Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Mkuu wauaji wote wangelikuwa wanakamatwa.

Kuna mauaji mengine hata Polisi hukosa pa kuanzia, kesi za nmna hiyo zipo.
Ni suala la muda tu labda police waamue tu kuacha kwa sababu mbalimbali kumbuka mambo ya ufatiliaji ni gharama zinatumika je bajeti hio ipo.Pia interest ya wenye kesi hio mfano kama hakuna anaefatilia police watashughulikaje nayo kwa faida ipi.
Zipo fact nyingi
 
Aaah wapi,
Kwanza Tanzania ndo rahisi kufanya uhalifu na ukapotea kimya kimya

maana uku ata serikali yenyewe Haina bajeti ya kufanya upelelezi.

Yaani upelelezi WA bongo unategemea na mfuko WA aliefanyiwa uhalifu ukoje.

Bongo Sio ajabu umepeleka kesi kituoni, afu afande mwenye kesi Yako anakuomba Ela ya vocha ampigie mgambo ili muongozane mkamkamate mhalifu

Na usipotoa Ela ya vocha, mhalifu akamatwi 😀
Bongo unaweza kutwa na hatia ya jinai mara , na ukafungwa miaka 15, ila baada ta mda kidogo,ukakutwa huko nachingwea unazurura tu.🤔
 
Matukio mengi ya mauji hufanyika sirini lakini huja kuwa dhahiri tena kwenye mwanga mkali

Wazungu wanasema " no perfect murder"
Murder ikitendeka na isijulikane labda vyombo vya uchunguzi visiamuwe kuingia kazini

Ukitenda jinai ya murder Kuna uhakika asilimia 💯 utajulikana na ushahidi utakutia hatiani
Jiweke mbali na jinai hii

Kesi na upelelezi vinaweza chukua hata miaka 30 lakini amini wapelezi watakutia hatia na uovu utawekwa wazi

Hapa nitatoa baadhi ya hujuma maarufu hapa Tanzania

1. Mauaji ya Milembe Suleimani
Hawa wauaji walikuwa smart, jinsi walivyo mlaghai hadi kumpeleka site,
Kuzuia mawasiliano, kuficha simu na vifaa au silaha
Lakini wakasahau chupa ya fanta, na wapelelezi walivoikuta wakachukua vinasaba na kugundulika kuwa aliishika mmoja wa mtuhumiwa na kilichofuata mambo yalikuwa kwenye mwanga wa jua kali

2. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya KHamis Luwoga.
Huyu bwana alimuuwa mke wake huko Kigomboni kwenye jumba lake kifahari.

Vyote alicheza smart, kuanzia kuchoma mwili moto na kutupa majibu shambani Kwake Kibiti

Tatizo akapanic na kujitumia SMS Kwa kutumia simu yake wake
Sms zilivyofutiliwa ikandulika alituma sms wakiwa umbali mdogo yani kama walikaa pamoja
Vile ku report kesi 1 vituo tofauti vya police
Na kuacha mkoba wa mkewe ambao alikuwa hawezi kuuacha
Ushahidi ulivopeleka mahakamani Luwoga alicheka na kukiri kosa mwenyewe

3 Mauaji ya RPC Barlow 2012 Mwanza

Hapa wauaji walivamia na kumuua kamanda nakufanikiwa KutorokA eneo la tukio
Kipengele kikaja walishika gari na maganda ya risasi
Finger Print zilivochukulia, mambo yakawa dhahiri na hukumu ya kifo Kwa watu 4 ikafuata

4 Mauaji ya dada wa Msuya
Huyu Binti alikuwa kwenye migogoro ya mirathi na mjane wa Msuya
Huyu Binti alichinjwa kama mbuzi wa Vingunguti
Wauaji wakitenda yote, lakini wakasahau panga
Uchunguzi ukaanza Kwa watuhumiwa na mke wa Hayati Msuya alikutwa na hatia ya kufadhili na hivo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini hali iliyotuacha mdomo wazi alishinda rufaa yake na kuachiwa huru na mahakama

5. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya Bageni 2006
Bageni alikuwa RCO kinondoni
Alipanga njama za kuwauwa wafanya biashara 4, kati ya hao watatu walikuwa ndugu wa damu
Inasemekana aliwapora million 200 na madini
Kwa mamlaka yake aliita press na kutangaza kuwauwa majambazi waliokuwa na silaha
Rais Kikweta alivopewa za kikachero aliunda time ya majaji kuchunguza na mambo Bageni aliyotenda gizani yalikuwa wazi kama uchi wa mbuzi

Hizi ni baadhi ya kesi maarufu ila zipo nyingi mtaani ambazo watenda jinai ya murder hawakutoboa licha ya kufanya uhalifu huu sirini na gizani

Hapa nasubiri hukumu ya mtoto Asimwe wa Muleba Kagera aliyekuwa albino, ambayo mauaji hayo alihusishwa baba yake mzizi na Padre wa Kanisa katoliki
Bado Kesi nyingi hazijafahamika

1. Ali Kibao
2. Deus Soka na wenzake akina Mrai
3. Ben Saanane
4. Azory Gwanda
5. Mo
6. Kesi ya Lissu
7. Aliyemteka Roma
 
Kiukweli,
Bongo hatuna wapelelezi hodari,

Na Ukitaka kuamini hili,
Chunguza watuhumiwa wanapopelekwa mahakamani.

