Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Hakuna murder case isiyoacha alama/ushahidi

Unaongea na kuandika mambo ambayo hauyajui na hauna ufahamu nayo.

Kitu ambacho unabidi kujua wanoratibu mauaji sio wanaoua Ila wanaouwa huwa wanakuwa wametumwa kutekeleza Kazi maalumu ya WATU.
Ukishapata muuaji ni sehemu ya kuanzia kupata walioratibu na wafadhili

Rejea kesi mauji ya Milembe aliyeratibu ni Daifath lakini hata kwenye tukio hakufika ila alijulikana nae akahukumiwa hukumu ya kifo
 
Kwenye murder yoyote cha kwanza ni kuangalia na ku checklist motives zote ambazo mtu angeweza kuuliwa. Mke wako akiuliwa hata na vibaka kwa bodaboda barabarani polisi wanaanza kufatilia motives zozote na kwa kawaida Mume unakua suspect. Migogoro,mali,ugomvi na matishio yote kwnye ndoa yenu watayajua na wanaunganisha dots ndio maana most of the time watu wengi wanauliwa kwa sababu na ukifuatilia sababu utampata muhusika.

Serial killers au siku uamue tu umuue mtu random, kwa kificho itakua ngumu kupatikana. Ndio maana serial killers hawapatikani kwa kuua mtu mmoja mtu anaua kadhaa mpaka anadakwa.
 
Matukio mengi ya mauji hufanyika sirini lakini huja kuwa dhahiri tena kwenye mwanga mkali

Wazungu wanasema " no perfect murder"
Murder ikitendeka na isijulikane labda vyombo vya uchunguzi visiamuwe kuingia kazini

Ukitenda jinai ya murder Kuna uhakika asilimia 💯 utajulikana na ushahidi utakutia hatiani
Jiweke mbali na jinai hii

Kesi na upelelezi vinaweza chukua hata miaka 30 lakini amini wapelezi watakutia hatia na uovu utawekwa wazi

Hapa nitatoa baadhi ya hujuma maarufu hapa Tanzania

1. Mauaji ya Milembe Suleimani
Hawa wauaji walikuwa smart, jinsi walivyo mlaghai hadi kumpeleka site,
Kuzuia mawasiliano, kuficha simu na vifaa au silaha
Lakini wakasahau chupa ya fanta, na wapelelezi walivoikuta wakachukua vinasaba na kugundulika kuwa aliishika mmoja wa mtuhumiwa na kilichofuata mambo yalikuwa kwenye mwanga wa jua kali

2. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya KHamis Luwoga.
Huyu bwana alimuuwa mke wake huko Kigomboni kwenye jumba lake kifahari.

Vyote alicheza smart, kuanzia kuchoma mwili moto na kutupa majibu shambani Kwake Kibiti

Tatizo akapanic na kujitumia SMS Kwa kutumia simu yake wake
Sms zilivyofutiliwa ikandulika alituma sms wakiwa umbali mdogo yani kama walikaa pamoja
Vile ku report kesi 1 vituo tofauti vya police
Na kuacha mkoba wa mkewe ambao alikuwa hawezi kuuacha
Ushahidi ulivopeleka mahakamani Luwoga alicheka na kukiri kosa mwenyewe

3 Mauaji ya RPC Barlow 2012 Mwanza

Hapa wauaji walivamia na kumuua kamanda nakufanikiwa KutorokA eneo la tukio
Kipengele kikaja walishika gari na maganda ya risasi
Finger Print zilivochukulia, mambo yakawa dhahiri na hukumu ya kifo Kwa watu 4 ikafuata

4 Mauaji ya dada wa Msuya
Huyu Binti alikuwa kwenye migogoro ya mirathi na mjane wa Msuya
Huyu Binti alichinjwa kama mbuzi wa Vingunguti
Wauaji wakitenda yote, lakini wakasahau panga
Uchunguzi ukaanza Kwa watuhumiwa na mke wa Hayati Msuya alikutwa na hatia ya kufadhili na hivo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini hali iliyotuacha mdomo wazi alishinda rufaa yake na kuachiwa huru na mahakama

5. Hukumu ya Kunyongwa hadi kufa ya Bageni 2006
Bageni alikuwa RCO kinondoni
Alipanga njama za kuwauwa wafanya biashara 4, kati ya hao watatu walikuwa ndugu wa damu
Inasemekana aliwapora million 200 na madini
Kwa mamlaka yake aliita press na kutangaza kuwauwa majambazi waliokuwa na silaha
Rais Kikweta alivopewa za kikachero aliunda time ya majaji kuchunguza na mambo Bageni aliyotenda gizani yalikuwa wazi kama uchi wa mbuzi

