Na kakikundi ka watu wasiozidi watano wenye multiple ID za kutosha ndio wanasumbua
Ishu sio mtoa hoja bali ni hoja iliyoibuliwa kutokana na matamshi ya kibaguzi ya Mbowe
Ni Mwenyekt wetu wa Chadema, yes, ni nguli wa siasa lakn matamshi yake kusema eti Wachaga walikuwa hawaajiriwi ktk utawala wa Magufuli ni maneno ambayo sikutegemea yatoke ktk kinywa cha mtu kama Mbowe
Inamaana Chadema ni chama cha kutetea kabila la Wachaga?
Kwamba toka 2015 kazi kuu ya Mbowe ni kuhesabu wachaga wangapi wameajiriwa/kuteuliwa au kutenguliwa Serikalini!???
Hivi ni viashiria vya kuonesha kuwa kumbe ajenda ya SIRI ya Chadema ni kutetea maslahi ya kabila la Wachaga na ndio maana hata muanzilishi wa Chama Bw Edwin Mtei akaamua kumrithisha mkwe wake bw Mbowe uenyekiti
Kwamba zile tuhuma zilizokuwa zikizagaa miaka ile kwamba Chadema imejaa ukabila ni za kweli,, kupeana vyeo na nyadhifa hasa za ubunge viti maalum kindugu, kishemeji, na kikabila zilikuwa na ukweli
Sisi wengne wa makabila kama Wakinga, Wahaya, Wanyaturu, wanyakyusa, wadigo etc tulioamua kuiunga mkono Chadema je tutafute na sisi vyama vyetu vya siasa kufatilia watu wa makabila yetu wangapi wameajiriwa au kutenguliwa Serikalini!????
Tutafika kweli kwa mtindo huu?
Inasikitisha sana hii kauli ya Mbowe, sana sana
Na si ajabu hata wewe Mshana Jr unaitetea kauli hii kwakuwa Mbowe ni wa kabila/Jamii yako