. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya KHamis Luwoga.
Huyu bwana alimuuwa mke wake huko Kigomboni kwenye jumba lake kifahari.

Vyote alicheza smart, kuanzia kuchoma mwili moto na kutupa majibu shambani Kwake Kibiti

Tatizo akapanic na kujitumia SMS Kwa kutumia simu yake wake
Sms zilivyofutiliwa ikandulika alituma sms wakiwa umbali mdogo yani kama walikaa pamoja
Vile ku report kesi 1 vituo tofauti vya police
Na kuacha mkoba wa mkewe ambao alikuwa hawezi kuuacha
Ushahidi ulivopeleka mahakamani Luwoga alicheka na kukiri kosa mwenyewe

3 Mauaji ya RPC Barlow 2012 Mwanza

Hapa wauaji walivamia na kumuua kamanda nakufanikiwa KutorokA eneo la tukio
Kipengele kikaja walishika gari na maganda ya risasi
Finger Print zilivochukulia, mambo yakawa dhahiri na hukumu ya kifo Kwa watu 4 ikafuata

4 Mauaji ya dada wa Msuya
Huyu Binti alikuwa kwenye migogoro ya mirathi na mjane wa Msuya
Huyu Binti alichinjwa kama mbuzi wa Vingunguti
Wauaji wakitenda yote, lakini wakasahau panga
Uchunguzi ukaanza Kwa watuhumiwa na mke wa Hayati Msuya alikutwa na hatia ya kufadhili na hivo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini hali iliyotuacha mdomo wazi alishinda rufaa yake na kuachiwa huru na mahakama

5. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya Bageni 2006
Bageni alikuwa RCO kinondoni
Alipanga njama za kuwauwa wafanya biashara 4, kati ya hao watatu walikuwa ndugu wa damu
Inasemekana aliwapora million 200 na madini
Kwa mamlaka yake aliita press na kutangaza kuwauwa majambazi waliokuwa na silaha
Rais Kikweta alivopewa za kikachero aliunda time ya majaji kuchunguza na mambo Bageni aliyotenda gizani yalikuwa wazi kama uchi wa mbuzi

Hizi ni baadhi ya kesi maarufu ila zipo nyingi mtaani ambazo watenda jinai ya murder hawakutoboa licha ya kufanya uhalifu huu sirini na gizani

Hapa nasubiri hukumu ya mtoto Asimwe wa Muleba Kagera aliyekuwa albino, ambayo mauaji hayo alihusishwa baba yake mzizi na Padre wa Kanisa katoliki
Unsolved

1. The Dyatlov Pass Incident (1959, Russia)

2. Jack the Ripper (1888, England)

3. The Hinterkaifeck Murders (1922, Germany)

4. The Zodiac Killer (1960s-70s, USA)

5. The Tamam Shud Case (1948, Australia)

6. The Villisca Axe Murders (1912, USA)

7. The Isdal Woman (1970, Norway)


Fuatilia hizo ni very interesting ila hao jamaa waliohusika hakuna hata mmoja aliyekamatwa imefikia hatua watu wanadhani ni hadithi za kufikirika.
 
Unsolved

1. The Dyatlov Pass Incident (1959, Russia)

2. Jack the Ripper (1888, England)

3. The Hinterkaifeck Murders (1922, Germany)

4. The Zodiac Killer (1960s-70s, USA)

5. The Tamam Shud Case (1948, Australia)

6. The Villisca Axe Murders (1912, USA)

7. The Isdal Woman (1970, Norway)


Fuatilia hizo ni very interesting ila hao jamaa waliohusika hakuna hata mmoja aliyekamatwa imefikia hatua watu wanadhani ni hadithi za kufikirika.
Asante nitapata muda nizichimbe nijue vizuri
 
Hiyo ni kwa bongo tu


Refer to Jamal khashoggi assassinated 2 Oct 2018 in Instanbul Turkey aliingia ubalozini tu na hakutoka tena huko mkewe mtarajiwa akimsuburi nje ya ubalozi for many hours
😃😃 nilidhan atatoa mifano kwa nchi zilizoendelea kwa upelelez wa makosa kama ayo matokeo yake anatolea mfano kwa bongo tu
 
Hii mbona kama walisolve , kuna documentary nilicheki ila kama sikosei kuna mamlaka ikakataa mbinu zilizotumika in summary watu wa kundi la biggie walimpiga tupac na watu wa tupac wakapiga revenge kwa biggie
Mbona kuna wanaosema kauwawa na Diddy
 
Asante nitapata muda nizichimbe nijue vizuri
Huwa una fuatilia channel inaitwa Discovery ID,Kuna cases nyingi sana unsolved na pia kipindi kinaitwa perfect murder ndani yake,ni channel nzuri Sana na kiukweli watu wanaacha Sana alama na kupelekea kukamatwa kwenye baadhi ya cases
 
Back
Top Bottom