Usahihi kamili wa hoja yako ni huu:
"Hakuna serikali yoyote ya kidunia (ikiwemo ya Tanzania) inaweza kupambana na kupingana na KANISA LA MUNGU na serikali hiyo ikaendelea kuwepo na kusimama..!"
TEC ni sehemu (kipande tu cha kanisa la Mungu). Lakini ukweli mkuu ni kuwa wapo watu wengi (jeshi la Mungu aliye hai hapa Tanzania) kote nchini (ukiacha TEC ambao wametoa official statement ya kukataa mpango huu wa Rais samia) ambao wanafunga na kuomba mchana na usiku kuhakikisha kuwa Mungu anaiponya nchi hii toka Kwa hayawani hawa..
Na mfano ulio dhahiri wa kuwa KANISA LA MUNGU liko kazini ni Mch. Mbarikiwa Mwakipesile na wafuasi wake huko Mbeya wanaomba usiku na mchana wakisema kwa uwazi bila kificho wala kumung'unya maneno kuwa Mungu aiangushe na kuipoteza CCM na serikali yake huku matangazo ya ibada zake yakirushwa live katika channel yake YouTube...
But all in all, huu ulioandika kwa ujumla wake ndiyo ukweli na wote wanaopingana na KANISA LA MUNGU wanajisumbua na kujipaka kinyesi tu...
Na ni kweli hii 👇👇👇 statement ya TEC ndiyo iliyomaliza na kuua kila kitu kabisa..!!
".....Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.
This is bold and most importantly authoritative statement. No any other authority will surpass this!!