1. Sayansi haijawahi kusema nadharia zake zimekamilika. Ukisikia mtu anakwambia nadharia ya sayansi imekamilika, ujue huyo hajui sayansi ni nini.
Mwanafalsafa nguli Kurt Godel aliandika "Godel's Incompleteness Theorems" zinazoelezea kwa undani kabisa suala hili.
Nakushauri uzisome na kuzielewa.
2. Kupinga uwepo wa Mungu ni kitu kimoja, nadharia za kisayansi ni kitu kingine. Mtu anaweza kupinga uwepo wa Mungu kwa kutumia mantiki na falsafa tu, bila kuhitaji nadharia yoyote kati ya hizi za kisayansi.
Kwa mfano, proof by contradiction, using the problem of evil, inaweza kupinga uwepo wa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote (kama wa Biblia na Quran) bila kuhitaji nadharia yoyote ya sayansi.
Ni sawa na kuweza kujua kwamba 10 si square root ya 2 bila kujua square root ya 2 ni nini.
Ni kama kujua binti mchanga mwenye umri wa miezi 6 leo hawezi kuwa mama mzazi wa mwanamme mwenye miaka 30 leo, bila hata kumjua mama mzazi wa huyo mwanamme mwenye miaka 30 ni nani.
Ni kama kujua the sum of two even numbers will always give you an even number, without knowing all numbers.
Kitu kikubwa kuelewa ni kwamba, hata katika sayansi, huhitajibsayansi ikamilike, au huhitaji hata kujua jibu sahihi la kisayansi, ili kujua kuwa jibu fulani si sahihi.
Kwa maneno mengine, hata kwenye sayansi, tunaweza kuwa hatujakamilisha jibu la ulimwengu umeanzaje, lakini tukajua kuwa jibu la Mungu yupo na ndiye aliyeumba ulimwengu tukajua si la kweli.
carnage21