Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Nikiwaga na wasaa wa kuangalia TV moja ya channel zangu pendwa ni DISCOVERY ID pale mjini DSTV

Kuna mapindi ya upelelezi wa case mbali mbali kuanzia za mauaji, wizi, utekaji nk
Zipo zilizo kuwa solved na ambazo ni unsolved

Ila ukiangalia hiyo channeli ndio utajua law enforcers wa wenzetu wanafanya kazi kweli kweli sio utani
Jamaa wanachungunza hadi unaogopa

Njoo bongo sasa
Bongo unaona WAHALIFU wale pale wanapiga tukio, unapg simu polisi waje haraka, unaambiwa gari Haina mafuta, tuma Ela ya mafuta kwanza.
 
Matukio mengi ya mauji hufanyika sirini lakini huja kuwa dhahiri tena kwenye mwanga mkali

Wazungu wanasema " no perfect murder"
Murder ikitendeka na isijulikane labda vyombo vya uchunguzi visiamuwe kuingia kazini

Ukitenda jinai ya murder Kuna uhakika asilimia 💯 utajulikana na ushahidi utakutia hatiani
Jiweke mbali na jinai hii

Kesi na upelelezi vinaweza chukua hata miaka 30 lakini amini wapelezi watakutia hatia na uovu utawekwa wazi

Hapa nitatoa baadhi ya hujuma maarufu hapa Tanzania

1. Mauaji ya Milembe Suleimani
Hawa wauaji walikuwa smart, jinsi walivyo mlaghai hadi kumpeleka site,
Kuzuia mawasiliano, kuficha simu na vifaa au silaha
Lakini wakasahau chupa ya fanta, na wapelelezi walivoikuta wakachukua vinasaba na kugundulika kuwa aliishika mmoja wa mtuhumiwa na kilichofuata mambo yalikuwa kwenye mwanga wa jua kali

2. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya KHamis Luwoga.
Huyu bwana alimuuwa mke wake huko Kigomboni kwenye jumba lake kifahari.

Vyote alicheza smart, kuanzia kuchoma mwili moto na kutupa majibu shambani Kwake Kibiti

Tatizo akapanic na kujitumia SMS Kwa kutumia simu yake wake
Sms zilivyofutiliwa ikandulika alituma sms wakiwa umbali mdogo yani kama walikaa pamoja
Vile ku report kesi 1 vituo tofauti vya police
Na kuacha mkoba wa mkewe ambao alikuwa hawezi kuuacha
Ushahidi ulivopeleka mahakamani Luwoga alicheka na kukiri kosa mwenyewe

3 Mauaji ya RPC Barlow 2012 Mwanza

Hapa wauaji walivamia na kumuua kamanda nakufanikiwa KutorokA eneo la tukio
Kipengele kikaja walishika gari na maganda ya risasi
Finger Print zilivochukulia, mambo yakawa dhahiri na hukumu ya kifo Kwa watu 4 ikafuata

4 Mauaji ya dada wa Msuya
Huyu Binti alikuwa kwenye migogoro ya mirathi na mjane wa Msuya
Huyu Binti alichinjwa kama mbuzi wa Vingunguti
Wauaji wakitenda yote, lakini wakasahau panga
Uchunguzi ukaanza Kwa watuhumiwa na mke wa Hayati Msuya alikutwa na hatia ya kufadhili na hivo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini hali iliyotuacha mdomo wazi alishinda rufaa yake na kuachiwa huru na mahakama

5. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya Bageni 2006
Bageni alikuwa RCO kinondoni
Alipanga njama za kuwauwa wafanya biashara 4, kati ya hao watatu walikuwa ndugu wa damu
Inasemekana aliwapora million 200 na madini
Kwa mamlaka yake aliita press na kutangaza kuwauwa majambazi waliokuwa na silaha
Rais Kikweta alivopewa za kikachero aliunda time ya majaji kuchunguza na mambo Bageni aliyotenda gizani yalikuwa wazi kama uchi wa mbuzi

Hizi ni baadhi ya kesi maarufu ila zipo nyingi mtaani ambazo watenda jinai ya murder hawakutoboa licha ya kufanya uhalifu huu sirini na gizani

Hapa nasubiri hukumu ya mtoto Asimwe wa Muleba Kagera aliyekuwa albino, ambayo mauaji hayo alihusishwa baba yake mzizi na Padre wa Kanisa katoliki
kwa Bageni,aliyeita press no Abdalah Zombe siyo Bageni
 
Andiko zuri. Ni sahihi kwamba ni ngumu kuua na kuziba mianya ya kufuatiliwa. Ushahidi wa kisayansi kama DNA, alama za vidole, mawasiliano ya simu ni ngumu kukuacha salama. Lakini pia kila anayeua kwa kawaida huwa na hamasa (motive) fulani ambayo huchangia kumhusisha na mauaji. Lakini kuna scenario ukizifikiria nadhani zina ugumu mno kumkamata muuaji.

Hebu chukulia mtu anaambiwa na mganga wa kienyeji aue mtu yeyote tu ili apate utajiri. Huyo mtu anasafiri umbali kutoka mkoa mmoja mpaka mwingine. Anaacha simu yake kule anapoishi. Anafika kule alikoenda anatafuta kichaka anajificha usiku.

