Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Hakuna namna, Wamasai lazima wakubali kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao

Tunaendelea kuwaelimisha mpaka waelewe hawana hati miliki ya ngorongoro serikali ndio yenye mamlaka ya kubadili matumiz ya ardhi na kulinda rasilimali zetu Sasa Hawa wamasai wataka kukwamisha juhudi za serikali na mipango mizuri
Mipango mizuri ipi??? Elimu ipi unatoa ww?? Unaonekana mchumia tumbo tu wewe....
 
Walitaka kuibadilisha hati kutoka Hifadhi mpaka kuwa makazi ya watu
Wamasai wale wa zamani sawa ila sasa wamekuja watu kuwekeza Ng’ombe kwao na kujenga nyumba za kudumu

Hilo hata mimi napinga kadri wanavyoongezeka ndivyo wadudu, ndege, na hata baadhi ya wanyama wanapotea kabisa katika ardhi hiyo

Wengi wasiopenda natures watapinga vikali
 
Sio ufugaji wa kujaza mifugo mingi katika eneo dogo
Elimu ni pamoja na kukubali kujifunza upya ulichofundishwa mwanzo......

Zile pointi za overstocking na overgrazing zinafeli ikiwa hawa watu watakuwa wanazungukazunguka pori zima.

Kwa hiyo formula ya kutengeneza jangwa inabadili ka na kuwa; ukitaka kupata jangwa wachukue wafugaji, waweke kwenye kieneo kidogo walazimishe wasitoke hapo wachungie hapohapo tena na tena utapata jangwa.

Na ukitaka kuhifadhi msitu waruhusu wachungaji wautawale msitu mzima wasikae sehemu moja tu!!
 
Tunaendelea kuwaelimisha mpaka waelewe hawana hati miliki ya ngorongoro serikali ndio yenye mamlaka ya kubadili matumiz ya ardhi na kulinda rasilimali zetu Sasa Hawa wamasai wataka kukwamisha juhudi za serikali na mipango mizuri
Ni kweli na wao wanaishi katika umaskini uliokithiri pale mbugani.Hakuna zahanati wala shule na wao hawaruhuhusiwi kujenga chochote
 
Walitaka kuibadilisha hati kutoka Hifadhi mpaka kuwa makazi ya watu
Wamasai wale wa zamani sawa ila sasa wamekuja watu kuwekeza Ng’ombe kwao na kujenga nyumba za kudumu

Hilo hata mimi napinga kadri wanavyoongezeka ndivyo wadudu, ndege, na hata baadhi ya wanyama wanapotea kabisa katika ardhi hiyo

Wengi wasiopenda natures watapinga vikali
Mimi nakuunga mkono
 
Watanzania wenzangu, ngorongoro NI lazima ilindwe kwa nguvu zote.

Japo wamasai hawataki kuondoka Ngorongoro kwa hiari yao Kama maeneo mengine ambapo paliwahi kufanyika operation Kama hii lkn ni lazima waondoke ili Nia njema ya serikali ya kuilinda na kuhifadhi ngorongoro yafanikiwe.

Hatuwezi kuchekea kundi dogo la watanzania wenzetu kutuharibia rasilimali yetu, wametengewa maeneo mazuri kabisa kwa ajili ya shughuli zao, wamejengewa makazi na huduma Bora za kijamii Kama maji, shele na hospital zinapatikana lkn wanaigomea serikali kwa hoja za kipuuzi kabisa.

Pia Wamasai hawana ubavu wa kushindana na serikali wasidanganywe na hizi kelele za wapingaji ambao ni waoga, wanafiki na watakaa pembeni wamasai wabishi watakapoanza kushughulikiwa.

