Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Memba mpya au wa zamani si hoja iliyopo mezani mkuu, wamasai NI vyema mkaondoka kwa hiari
Hatuondoki bila kumwaga damu dunia ijue kuwa mwarabu ni bora apewe ardhi ya tanzania kwa kuua wazawa.
 
Mlioingia ili kuhadaa watanzania. Muwapige tu ili ijulikane, waarabu ni watesi sana. Wanakuja kuwekeza nini huko? Au mnawagawia hifadhi ili wale cha juu na nyie mle cha juu? Royal tour si ndo inaleta watalii sa mnaweka mwekezaji alete nini?
Huyo ni kiazi
 
Hakuna hila kwenye Jambo hili mkuu serikali Ina Nia njema kabisa
Mbona kuna allegations nyingi kuhusu kumilikishwa mwarabu na serikali haitoi ufaganuzi wowote. Watu wate wanasema Grumet Grumet, imekuwa Grumet ya mwaarabu .hakuna mtu wankuissuport mpaka iweke clear doubts zinazosambaa.
 
KiLa kaya Moja imepewa nyumba serekali haiwezi kutoa nyumba mpaka kwa watoto
Natural habitat za wamasai ni za kipekee serikali inawapelekea usasa wakati wenyewe wanajenga boma zao burudani kama sisimizi sasa research haikufanywa kuona wanaishije au ?kufikiri kwa mwafrika kuna taabu sana
 
Nyumba zaidi ya 100 zimekamilika na ujenzi unaendelea

Nyumba mia? Na hao 190,000 mtawabwaga maporini na kuwaambia mtajiju.
Yaani kama vile Makaburu enzi hizo walikuwa wanawahamisha Wabantu kwa nguvu na kuwabwaga katika maeneo waliyowatengea waliyoyaita Bantustan?
Hakuna serikali duniani iliyofanikisha malengo yake kwa propaganda na vitisho.
 
Watanzania wenzangu, ngorongoro NI lazima ilindwe kwa nguvu zote.

Japo wamasai hawataki kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao Kama maeneo mengine ambapo paliwahi kufanyika operation Kama hii lkn ni lazima waondoke ili Nia njema ya serikali ya kuilinda na kuhifadhi ngorongoro yafanikiwe.

Hatuwezi kuchekea kundi dogo la watanzania wenzetu kutuharibia rasilimali yetu, wametengewa maeneo mazuri kabisa kwa ajili ya shughuli zao, wamejengewa makazi na huduma Bora za kijamii Kama maji, shele na hospital zinapatikana lkn wanaigomea serikali kwa hoja za kipuuzi kabisa.

Pia Wamasai hawana ubavu wa kushindana na serikali wasidanganywe na hizi kelele za wapingaji ambao ni waoga, wanafiki na watakaa pembeni wamasai wabishi watakapoanza kushughulikiwa.

Kwa hili la Ngorongoro naiunga mkono serikali ya Mama Samia, kwamba kuongoza nchi sio kuchekeana chekeana.
WAELIMOSHWE WATOLEWE ILE NI HAZINA YETU NI URITHI WETU
 
Baba yake Sabaya aliwahi kuwa DC wakati wa Hayati Mzee Mkapa …hakubembeleza bembeleza kama kina Samia mara sijui kujengea nyumba sijui makazi bora, yeye aliamka asubuhi na kutia kiberiti nyumba zote zilikuwa Serengeti wakati huo
Sabaya amerithi ukatili kutoka kwa baba yake pumbav kabisa
 
Mlioingia ili kuhadaa watanzania. Muwapige tu ili ijulikane, waarabu ni watesi sana. Wanakuja kuwekeza nini huko? Au mnawagawia hifadhi ili wale cha juu na nyie mle cha juu? Royal tour si ndo inaleta watalii sa mnaweka mwekezaji alete nini?
Watu wameshakula Cha juu kilichobaki ni kazi ya kuwahamisha wamasai kwenye ardhi yao hata kwa mtutu wa bunduki
 
Tunafanya hivi mkuu kwa maslahi ya umma wa watanzania na vizazi vyetu vijavyo tukiacha kufanya hivyo ngorongoro haitakuwepo Tena miaka michache mbele
Kwani ngorongoro imekuwepo kwa miaka mingapi sasa
 
Kwa maoni yako ya uhifadhi, je unatambua kuwa ufugaji sehemu za hifadhi ni moja ya njia za kuzihifadhi pia? Haikatai.

Kila sehemu ni rasilimali ya umma. Unawekeza nini hasa huko ngorongoro? Kwani hao wamasai walipavamia au ni wakazi wa kudumu huko?
Hakuna kitu inaitwa makazi ya kudumu ya Kabila fulani hapa nchini, Serikali ina mandate ya kubadilisha matumizi ya ardhi yake wakati wowote inaona inafaa. Ilitokea kwa wakazi wa Kakola (Kahama) enzi hizo ilipokuwa inaingia Barrick kuchimba dhahabu. Wenyeji walihamishwa. Kuna ugumu gani kwa wamasai?
Hata ikitokea Wachaga wanaingilia hifadhi ya mlima Kilimanjaro watahamishwa mara moja.
 
Hatuondoki bila kumwaga damu dunia ijue kuwa mwarabu ni bora apewe ardhi ya tanzania kwa kuua wazawa.
Ubishi wenu utawagharim Sana ardhi NI Mali ya umma na serikali ndio yenye dhamana ya kuratibu matumiz ya ardhi kwa manufaa ya umma, ngorongoro ikiachwa iendelee kuharibiwa kama Sasa basi tutaipoteza Kama mna hamu ya kumwaga damu kwa manufaa ya umma sawa
 
Nyumba mia? Na hao 190,000 mtawabwaga maporini na kuwaambia mtajiju.
Yaani kama vile Makaburu enzi hizo walikuwa wanawahamisha Wabantu kwa nguvu na kuwabwaga katika maeneo waliyowatengea waliyoyaita Bantustan?
Hakuna serikali duniani iliyofanikisha malengo yake kwa propaganda na vitisho.
Ujenzi bado unaendelea na serikali imejipanga vizur katika hili mkuu
 
WAELIMOSHWE WATOLEWE ILE NI HAZINA YETU NI URITHI WETU
Tunaendelea kuwaelimisha mpaka waelewe hawana hati miliki ya ngorongoro serikali ndio yenye mamlaka ya kubadili matumiz ya ardhi na kulinda rasilimali zetu Sasa Hawa wamasai wataka kukwamisha juhudi za serikali na mipango mizuri
 
Hakuna kitu inaitwa makazi ya kudumu ya Kabila fulani hapa nchini, Serikali ina mandate ya kubadilisha matumizi ya ardhi yake wakati wowote inaona inafaa. Ilitokea kwa wakazi wa Kakola (Kahama) enzi hizo ilipokuwa inaingia Barrick kuchimba dhahabu. Wenyeji walihamishwa. Kuna ugumu gani kwa wamasai?
Hata ikitokea Wachaga wanaingilia hifadhi ya mlima Kilimanjaro watahamishwa mara moja.
Hatuondoki....hayo mapato mliyo nayo kwasasa mmeshindwa kupangilia ya kututoa ndo mtafikia malengo??? Vipi mapato ya kwenye simu billions of mahela...mmefanyia nn mana shule mpya tunaona ni hisani ya covid!!!!
 
Kwa maoni yako ya uhifadhi, je unatambua kuwa ufugaji sehemu za hifadhi ni moja ya njia za kuzihifadhi pia? Haikatai.

Sio ufugaji wa kujaza mifugo mingi katika eneo dogo
 
Back
Top Bottom