Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Fukua

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2022
Posts
546
Reaction score
479
Watanzania wenzangu, Ngorongoro ni lazima ilindwe kwa nguvu zote.

Japo Wamasai hawataki kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao kama maeneo mengine ambapo paliwahi kufanyika operation kama hii lakini ni lazima waondoke ili nia njema ya serikali ya kuilinda na kuhifadhi ngorongoro yafanikiwe.

Hatuwezi kuchekea kundi dogo la watanzania wenzetu kutuharibia rasilimali yetu, wametengewa maeneo mazuri kabisa kwa ajili ya shughuli zao, wamejengewa makazi na huduma Bora za kijamii Kama maji, shele na hospital zinapatikana lkn wanaigomea serikali kwa hoja za kipuuzi kabisa.

Pia Wamasai hawana ubavu wa kushindana na serikali wasidanganywe na hizi kelele za wapingaji ambao ni waoga, wanafiki na watakaa pembeni wamasai wabishi watakapoanza kushughulikiwa.

Kwa hili la Ngorongoro naiunga mkono serikali ya Mama Samia, kwamba kuongoza nchi sio kuchekeana chekeana.
 
Wadundwe.
Sheria ziko wazi kabisa, kuwa rasilimali na ardhini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya Jamhuri (serikali) na si vya bepari yeyote.
Kwa uhai wa uchumi wetu ngorongoro lazma ipewe wawekezaji watakao zidusha idadi ya watalii nchini, ili huduma za kijamii shule hosipitali nk vipatikane kwa raia, hao wa masai laki mbili hawawezi kuiingizia serikali kipato hata 1% ya muwekezaji atakae pewa hilo eneo
 
Wadundwe.
Sheria ziko wazi kabisa, kuwa rasilimali na ardhini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mali ya Jamhuri (serikali) na si vya bepari yeyote.
Wamesababisha mlinzi wetu mmoja kufa,
 
Kwa uhai wa uchumi wetu ngorongoro lazma ipewe wawekezaji watakao zidusha idadi ya watalii nchini, ili huduma za kijamii shule hosipitali nk vipatikane kwa raia, hao wa masai laki mbili hawawezi kuiingizia serikali kipato hata 1% ya muwekezaji atakae pewa hilo eneo
Umesema vyema kabisa na mwekezaji tayari yupo Hawa wamasai wanataka kukwamisha juhudi za serikali
 
Wamasai wako zaidi ya laki 2 huko Ngorongoro sasa hizo nyumba walizojengewa Handeni ni ngapi?
Acheni propaganda!
Nyumba zaidi ya 100 zimekamilika na ujenzi unaendelea
 
Baba yake Sabaya aliwahi kuwa DC wakati wa Hayati Mzee Mkapa …hakubembeleza bembeleza kama kina Samia mara sijui kujengea nyumba sijui makazi bora, yeye aliamka asubuhi na kutia kiberiti nyumba zote zilikuwa Serengeti wakati huo
 
Baba yake Sabaya aliwahi kuwa DC wakati wa Hayati Mzee Mkapa …hakubembeleza bembeleza kama kina Samia mara sijui kujengea nyumba sijui makazi bora …yeye aliamka asubuhi na kutia kiberiti nyumba zote zilikuwa Serengeti wakati huo
Hata leo habembelezwi mtu, watahama tu serikali ikamilishe adhima yake njema
 
Umesema vyema kabisa na mwekezaji tayari yupo Hawa wamasai wanataka kukwamisha juhudi za serikali
Mlioingia ili kuhadaa watanzania. Muwapige tu ili ijulikane, waarabu ni watesi sana. Wanakuja kuwekeza nini huko? Au mnawagawia hifadhi ili wale cha juu na nyie mle cha juu? Royal tour si ndo inaleta watalii sa mnaweka mwekezaji alete nini?
 
Hata leo habembelezwi mtu, watahama tu serikali ikamilishe adhima yake njema
Adhima yake njema wapi? Mnawaonea wakazi wa watu sana nyie wazanzibar huku kwenu huko mko shwari.
 
Mlioingia ili kuhadaa watanzania. Muwapige tu ili ijulikane, waarabu ni watesi sana. Wanakuja kuwekeza nini huko? Au mnawagawia hifadhi ili wale cha juu na nyie mle cha juu? Royal tour si ndo inaleta watalii sa mnaweka mwekezaji alete nini?
Hapana ndugu tunataka kuwekeza na pia kuihifadhi na kuilinda ngorongoro hii NI rasilimali ya umma
 
Hapana ndugu tunataka kuwekeza na pia kuihifadhi na kuilinda ngorongoro hii NI rasilimali ya umma
Kila sehemu ni rasilimali ya umma. Unawekeza nini hasa huko ngorongoro? Kwani hao wamasai walipavamia au ni wakazi wa kudumu huko?
 
Adhima yake njema wapi? Mnawaonea wakazi wa watu sana nyie wazanzibar huku kwenu huko mko shwari.
Tunafanya hivi mkuu kwa maslahi ya umma wa watanzania na vizazi vyetu vijavyo tukiacha kufanya hivyo ngorongoro haitakuwepo Tena miaka michache mbele
 
Back
Top Bottom