Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Nashauri TEC ndio liwe Bunge letu.
Maana wanaiwezo wa kusoma na kuitahadharisha Serikali mambo ya msingi kama mikataba ya Kimangungo.
Nawashangaa sana wanaoipinga TEC.
TEC imeishauri vizuri Serikali dhidi ya Hila Za Waarabu na Vibaraka wao wa humu nchini wanao waona Waarabu kama Miungu yao.
Huku Bunge likipiga makofi pwa pwa pwa na kushangilia bila hata ya kuusoma na kuuelewa huo Mkataba.

TEC ndio liwe Bunge letu.
Hao wabunge waache wakutane Dodoma na kula ruzuku ya Serikali maana ndicho wanancho kipigania.
Ikiwezekana libinafsishwe kwa DP World.

Mkuu, sikubaliani na hoja yako! HAPANA.

Waachwe TEC waendelee na kazi zao katika jamii.

Kazi wanayoifanya ni kubwa kuliko hii unayotaka kuwapa!
 
Hebu punguza uongo kidogo Benjamin Mkapa aliwanyoosha kanisa Katoliki mpaka wenyewe waliomba po ingawa yeye mwenyewe mkatoliki hebu muulize vizuri Pengo awamu ya pili ya utawala wa Ben ilikuwaje? chamoto alikiona na ndio Raisi pekee aliyekuwa anabalance teuzi zake kati ya waislam na wakristo btn 50%-45%,.
 

Alisema Corona hakuna Tanzania na akapiga marufuku kuvaa barakoa.Wakatoliki chini ya Fr.Kitima wakasisitiza kuwa Corona ipo na imewaua baadhi ya waumini,mapadre,maaskofu,masista hata mabruda na kuwasihi kuvaa barakoa hata kwenye mikutano ya Magufuri jambo ambalo hakupenda kabisa.Badala yake yeye aligeuka kuwa Papa wa kuwafokea viongozi hao na kuwaambia hawana imani.Unaona kilichotokea?Wakatoliki wanathamini afya na uhai wa waumini wao na ndio maana hata kwenye mkataba huu wa DP World wamejitahidi kuonya ila sisi bado tunawaona kama wanaingilia mambo ya serikali.Uzuri ni kuwa majibu ni hapa hapa duniani.
Magufuli akupiga marufuku barakoa,ila alishauri barakoa za kutoka nje tuwe na tahadhari nazo ikiwezekana mtu ashone ya kwake.

Alafu kwanini mnapenda sana kumpaka matope Magufuli,Magufuli hakuwai kurumbana na taasisi yeyote ya dini hii yako ni uzushi mtupu hata waraka aukutolewa na TEC kwa hili la Covid 19 na Magufuli.
 
TEC ndo kitu gani ktk nchi? Acha uzuzu.
Serikali ina vyombo vya DOLA vyote.
TEC haina vyombo vya DOLA., ni dini tu.
Je TEC ina polisi? Ina magereza? ina TISS? nk.
Serikali ikiamua kufanya ya kwake TEC itapotea kwenye ramani ya Tz ndani ya muda mfupi sana. Be ware. Usicheze na serikali.
Good✔
 
Hebu punguza uongo kidogo Benjamin Mkapa aliwanyoosha kanisa Katoliki mpaka wenyewe waliomba po ingawa yeye mwenyewe mkatoliki hebu muulize vizuri Pengo awamu ya pili ya utawala wa Ben ilikuwaje? chamoto alikiona na ndio Raisi pekee aliyekuwa anabalance teuzi zake kati ya waislam na wakristo btn 50%-45%,.
Unaweza kuja na taarifa rasmi na evidence ya baadhi ya matukio
 
Wapo waislamu wanaozungumza kwamba Tanzania ipo chini ya Mfumo kristo, na yupo Muislamu Moja kiongozi anayehamasisha waislam wainuke wajitetee. Inajenga dhana gani

Hiyo ni haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kutoa maoni yao. Mwisho wa siku ukweli utajisimamia wenyewe. Kinacho shangaza wengine na kustaabisha ni wale wanao hangaika kupambana na Wakili Mwambukuzi na linaloitwa genge lake badala ya kufanyia kazi na kurekebisha kile kilicho lipa hili genge umaarufu wa ghafla.
 
Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa!
Nilidhani kuna mifano kwa kila rais (awamu) kumbe stori
 
wachoyo wa nini sasa, wamekunyima ubwabwa? na mgao gani mliodanganywa kwamba maaskofu wa katoliki huwa wanapewa? ukitaka kuwapa hao rushwa nenda kaanze na papa. zote hizo ni propaganda mnadanganyana kwenye tv iman huko baada ya kushiba kalmati.
Walikula mgao wa escrow hata walipogundua ni pesa chafu wamegoma kurudisha hata senti, watulie huko kanisani huku ni maendeleo kwa wote , wao wanawaza dili tu saa zote
 
Wewe mfano una elimu gani hata ya kumpita mkenya?🤣🤣

Mtu mzima halafu hujielewi !?


Ujinga na ukatoliki wenu ndo umemaliza elimu ya Tz ,kilichobaki ni kusambaza tamaduni zao ila hao maprofessor kama wote hawana kitu kichwani.
Wamekariri tu ila akili zenyewe hawana
 
Walikula mgao wa escrow hata walipogundua ni pesa chafu wamegoma kurudisha hata senti, watulie huko kanisani huku ni maendeleo kwa wote , wao wanawaza dili tu saa zote
Una ushahidi kwamba pesa za escrow zilipokelewa kwenye account ya Baraza la Maaskofu Tanzania na Maaskofu wakazichukua zikagawanywa majimboni Tanzania, na una ushahidi wa ujenzi wa kanisa, shule au hospitali ya kanisa ambapo fedha hizo zilielekezwa kuwezesha ujenzi huo? Ama una ushahidi kwamba fedha hizo zilitumika kuendesha PASADA, convent au shule iwe ya sekondari au seminari?

Anyway una orodha ya Maaskofu 38 waliosaini kupokea fedha hizo mmoja mmoja? Kama hakuna basi ukae kimya milele! Personal issue ya askofu na aliyempa Hela (man to man) haiwezi kuwa ya kanisa na haiwezi kuizuia Baraza kutoa maoni yake katika maslwa ya kijamii na kiuchumi ya taifa hili kwakua na yeye na mdau wa maendeleo..
 
Magufuli akupiga marufuku barakoa,ila alishauri barakoa za kutoka nje tuwe na tahadhari nazo ikiwezekana mtu ashone ya kwake.

Alafu kwanini mnapenda sana kumpaka matope Magufuli,Magufuli hakuwai kurumbana na taasisi yeyote ya dini hii yako ni uzushi mtupu hata waraka aukutolewa na TEC kwa hili la Covid 19 na Magufuli.
Ndugu yangu Magufuri hapakwi matope hata siku moja bali ni yale aliyoyatenda akiwa hai ndiyo tunayashuhudia.Mfano leo mpaka TEC wameandika waraka kutokubaliana na swala la DP World,wanasiasa wamemipinga,wanaharakat wamepinga,CHADEMA wamepinga,Wanasheria wamepinga,Wasomi mbalimbali wamepinga,Viongozi wastaafu wamepinga hata Wana ccm wamepinga.Ila mkataba huo ukianza kufanya kazi na bahati mbaya ukaleta hasara isiyolipika mtakuja kusema tunampaka matope Mama Samiah maana siyo yeye aliyesaini huo mkataba.
Sisi hatuamini katika uongo,bali tunaamini katika ukweli maana 1961 tulipata uhuru ili tuwe huru na tufanye kazi bila kumtegemea mtu yeyote.
 
Walikula mgao wa escrow hata walipogundua ni pesa chafu wamegoma kurudisha hata senti, watulie huko kanisani huku ni maendeleo kwa wote , wao wanawaza dili tu saa zote
SEMA ALIKULA, kwasababu ni askofu mmoja tu. kwahiyo mtu mmoja akifanya kosa wote wamefanya? ustaadhi wa zanzibar askali aliyejirekodi anapumuliwa tuseme wote wanapumuliwa?
 
Raisi Samia lazima awe makini na watu wanaomzunguka.
Wanamgombanisha na Watanganyika.
Hao wapigaji.

Wapigaji (Wanaume) kwa niaba ya Dr. Mongela.

Ila Raisi lazima atuombe radhi Watanganyika.
Tulisha uzwa kwa Waarabu.
 
SEMA ALIKULA, kwasababu ni askofu mmoja tu. kwahiyo mtu mmoja akifanya kosa wote wamefanya? ustaadhi wa zanzibar askali aliyejirekodi anapumuliwa tuseme wote wanapumuliwa?
Yule si kiongozi wa dini
 
Back
Top Bottom