Kwa hili la Ngorongoro naiunga mkono serikali ya Mama Samia, kwamba kuongoza nchi sio kuchekeana chekeana.
Una uhakika huko wanakohamishiwa kimabavu na serikali kuna hizo huduma unazosema? Au unakubali kila unachoambiwa? Waziri mkuu anasema Ngorongoro hakina machafuko, kisha mkuu mkoa anajitokeza kusema polisi kauwawa?! Ukiamini waongo wa hivyo utakuwa na akili nzito sana.

Ni hivi hao Wamasai wakikubali kuondoka huko ngorongoro kwa mabavu wataenda kuteseka ile mbaya huko handeni.
 
Kutukanana hakuleti tija , tujitahidi kujibiana kwa hoja
Anafikiri kutukanana ndio wamasai hawataondoka ngorongoro tumedhamiria kwa dhati kuilinda na kuhifadhi ngorongoro kwa manufaa ya umma
 
Ni kweli na wao wanaishi katika umaskini uliokithiri pale mbugani.Hakuna zahanati wala shule na wao hawaruhuhusiwi kujenga chochote
Haliwezekani watanzania wenzenu waitwao Masai waendelee kuishi Kama wanyama, tunataka wawe na huduma Bora za kijamii Kama maji shule afya n.k
 
Mipango mizuri ipi??? Elimu ipi unatoa ww?? Unaonekana mchumia tumbo tu wewe....
Wale ni binadamu Tena watanzania haliwezekani Karne hi waendelee kuishi Kama wanyama tunataka wawe na ustaarabu ili tuende pamoja Kama nchi
 
Walitaka kuibadilisha hati kutoka Hifadhi mpaka kuwa makazi ya watu
Wamasai wale wa zamani sawa ila sasa wamekuja watu kuwekeza Ng’ombe kwao na kujenga nyumba za kudumu

Hilo hata mimi napinga kadri wanavyoongezeka ndivyo wadudu, ndege, na hata baadhi ya wanyama wanapotea kabisa katika ardhi hiyo

Wengi wasiopenda natures watapinga vikali
Nakubaliana na wewe asilmia [emoji817]
 
Una uhakika huko wanakohamishiwa kimabavu na serikali kuna hizo huduma unazosema? Au unakubali kila unachoambiwa? Waziri mkuu anasema Ngorongoro hakina machafuko, kisha mkuu mkoa anajitokeza kusema polisi kauwawa?! Ukiamini waongo wa hivyo utakuwa na akili nzito sana.

Ni hivi hao Wamasai wakikubali kuondoka huko ngorongoro kwa mabavu wataenda kuteseka ile mbaya huko handeni.
Wajidanganye kunyanyua miguu kutoka Masai land kwenda handen ndio wataisoma namba vizur
 
Wanafukuzwa wazawa wanapewa waarabu afu kunatokea mapopoma yanashabikia upumbavu
 
Tunafanya hivi mkuu kwa maslahi ya umma wa watanzania na vizazi vyetu vijavyo tukiacha kufanya hivyo ngorongoro haitakuwepo Tena miaka michache mbele

Umma upi huo?

Maslahi gani hayo mepesi mepesi hivyo kudai 'yalindwe kwa nguvu zote'?

Kudai kwamba Ngorongoro haitakuwepo ni hadaa kubwa kuliko aliyodai Mh. Waziri mkuu, Bungeni!
Nikusii, ukome kutumia "Watanzania" hivyo uitumiavyo kijumla jumla kana kwamba ndio Waliokutuma hapa.
 
Hata leo habembelezwi mtu, watahama tu serikali ikamilishe adhima yake njema
Hiyo "Serikali" yako haina, narudia, HAINA adhma njema. Hakuna.
...na kwa Taarifa yako, hakuna Serikali isiyokuwa na Kikomo.

Mjipange na mengine lakini siyo ya kujitweka Ardhi bila kufuata sheria, bila kufuata Katiba.

Itafika nako, sehemu, hiyo "Serikali" yako unayodai nayo haita bembelezwa.

Wacheni kuhalalisha Uangamizaji wa Jamii.
 
Back
Top Bottom