Hizi ni baadhi ya kesi maarufu ila zipo nyingi mtaani ambazo watenda jinai ya murder hawakutoboa licha ya kufanya uhalifu huu sirini na gizani
Andiko zuri. Ni sahihi kwamba ni ngumu kuua na kuziba mianya ya kufuatiliwa. Ushahidi wa kisayansi kama DNA, alama za vidole, mawasiliano ya simu ni ngumu kukuacha salama. Lakini pia kila anayeua kwa kawaida huwa na hamasa (motive) fulani ambayo huchangia kumhusisha na mauaji. Lakini kuna scenario ukizifikiria nadhani zina ugumu mno kumkamata muuaji.

Hebu chukulia mtu anaambiwa na mganga wa kienyeji aue mtu yeyote tu ili apate utajiri. Huyo mtu anasafiri umbali kutoka mkoa mmoja mpaka mwingine. Anaacha simu yake kule anapoishi. Anafika kule alikoenda anatafuta kichaka anajificha usiku.

Anamvizia mpita njia anampiga na rungu moja la kichwa ambalo linamdondosha chini. Anamuongeza marungu mengine matatu mpaka anaridhika kuwa yule mtu amekufa. Hamgusi mahala popote na anaondoka na rungu lake anaenda kulitupia mbali mno. Je, kwa namna gani huyu mtu anaweza kupatikana?
 
Murder chache sana suspects wanakamatwa na kutiwa hatiani wengi wanashinda kesi, kwenye mauaji hakuna ushahidi wa kusikia, ushahidi wenye nguvu ni eyewitness au ushahidi wa kisayansi ukikosekana huo ushahidi hata kama mtu kaua yeye ni ngumu sana kufungwa otherwise akiri mwenyewe ila asipokiri atakaa mahabusu muda mrefu baadae ataachiwa au baada ya kufungwa atakata rufaa na kuwa huru

hiyo mifano yako ni michache na yenye public interest muda mwingine hakimu anafunga macho na kumfunga mtu kutokana na msukumo uliopo kwenye jamii, japo siungi mkono matendo hayo lakini kusema kila anaeua anafahamika hiyo ni uongo mkubwa, siyo Tanzania tu duniani kote.
 
uzii umeeleweka sana, ila Kwa kuongezea tu kuna aina tofauti ya tukio lolote la mauaji.
Organized killer... Hili ni tukio ambalo muuaji anakua amejipanga na ni ngumu sana kubaini kwani tukio Zima Huwa linaanzia kwenye mchoro, pia dhana zote za kazi vinaandaliwa, mistakes kidogo tu unaunguza picha, muuaji anajua kitu anachokifanya na kuhakikisha haachi ushahidi...yako matukio mengi ambayo mpka kesho hajapata kujulikana, ndio maana hata wapelezi wametofaiutiana uwezo, wako wabobevu zaidi, ama international.
Disorganized killer... Hili ni tukio ambalo muuaji anakua hajajipanga, anaweza akatumia hata silaha aliyoikuta Kwa target, hakuna mpango kabla ya tukio, ushahidi unapatikana kirahisi, muuaji hata grooves havai anakuja mzimamzima, hivyo hata wapelezi wanapata pa kuanzi.... Nawasilisha
 
Murder chache sana suspects wanakamatwa na kutiwa hatiani wengi wanashinda kesi, kwenye mauaji hakuna ushahidi wa kusikia, ushahidi wenye nguvu ni eyewitness au ushahidi wa kisayansi ukikosekana huo ushahidi hata kama mtu kaua yeye ni ngumu sana kufungwa otherwise akiri mwenyewe ila asipokiri atakaa mahabusu muda mrefu baadae ataachiwa au baada ya kufungwa atakata rufaa na kuwa huru

hiyo mifano yako ni michache na yenye public interest muda mwingine hakimu anafunga macho na kumfunga mtu kutokana na msukumo uliopo kwenye jamii, japo siungi mkono matendo hayo lakini kusema kila anaeua anafahamika hiyo ni uongo mkubwa, siyo Tanzania tu duniani kote.
Nimekuelewa sana mkuu
 
Back
Top Bottom