Hakuna sababu yoyote ya Lissu kuendelea kuteseka gerezani

Hakuna sababu yoyote ya Lissu kuendelea kuteseka gerezani

Na watamfunga jela. Huu uchaguzi unapita Lissu yuko ndani, amekuwa tishio mno kwao. They can't handle the heat, mtaniambia.
 
Pamoja na kwamba sikubaliani na Lissu kifalsafa ya maisha lakini sipendezwi kabisa na uwepo wake gerezani.

Lissu ni msomi mkubwa.

Alumni wa UDSM.

Ni moja Kati ya think tankers na hazina ya taifa hili la Tanzania.

Gerezani sio sehemu anayopaswa kulala..

Nimezaliwa mwaka 85 nimeanza primary miaka ya tisini. Enzi hizo tuliamini kwamba watu wanao paswa kwenda gerezani ni vibaka na watu kama hao na sio wasomi kama Lissu.

Wakati Lissu anapata admission ya kwenda UDSM sidhani kama wazazi wake waliwahi kuwaza kwamba siku moja anaweza kukaa gerezani.

Kipanga wa darasani kama Lissu.Alumni wa Ilboru then UDSM aende gerezani? Kweli? Usingeweza kutabiri jambo kama hilo kwa mtu kama Lissu.

Imagination is the most best gift that was given to human beings by God the creator cause with the power of imagination you can own what you don't have.

Kwa hili la kutumia nguvu ya imagination ninajaribu kuescape the reality through imagination kwa kuimagine kwamba, Lissu halali gerezani. Analala hotelini. Samia hawezi kukubali mtu kama Lissu alale gerezani. ( Anyways its just imagination).


Nimesema sikubaliani na Lissu kifalsafa na sio kiitikadi.

Mimi naamini maisha ni ujinga ujinga na kwamba tupo duniani kwa ajili ya kustarehe na kuzaliana ili kuijaza dunia ( MWANZO 1:28) .

Tukisha ijaza dunia, Yule alie tuleta duniani ndio atajua afanye nini kwa sababu kiukweli hakuna ajuae sababu halisi kwanini tupo duniani isipokuwa alie tuumba. Anacho taka yeye ni dunia ijae period.

Lissu yeye anaamini maisha ni jambo moja serious Sana ndio maana anatumia nguvu na muda wake mwingi kufanya harakati.

Kwa mvua hii inayo nyesha jijini Dar es salaam, Lissu kukaa ndani sio sahihi. Mawakili wa Chadema fanyeni mnavyo weza Lissu apate dhamana arudi uraiani.

Apambane na kesi yake akiwa uraiani. Gerezani sio powa.

Najua mtasema kesi ya uhaini haina dhamana Ila hiyo haimzuii Lissu kupewa dhamana.

Mimi sio lawyer Ila najua to every general rule there is an exception.

Mnaweza kufanya lobbying mashtaka yakabadilishwa yakawa ya uchochezi then akapewa dhamana hata kama atapewa masharti ya kutojihusisha na hiyo movement yake hakuna shida. Kikubwa Lissu arudi uraiani.

Yote yanayo fanyika chini ya jua ni ujinga ujinga tu wala hayana maana yoyote.

Hakuna sababu yoyote Lissu kuendelea kuteseka gerezani.

Nimeona video ya Lissu akitembea kwa kuchechemea nimejisikia vibaya Sana.


Kingine ; Lissu ana nyota Kali Sana ya kukubalika kwa watu. Iwe mitandaoni iwe mitaani misikitini kwa makanisani. Kupitia upendo mkubwa unao onyeshwa na watanzania kwa Lissu kuna kitu ambacho universe inajaribu Ku communicate na watanzania kuhusu Lissu.
Kwamba hukubaliani na Tundu Lissu kifalsafa kwa sababu falsafa yake ni kuamini kuwa maisha ni kitu very serious sana wakati wewe unaamini kuwa maisha ni kula na kunywa na kustarehe halafu unasubiri Mungu atafanya nini juu yako baadae...

You're very wrong. Na kumbe ni halali mtofautiane naye, because you have nothing to offer...

By the way, najiuliza hicho utakacho kula, kunywa na ku - finance starehe zako kitatoka wapi kama sio kufanya kazi...?

Na unajua utafanya kazi ktk mazingira gani ili ikupatie cha kunywa, kula na kukustarehesha..?

Isingekuwa harakati za kina Julius K. Nyerere, Bibi Titi Mohammed, Oscar Kambona miaka ya 1950s na 1960s kupigania Uhuru, wala usingekuwa hapo ulipo...!

Tanzania inahitaji Uhuru wa pili toka kwa mkoloni mweusi. Bila harakati za kina Tundu Lissu hatuwezi kuupata Uhuru huo...

Yesu Kristo asingekuwa mwanaharakati wa kupigania Uhuru na HAKI katika ulimwengu huu, hakika mpaka Leo tungekuwa captives wa shetani na mawakala wake...

Harakati za ukombozi na kupigania haki, wakati fulani hugharimu kupita ktk njia ya mateso na ikibidi hata kufa. Yesu Kristo alilazimika kufa ili mimi na wewe tupate Uhuru na ukombozi kamili wa mwili na roho....

Ushauri wako wa Tundu Lissu ku - compromise na shetani, haukubaliki. Nami nakukumea kusema, SHETANI RUDI NYUMA YETU, KWA JINA LA YESU KRISTO ALIYE HAI....!!

Haki haiwezi ku - compromise na dhuluma. The fight has to go on until the end. Tundu Lissu said this himself; "....I was born to do this - fighting for people's rights & Freedom..."

Suppose kama Yesu Kristo angekubali ku - compromise na shetani, hivi mimi na wewe tungekuwa wapi Leo...?

Ushauri wako is purely devilish. Take it to yourself...!
 
Na watamfunga jela. Huu uchaguzi unapita Lissu yuko ndani, amekuwa tishio mno kwao. They can't handle the heat, mtaniambia.
Hafungwi mtu jela, trust me...!!

Hakuna uchaguzi mkuu mwaka huu, 2025...!

Kumbuka: Bunge halijavunjwa, limeahirishwa hadi 3/8/2025...

Unaelewa maana yake..?

#NoReformsNoElection..
 
Back
Top Bottom