Kuna pande kuu mbili,
Kuna wanaoamini uwepo wa Mungu na wale wasioamini uwepo wa Mungu.
Wasioamini uwepo wa Mungu wanasema, Kila kitu kinacho-exist,uwepo wake lazima uelezewe kisayansi. Swali, kisayansi Ulimwengu ulianzia wapi?
Kundi la pili ni la wale wanaoamini uwepo wa Mungu. Hawa Imani yao inasema si mambo yote yanaweza kuelezewa Kwa akili ya binadamu. Kwaiyo ukimuuliza muumini nini chanzo cha baadhi ya mambo, hawezi kukupa jibu kwasababu msingi wa Imani yake ni kuwa si kila kitu kinaweza kuelezewa na binadamu. Huo ndio Msingi.
Tunapowauliza kuhusu chanzo cha Ulimwengu, na vitu vingine inabidi mtuonyeshe kwasababu msingi wa imani yenu ni kuwa Kila kitu hutokea kisayansi.
Mkituuliza Mungu alianzia wapi, sie jibu letu ni fupi tu kuwa yeye Hana chanzo wala mwisho. Na mkisema hili linawezekana vipi, basi tutasema msingi wa tunachoamini ni kuwa Kuna baadhi ya mambo yana limit.
Nyinyi sasa ambao mnaamini kuwa Kila kitu kinatokea kisayansi mnalo jukumu la kuelezea kila kitu kinachoonekena bila kurukaruka.
Ulimwengu wa Mungu unazo Siri kubwa sana hazifahamiki Wala hazitokuja kufahamika kamwe,Sayansi Ina mfululu wa magunduzi na ndani ya mfululu huo tukiwa kama binadamu tunapata maswali mengi kuliko majibu na tunajikuta tuna staajabu uumbaji na uumbaji na uumbaji na uumbaji,,maana kama bing bang existed 13.5 Billions of years ago,,then came the existence discovery of Methuselah which existed 14.5 billion of years ago.
Sayansi Ina maajabu ambayo Mimi naona inatupa raha na msisimko wa ajabu, exploration ya hali ya juu sana.
Imani juu ya uwepo wa Mungu inatupa nguvu kuwa yupo anayejua zaidi yetu,Kuna master wetu,Kuna mamlaka juu yetu,ni ukweli kuwa tupo kwenye matrix ambayo hayuwezi ku escape na njia pekee ya ku flow nayo vyema ni kuwa tu na imani juu ya uwepo wa Mungu,kwa sababu hatuwezi kuthibitisha kisayansi kuwa Mungu yupo au hayupo.
Kuna wale wanaamini na kusadiki hizi hadithi au hakaya za sumerian ancient civilizations,,the stories about Anunnaki as being our masters,,as the human kind creators,but the same question always will rise as in science,how did the Anunnaki exist and who created them,jibu linakuja Tena kwenye Sayansi na theories za dark matter,that everything in the Galaxies started out of the dark matter whereby the light was first created from the dark.
Kwa kifupi Sayansi ifanye kazi yake kwa maendeleo na exploration za wanadamu kwa sababu tunahitaji pia adventures in this life as life is boring in nature so we need explorations and adventures and new challenges.
Tunahitaji Sayansi kutatua changamoto zetu za kifizikia,kibailojia,kikemikali,kijiografia,kiuchumi Kila sekta na nyanja zote za kimaisha zinahitaji Sayansi ili mradi siku ziende vyema.
Lakini ni ukweli usiopingika binadamu ni wanyama katika mfumo wa mtu, we are animals in human form,kwa hivyo baadhi yetu tunahitaji Imani juu ya uwepo wa Mungu ili tuweze kuendelea kuwa salama katika matrix tuliyopo tuishi kwa matumaini na imani,maana Imani ni kama nira ya kuleta utengamano bila Imani sisi ni mahayawani na kawaida ya mahayawani ni kulana,kuchinjana, mwenyewe na nguvu ndio ata survive.
Hayo ni mtazamo wangu tu.
Nayatazama yote ulimwengu kwa mkabala unakwenda namna hii.