Anamvizia mpita njia anampiga na rungu moja la kichwa ambalo linamdondosha chini. Anamuongeza marungu mengine matatu mpaka anaridhika kuwa yule mtu amekufa. Hamgusi mahala popote na anaondoka na rungu lake anaenda kulitupia mbali mno. Je, kwa namna gani huyu mtu anaweza kupatikana?
Kwa uwezo wa mungu atapatikana
 
Kuna watu anakufumania Ila anaweka kiporo, afu anakuua Kwa simu ya polepole, ndani ya miez 6+ unaugulia kitandani, afu ndo anakumalizia kabisa.

Ripoti ya kifo inasomeka ni amefariki baada ya kuugua MDA marefu.

Kumbe tayar Kuna mtu keshalipiza kisasi chake na anaendelea na maisha yake
Aahhh
Nakumbuka ile stori ulileta ya jamaa aliuliwa polepole na dawa ya macho
Halafu hakuna ushahidi
Wawekee link hapa wasome wenyewe kuwa you can get away with murder
 
Youtube kuna video wanaziita "fbi files" nazikubali sana aina hizi za video case mbalimbali zilivokua solved. Majinanya channel zingine yamenitoka
Kuna True crimes, Crime investigation, catching a Killer. Serial killers
Zipo nyingi sana na unajifunza mengi sana kwenye ulimwengu wa Crimes
 
Burudani ya serial killer huwa ni kuona jinsi gani polisi Wana hangaika kumtafuta.

Kinachowaponza serial killer wengi Huwa ni kulewa sifa, hapo ndo uwa wanakamtwa
Kwa kumbukumbu zako bongo tushawahi kua na serial killers mkuu?
 
Ni kweli Kila tukio huacha alama,

Ila zipo kesi kibao mpk leo zimekosa alama na hazijawa solved.

Marekani Wana utaratibu, kesi ikizidi miaka 100 haijasoviwa, Hilo faili wanafunga.
Ni kweli zipo crimes ambazo zimekuwa pasua kichwa kwa wapelelezi
Ila kuna moja nimeangalia juzi kesi ya mtoto wa kike alieuwawa mwaka 1964 akiwa na umri wa miaka 9
Kesi walishindwa wabobezi wa kila aina ila walishindwa
Baada ya miaka 57 kijana mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ametatua hiyo kesi kwa kutumia Genetic genealogy

Very interesting hebu isome
Screenshot_20250228_155405_Chrome~2.png
 
Ni kweli zipo crimes ambazo zimekuwa pasua kichwa kwa wapelelezi
Ila kuna moja nimeangalia juzi kesi ya mtoto wa kike alieuwawa mwaka 1964 akiwa na umri wa miaka 9
Kesi walishindwa wabobezi wa kila aina ila walishindwa
Baada ya miaka 57 kijana mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ametatua hiyo kesi kwa kutumia Genetic genealogy

Very interesting hebu isome View attachment 3253323
Hii ni ajabu
 
Ni kweli zipo crimes ambazo zimekuwa pasua kichwa kwa wapelelezi
Ila kuna moja nimeangalia juzi kesi ya mtoto wa kike alieuwawa mwaka 1964 akiwa na umri wa miaka 9
Kesi walishindwa wabobezi wa kila aina ila walishindwa
Baada ya miaka 57 kijana mwanafunzi mwenye umri wa miaka 18 ametatua hiyo kesi kwa kutumia Genetic genealogy

Very interesting hebu isome View attachment 3253323
Genetic geneology mzuri sana sema ubaya unakuta mara nyingi perpetrators wameshakufa, ni mara chache wanakuwa hai.

Nilikuwa nafuatilia real crime tv series ya case za UK, walikuwa wanatumia pia, ila kama 90% wahuska walikuwa washafarika.
 
Genetic geneology mzuri sana sema ubaya unakuta mara nyingi perpetrators wameshakufa, ni mara chache wanakuwa hai.

Nilikuwa nafuatilia real crime tv series ya case za UK, walikuwa wanatumia pia, ila kama 90% wahuska walikuwa washafarika.
Kweli kabisa hata huyo jamaa aliekabaka hako katoto alikufa akiwa na miaka 38 tu
 
Hii ni ajabu
Sana mkuu, ila wenzetu wanatumia resources nyingi na hela nyingi sana kwa kufuatilia mauwaji, na pia wanajali sana utu
Sisi fedha na utaalamu ndio duni
Imagine kuna wakati unasikia kuna mtu kapotea leo siku ya tano (ulaya) kesi wanaingia askari zaidi ya 100 kufanya upelelezi
Sisi sasa daa
 
Sana mkuu, ila wenzetu wanatumia resources nyingi na hela nyingi sana kwa kufuatilia mauwaji, na pia wanajali sana utu
Sisi fedha na utaalamu ndio duni
Imagine kuna wakati unasikia kuna mtu kapotea leo siku ya tano (ulaya) kesi wanaingia askari zaidi ya 100 kufanya upelelezi
Sisi sasa daa
Huku mtu akifa kama ndugu hawatafuatilia hakuna kitakachoendelea
 
Aaah wapi,
Kwanza Tanzania ndo rahisi kufanya uhalifu na ukapotea kimya kimya

maana uku ata serikali yenyewe Haina bajeti ya kufanya upelelezi.

Yaani upelelezi WA bongo unategemea na mfuko WA aliefanyiwa uhalifu ukoje.

Bongo Sio ajabu umepeleka kesi kituoni, afu afande mwenye kesi Yako anakuomba Ela ya vocha ampigie mgambo ili muongozane mkamkamate mhalifu

Na usipotoa Ela ya vocha, mhalifu akamatwi 😀
Dah! Mwanangu umeua!👋👋
 
Hata wanaojaribu kutengeneza perfect murder wanaoshia kutengeneza perfect prosecution
 
Back
Top Bottom