Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,428
- 3,937
Habari zenu marafiki na maadui zangu,
Cheo cha Urais Tanzania siku zote kimekuwa ni cheo cha 'Rais Mtendaji' na siyo 'Ceremonial President' (msaada wa tafsiri ya Kiswahili).
Hata Marais kama Kikwete na Mwinyi ambao kidogo walichukua mlengo wa kuacha mambo yajiendeshe tofauti na Marais wengine tuliowahi kuwa nao, bado walibaki ni viongozi watendaji.
Inawezekana vyombo vyetu vya kimfumo vimekuwa vinajaribu kutumia mifumo hii miwili kwa njia ya kubadilishana ili labda kutotuchosha na aina moja ya uongozi maana "trend" inaonyesha kila baada ya Rais Mtendaji tumekuwa tunapata Rais ambaye kidogo anatumia "hands off" approach. Tukikumbuka pia taasisi hizi zimegoma kabisa mfumo wa kidemokrasia kufanya kazi nchini.
Baada ya kutoka kwenye mazishi ya Queen Elizabeth huku London, Rais Samia alielekea Msumbiji kwa ziara ya siku nne, na mpaka sasa yupo huko. Sioni umuhimu wowote wa Rais kukaa Msumbiji siku zote hizo. Tukumbuke, Rais amapokwenda sehemu, tayari majadiliano muhimu yanakuwa yameshafanyika na watendaji wa chini, Rais anakwenda tu kusaini mikataba. Vinginevyo, ni ile hali ya kuongeza tu ushirikiano kati ya nchi husika, ambapo ndiyo utaona anasaidia uzinduzi wa mradi fulani huko. Nje ya hapo, labda kuwepo na mkutano mkubwa unafanyika ambapo atahudhuria.
Sasa kama taasisi za kimfumo zimeamua Rais Samia ni ceremonial president na siyo Rais Mtendaji, maana style yake ya uongozi inaonyesha yuko hivyo, atakuwa anafanya nini siku zote nne hizo huko?
Siku nne ni nyingi saaana aisee. Itapendeza kama tukipewa mrejesho wa ratiba yake ilivyokuwa ili kama waajiri wake tujiridhishe na utumiaji wake wa muda.