Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Hakuna mwanasiasa/Rais aliweza kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na akashinda!

Kwa wajuzi wa historia ya Tanzania wameishajua kuwa Tamko la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) la kuhusu mkataba baina ya serikali ya Tanganyika AKA Tanzania na DP World ni kaa la moto mkali ambao unazidi kumchoma vikali muhusika mkuu na chama chake mpaka watakapokufa kisiasa mapema kama wataendelea kushupaza shingo.

Katika historia ya Tanzania hakuna mwanasiasa au Rais aliwahi kupambana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) halafu akashinda. Haijawahi kutokea na haitawahi kutokea katika miaka hii ya karibuni. Kufanya hivyo ni kujiangamiza kisiasa(political suicide).

Unaweza kuukataa huu ukweli lakini kuukataa kwako hakuwezi kuubadilisha kuwa uongo.

Mwl. Nyerere pamoja na nguvu zote za kikatiba alizokuwa nazo katika utawala wake lakini hakuwahi kutumia nguvu katika kupitisha ajenda zake za kisiasa pale ambapo maaskofu walikuwa na shaka au kumpinga. Alitumia nguvu ya ushawishi wa hoja kwa kujadiliana nao mpaka wakamwelewa na kukubali.

Nguvu za Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) zimeendelea hivyo katika tawala zote nchini. Hakuna mwanasiasa mwenye uelewa wa Tanzania na akili timamu aliweza kupuuza sauti ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Muhusika mkuu wa mkataba wa DP World hakutegemea kama TEC wanaweza kutoa waraka mkali kama waliotoa kwa sababu sehemu ya 17 ya waraka imepigilia msumari wa mwisho wa jeneza la mkataba.

TEC IMEITAKA SERIKALI IACHANE NA MKATABA HUU.

Sehemu ya 17 ya waraka wa TEC inasema, “Hivyo tukiwajibika kimaadili, tunaona ni jukumu la serikali kusikiliza wananchi wanaotaka mkataba huu ufutwe. Kwa kuwa tumeonesha kuwa Tanzania tumeshawekeza na kuendeleza bandari, reli na bandari za nchi kavu; niwajibu miradi hii tuiendeshe Watanzania wenyewe huku tukikaribisha ubia tunaoudhibiti wenyewe. Hiki ndicho wananchi wanachokililia kusudi tujenge uwezo wetu wenyewe. Kwa vile tumegundua mapungufu yetu ya uendeshaji wa bandari, tunaweza kujizatiti kurekebisha mapungufu hayo wakati njia za kiuchumi zikibaki mikononi mwetu. Kwa sababu hizo na maelezo yote ya hapo juu, sisi Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania hatuungi mkono Mkataba huu”.

Baada ta waraka kutolewa, muhusika mkuu na genge lake akaanza kuhaha akitafuta jinsi ya kukabiliana nao. Amemtuma kiongozi mkuu wa nchi mstaafu ili ajibu hoja lakini hakufanikiwa kuzima moto, amejaribu kutumia mbinu za kidini kwa kuwatuma baadhi ya mashekhe ili wawajibu TEC katika misingi ya kidini lakini pamoja na juhudi zote, moto wa waraka wa TEC ndio unashika kasi ya kumchoma kisiasa. Ametuma “wajinga” fulani washambulie haiba ya maaskofu badala ya kujibu hoja hawajafanikiwa.

Alichofanya kwa sasa ni kuwatuma baadhi ya viongozi ndani ya serikali kwenda Dubai ili kuwaeleza wenye DP World kuhusu moto unavyowaka nchini ili waangalie namna ya kufanya ili kuondokana na moto mkali kisiasa ili kuepuka maafa ya kisiasa. Kwa hivi karibuni ndege ya Rais imekuwa na safari nyingi za kwenda Uarabuni na kurudi.

Katika hali hiyo ya kutapatapa ametangaza eti tenda ya kukaribisha wawekezaji kwenye bandari Terminal 2 ili ionekane hakutaka kugawa bandari zote kwa DP World wakati mkataba(IGA) unabainisha ni bandari zote na maziwa yote ya Tanganyika AKA Tanzania bara. Mjinga gani atakuja kuwekeza kwenye terminal 2 wakati kuna IGA inasema uwekezaji wowote katika bandari na maziwa nchini lazima kwanza uridhiwe na DP World.
Tumeona pia amemuondoa waziri wa katiba na sheria ili eti ionekane kama ndiye aliyesababisha hili sakata la DP World wakati kwenye IGA kuna saini ya Rais! Huku ni kutapatapa.

Kama isingekuwa waraka wa TEC, mchakato wa kuzifuta Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Rasilimali na Maliasili na Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba inayohousu Rasilimali na Maliasili za Nchi za mwaka 2017 ungefanyika bungeni na hili tangazo lingine la tenda ya kukaribisha wawekezaji lisingetolewa! Hii yote ni imefanyika katika hali ya kutapatapa!
Wale maaskofu wale ni Watanzania kweli kweli.

Mungu awalinde Maaskofu, Msheikh, wachungaji, maulamaa, wanazuoni, wainjilisti, waalimu wa dini na watumishi wote wanaotumikia imani zao hapa Tanzania
 
Punguza hasira na siku zote TEC hawajawahi kuishinikiza au kuitaka serikali juu ya mambo yasiyokua ya manufaa kitaifa in favor ya mambo ya kanisa. Siku zote wamekua wakiadress national issues. na hata katika waraka wao hakuna jambo lolote au statement yoyote iwe kwa uficho au kwa uwazi imejielekeza kwenye maslahi au mahitaji ya kanisa.
Mbona pamoja na nguvu kubwa waliyowekeza kumfanya Padri Slaa awe Rais 2010 lkn waliangukia pua kwa JK
 
Usitake kuchochea kisichokuwepo.

