Hakuna nadharia yoyote ya Kisayansi inayoelezea kikamilifu chanzo cha ulimwengu

Uli uliza swali kwamba, Ulimwengu upo kwa mujibu wa nini, nani au kivipi?

Ndio maana nasema, Si lazima kwamba ulimwengu upo kwa mujibu wa kitu fulani au kwa mujibu wa nani.

Ulimwengu upo tu, Na Haujawahi kutokuwepo.
Hata wewe hujui.

Unabashiri tu kama wengine.
 
Hata wewe hujui.

Unabashiri tu kama wengine.
Wote tuna bashiri.

Hakuna mwenye Uthibitisho

Hivyo mtu yeyote asije na theories zake zozote zile kisha aseme ndizo za chanzo cha ulimwengu.

Maana hata hicho chanzo cha ulimwengu, kitazua maswali kimewezaje kuwepo from nothing?
 
Jibu swali nililo kuuliza, kisha uulize maswali yako.

Kinachowagharimu wakana Mungu ni kuwa mnakimbia maswali, Sasa maana ya mjadala inakuwa haipo.

Kingine aya yako ya pili inaonyesha una kiwango kidogo sana Cha kuhoji na hauko makini. Unakubali "Infinity" ina exist ? Sababu swali lako kwenye aya ya pili ni la kipuuzi na ni la uongo.
Wewe hunaga hoja zozote tofauti na Quran..

Unataka hoja zenye mrengo wa Quran na Uislamu tu.
 
Hapo ni sawa na kuangalia kisogo chako bila kioo.
Yani wewe unaona sawa Mungu huyo kuwepo bila chanzo ila unaona si sawa dunia kuwepo bila chanzo.

Kama Mungu huyo ameweza kuwepo bila chanzo, Inashindikana vipi kwa Dunia?

Automatically, Unataka hoja za kumtetea Mungu wako aonekane yupo kumbe hayupo.
 
Wote tuna bashiri.

Hakuna mwenye Uthibitisho

Hivyo mtu yeyote asije na theories zake zozote zile kisha aseme ndizo za chanzo cha ulimwengu.

Maana hata hicho chanzo cha ulimwengu kitazua maswali kimewezaje kuwepo from nothing.
Watu waje na hizi theories zao ili zipate kuhojiwa.

Bila kuhoji hatuwezi kupata maendeleo yoyote yale kwenye nyanja yoyote ile.
 
Mbona jibu rahisi tu Chanzo Cha ulimwengu ni Mungu ila Kwa wanao amini Mungu nyinyi msioamini endeleeni kutafuta Chanzo
 
Yani wewe unaona sawa Mungu huyo kuwepo bila chanzo ila unaona si sawa dunia kuwepo bila chanzo.

Kama Mungu huyo ameweza kuwepo bila chanzo, Inashindikana vipi kwa Dunia?

Automatically, Unataka hoja za kumtetea Mungu wako aonekane yupo kumbe hayupo.
Tufanye hivii...wewe ndiye unayejua tena umeshinda.
Siku ukipata utulivu ukiwa peke yako pengine unaweza kupata neema ya ufahamu....ambayo kwa wengine ni upumbavu.
 
Watu waje na hizi theories zao ili zipate kuhojiwa.
Umesema kwamba wote tuna bashiri tu.

Hata theories zikiletwa kuhojiwa zitahojiwa kwenye ubashiri tu.

Hakuna kipimo sahihi cha kuthibitisha ukweli na uhakika wa theories.
Bila kuhoji hatuwezi kupata maendeleo yoyote yale kwenye nyanja yoyote ile.
Linapo kuja swala la Dunia imekuwepo vipi, Hakuna mwenye Uthibitisho na ukweli sahihi maana wote ni sehemu ya Dunia.

Ni sawa na wewe Nyani Ngabu ujihoji, Je wewe ni Nyani Ngabu?

Au mimi infropreneur nijihoji mwenyewe, Je mimi ni infropreneur?
 
Mbona jibu rahisi tu Chanzo Cha ulimwengu ni Mungu ila Kwa wanao amini Mungu nyinyi msioamini endeleeni kutafuta Chanzo
Na chanzo cha Mungu ni nini?

Mtasema, Mungu hana chanzo.

Kama mna amini Mungu hana chanzo, Inashindikana vipi kwa Dunia kutokuwa na chanzo?

Kwa nini una amini Mungu Hana chanzo, ila Unashindwa kuamini pia Dunia haina chanzo vilevile?
 
Umesema kwamba wote tuna bashiri tu.

Hata theories zikiletwa kuhojiwa zitahojiwa kwenye ubashiri tu.

Hakuna kipimo sahihi cha kuthibitisha ukweli na uhakika wa theories.

Linapo kuja swala la Dunia imekuwepo vipi, Hakuna mwenye Uthibitisho na ukweli sahihi maana wote ni sehemu ya Dunia.

Ni sawa na wewe Nyani Ngabu ujihoji, Je wewe ni Nyani Ngabu?

Au mimi infropreneur nijihoji mwenyewe, Je mimi ni infropreneur?
Naona unarudia yaleyale ambayo ushayaongelea.

Deuces ✌️.
 
Naku uliza hivi👇

Kama wote tuna bashiri, Theories hizo zikiletwa zitahojiwa kwa kipimo kipi chenye ukweli na usahihi?

Maana wote si tuna bashiri..
 
Tufanye hivii...wewe ndiye unayejua tena umeshinda.
Siku ukipata utulivu ukiwa peke yako pengine unaweza kupata neema ya ufahamu....ambayo kwa wengine ni upumbavu.
Hakuna anaye jua.

Hata ninyi kufanya conclusion ya kwamba Mungu ndiye chanzo cha kila kitu hamna uthibitisho wowote ule.

Ni ubashiri tu wa mawazo yenu.
 
Wewe hunaga hoja zozote tofauti na Quran..

Unataka hoja zenye mrengo wa Quran na Uislamu tu.
Wewe jibu unavyotaka wewe acha uoga. Jibu maswali niliyo kuuliza, maswali niliyo kuuliza hayahusiani na unachokisema.
 
Wewe nakufahamu kwenye nyuzi mbalimbali za maswala haya ya Mungu, umebase kwenye Quran tu.
 
Sasa katika vitu ambavyo unaviona Sayansi haijavitolea majibu na kusema Sayansi haina majibu, unafikiri kuna vyanzo vingine nje ja sayansi vilivyotoa majibu ya hivyo vitu kwa njia ya uthibitisho?
Tatizo kubwa hapa ni uelewa wa mambo na elimu ya vitu. Kwa sababu hii ndio maana tunaona kwamba sayansi na imani vinakinzana.

Kama tunaelewa vizuri mambo na elimu ya vitu, kwa vyovyote vile haiwezekani sayansi kupingana na imani; si juu ya imani yenyewe wala chochote kilichofunuliwa kwa njia ya imani.

Kama imani ni kuhusu kujua na kuwa na hakika na sayansi ni hivyohivyo.
 
Tafsiri ya kusema imani ni kujua kitu kwa hakika ni tafsiri potofu.

Imani ni kuamini kitu bila kuwa na uthibitisho
 
Back
Top Bottom