Asilimia kubwa unakuta wamekiri makosa Baada ya kichapo kikali na Sio uchunguzi ule WA kitaalam, tunaita kuunganisha DOTS

YAANI Mtuhumiwa anaenda mahakamani kusomewa Mashtaka, tayari Hana jino, mguu umevunjika,kang'olewa kucha, katumbukiziwa spoku kwny uume n.k
 
Kiukweli,
Bongo hatuna wapelelezi hodari,

Na Ukitaka kuamini hili,
Chunguza watuhumiwa wanapopelekwa mahakamani.

Asilimia kubwa unakuta wamekiri makosa Baada ya kichapo kikali na Sio uchunguzi ule WA kitaalam, tunaita kuunganisha DOTS

YAANI Mtuhumiwa anaenda mahakamani kusomewa Mashtaka, tayari Hana jino, mguu umevunjika,kang'olewa kucha, katumbukiziwa spoku kwny uume n.k
Na kama mtuhumiwa ana koneksheni na watu wakubwa waliohusika utasikka alikufa ghafla akiwa jela.

Hii sio perfect murder bali watu wamelindwa kiaina
 
Hizo zinapigwa Dana dana tu. Mauwaji unless wamekulinda tu lakini huwezi pona hata kidogo.
Sio danadana mkuu, Kuna kesi unakuta inakupasua kichwa balaa.

Yaani kesi ina dead ends kibao,

Yaani unajikuta unachunguza kesi afu unajihisi kama vile inakuja mule mule unakowaza, unajihisi tayar ushamdaka mhalifu kabisa.

Ila unafika mbele,tena hatua za mwishoni kabisa, unajikuta kumbe kote ulikokua unapeleleza ilkua unapoteza muda. UNAEMDHANIA SIYE KABISA.

Na hapo tayar ushapoteza muda na rasilimali fedha na ushawamiinisha maboss wako kesi imekwisha.

Sasa kesi za hivi, ndo wale wapelelezi uchwara WASIO na weledi huamua kumuangushia jumba bovu asiyehusika ili aonekane kweli umepelelezi umekamilika na aliekamatwa ndo mhusika.

Kesi za hivi Mara nyingi huishia mahakamani kamashtakiwa atakua na wakili mzuri, au anafungwa asiye na hatia.
 
Na kama mtuhumiwa ana koneksheni na watu wakubwa waliohusika utasikka alikufa ghafla akiwa jela.

Hii sio perfect murder bali watu wamelindwa kiaina
Wengine Hawaii jela,bali anahamishwa nchi au mkoa, afu ndo imetoka hiyo
 
T
Kila jambo lifanyikalo huacha traces.
Traces zinaweza kuachwa Sana tu,
Ila je, ni wote mnaweza kuziona ?,

Hapa ndo levo ya wapelelezi hutofautiana mkuu.

Umesahau lile tukio la ugaidi Zanzibar?

Bongo na Zanzibar walifeli kumpata mhalifu, wakaomba msaada FBI,

Yule mhalifu aliodakwa Kwa picha ya kuchorwa na penseli ambako Shahid pekee aliekua aliemuona mhalifu alkua ni Mtoto WA miaka 4.
 
Nikiwaga na wasaa wa kuangalia TV moja ya channel zangu pendwa ni DISCOVERY ID pale mjini DSTV

Kuna mapindi ya upelelezi wa case mbali mbali kuanzia za mauaji, wizi, utekaji nk
Zipo zilizo kuwa solved na ambazo ni unsolved

Ila ukiangalia hiyo channeli ndio utajua law enforcers wa wenzetu wanafanya kazi kweli kweli sio utani
Jamaa wanachungunza hadi unaogopa

Njoo bongo sasa
 
Ukitaka kujua bongo ni holela holela,
Angalia jinsi crime scene inavokua treated Baada TU ya tukio kutokea.

1. Ni Mara chache Sana kukuta utepe kuzunguka eneo la tukio ili kuzuia kuharibu ushahidi.

2. Unakuta mpelelezi Hata hajamaliza Hata kukusanya ushahidi eneo la tukio, tayar keshaita press conference na hapo hapo anatamka wazi kua mtuhumiwa anaehisiwa na mashahidi eneo la tukio atafikishwa mahakamani kujibu Mashtaka yanayomkabili.
 
Uyo zodiak mbona alishadakwa kitambo Sana
Gary francis poste? Kama ni huyo jamaa basi jua bado haijawa officially confirmed maana kwa muda mredu walikuwa proposed watu tofauti tofauti lakini hakuna hata mmoja aliyethibitika .
 
Back
Top Bottom