TEC haishindani na serikali, kile sio chama cha siasa. Hakuna vita yoyote kati ya TEC na serikali isipokuwa kuna raia tusioafiki walakini uliojitokeza katika mkataba wa bandari. TEC ni mjumbe wa raia wakatoliki na tusio wakatoliki. SAUTI YA WATU SAUTI YA MUNGU, siyo sauti ya TEC.
 
Mungu yupi Allah, Mungu baba, Mungu mwana , budha, mzimu wa kolelo, Jehova, au mungu jiwe?
Authority ipi ya huu cartel ya kihuni(Mafia)iliyotupwa kule kwa waliostaaribika ulaya na Marekani,?
Mamlaka hayo labda huko kwenye vigango vyao sio kwa serikali.
Mungu - Yehova muumba wa mbingu na nchi na vyote vilivyomo katika Yesu Kristo mwokozi wa ulimwengu ukiwemo wewe. Soma👇👇

Yohana 3:16-18 SUV
"
...Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu..."

Kama huamini hayo☝️☝️ maneno hilo ni tatizo lako la kutoamini. Ila siku hiyo utakuja kushangaa kukumbushwa kuwa alitokea mtu kwenye mtandao mmoja wa kijamii uitwao Jamii Forum akakuambia habari zangu lakini hukuamini..


 
Mkuu, sikia bana, mm maisha yangu nayaweka kwa Mungu, sio kwa wanasiasa wa kibongo hawa, pambana upate kula yako, hapo bandarini lazima atakuja mwekezaji, iwe DPW au Adan Au TICTS kwa hio mkuu, mm sina shida na mbwa gani yupo hapo bandarini, as long as kuna ufanisi, kodi za kijinga hazipo basi sina shida
Kwa kiwango kikubwa nakubaliana na hoja zako!

Ni mjinga anayeweka maisha yake kwa wanasiasa. Wanasiasa ndio wanatakiwa wayaweke maisha yao ya kisiasa kwa wananchi.

Mkataba wa serikali na DP World ungekuwa hauna matatizo hata mimi ningewaunga mkono!
 
Aliye mshauri Mh Rais akae kimya huyo ndio asiyemtakia mema. Unakaje kimya wakati baadhi ya vipengele vya makubaliano ya awali vina ukakasi wa wazi kwa kila mwenye akili timamu kuelewa?

Unaweza kuupotezea waraka wa Maaskofu zaidi ya 30 unao elekezwa kwa namilioni ya wafuasi wao waliokatika kila nyanja ya maisha uijuayo wewe khalafu uwe bado na amani moyoni???, Mungu anahitaji mwenye haki wake mmoja tu kufanya naye kazi. Eliya mmoja aliangamiza makuhani 450 wa mungu baal chini ya Jezeebel???!! CCM na viongozi wenu someni maneno haya ya Biblia, Zaburi 33:16.
Mkuu, hii dhana ya kuwalaumu "washauri" wa Rais mnaitoa wapi? Kwa hiyo huyu Rais hatumii uwezo wake katika kupambanua mambo?
 
hawa jamaa wameletwa na Mungu, wametufumbua macho, pamoja na kwamba bado kuna watu wapo gizani na wengine macho wanayo ila hawataki kuona.
Kwa kweli wamefanya kazi ya kitume katika tamko lao kuhusu mkataba wa serikali na DP World
 
wamissionari au TEC ni kweli wana nguvu pitia historia yao ndiyo chimbuko la ukoloni Afrika, kukomesha biashara ya utumwa,nchi nyingi kupata uhuru etc they are very influencial
Uhuru wakoloni(corporates) waliamua kuachana na ukoloni wa kale na kuja na ukoloni mamboleo,kwa kuwa walifuata malighafi wakabuni njia mpya ya kupata malighafi zilezile bila ya migongano na makoloni yao, biashara ya utumwa kukoma ni baada ya mapinduzi ya viwanda,siyo kanisa,usiwape credit ziso zao
 
Mbona pamoja na nguvu kubwa waliyowekeza kumfanya Padri Slaa awe Rais 2010 lkn waliangukia pua kwa
Angalia utachekwa sana kwenye huu mjadala unapiga Dana Dana na kuruka ruka! Hata yeye akisoma atakushangaa.
 
Kwa kifupi kabisa, Viongozi wa Serikali yetu hawawezi hata kidogo kushindana na TEC.
TEC hawana tabia ya kuropoka ropoka, lakini wana power kweli kweli.
 
TEC ndo kitu gani ktk nchi? Acha uzuzu.
Serikali ina vyombo vya DOLA vyote.
TEC haina vyombo vya DOLA., ni dini tu.
Je TEC ina polisi? Ina magereza? ina TISS? nk.
Serikali ikiamua kufanya ya kwake TEC itapotea kwenye ramani ya Tz ndani ya muda mfupi sana. Be ware. Usicheze na serikali.
Kojoa ukalale sasa!!
 
Baada ya DG Tiss kuondolewa au kubadilishwa ilifuata kulifumua na kulisuka upya baraza la mawaziri ikiwemo kutolewa cheo kipya cha naibu waziri mkuu ambacho hakiko kikatiba nilijua lengo kuu lilikuwa kuupoteza mjadala wa bandari.

Lakini naona ngoma bado iko palepale na waraka wa TEC unaendelea kusomwa kwenye makanisa yote.

Nadhani ni wakati sasa wa serikali kuachana na hili dubwana la DPW
Watanzania wengi bado ni wazalendo.

Unaweza kuwachezea watanzania wengi kwa mambo ambayo hayana athari kubwa kitaifa lakini sio kwenye mali za asili na adhimu kama bandari zote za nchi.

Hii ngoma bado ni pevu!
 
Back
Top Bottom