Tulifikishwa pale tulipofika kutokana style ya uongozi uliopita. Awamu ya 4 ilifanya hayo yote anayofanya mama lakini tulipata nn? Hii nchi utadhani ina laana.Nikuhakikishie kuwa hamtaweza kumzuia mama kufanya kazi ngumu ya kulinyoosha taifa na kurudisha umoja ndani ya nchi mlio iharibu.
Kitendo cha kurudisha uhusiano wetu na majirani zetu kimewaumiza maana mnajua kuwa sasa mama anaanza kufagia maovu yaliyofanywa na mtangulizi wake.
Revisit your source of information.Hakuna nchi inayoongoza kwa kujifanya iko chini kama Marekani. Sasa hivi ukiwasoma wamarekani mara zote wanaonesha kama nchi yako inaenda kupitwa na China au inazidiwa na China kwa baadhi ya mambo.
Hata vidole vya mikono yako havilinganiTulifikishwa pale tulipofika kutokana style ya uongozi uliopita. Awamu ya 4 ilifanya hayo yote anayofanya mama lakini tulipata nn? Hii nchi utadhani ina laana.
Sent from my SM-A730F using JamiiForums mobile app
Reserved for future referencesJikwae sisi tunasonga
umeandika vema nadhani kuna cha kujifunza hapo, kazi iendeleee.Tanzania ndo Taifa pekee hasa kwa miaka ya sasa ambapo kuanzia viongozi wake na wananchi ujidharau na kusifia mataifa mengine kwa kujipendekeza.
Wakati wa Baba wa Taifa haya mambo hayakuwepo. Hatukubembeleza mtu au Taifa. Hata Jomo Kenyatta enzi hizo alionja shubiri za Nyerere. Si mara ya kwanza Tanzania kuwa na vita ya maneno na ya kiuchumi na Kenya.
Rais Kamuzu Banda pia aliwahi onja joto ya jiwe. Nakumbuka mashuleni hadi tuliimba. "Banda wa malawi katuvalia ngozi simba, kututishia watanzania hatujali...hatujalii. Watanzania tulisimama wamoja. Banda kwa mkwara tu akafyata mkia. Lakini bado Tanzania tulibaki imara (Kwa sauti ya Msechu)
Viwanda viliendelea, tulisoma bure kuanzia chekechea au vidudu hadi chuo kikuu. Tulisafirishwa bure kwa wale wa boarding. Tulipewa daftari na kalamu shuleni. Kulikuwa pia na magari ya shule. Maduka ya serikali na mabasi ya serikali kila mkoa. Kulikuwa na viwanda mikoa mingi. Mabus ya wafanyakazi. Kulikuwa na bustani au park zilitunzwa vizuri. Watu tulienda kupumzika mandhari nzuri na familia. Miji ilipangiliwa. Barabara nyingi zilikuwa na miti pembeni. Leo hakuna kitu. Sijui vilienda wapi.
Pamoja na kiburi chetu hakuna kubembeleza. Tulifunga balozi hadi za uingereza na kukataa misaada yao. Ujerumani Mashariki nao tukawagomea. Israel na wengineo lkn bado Tanzania tulieshimika duniani.
Leo tumekuja na siasa za kubembeleza. Kujipendekeza, kusifia wengine. Leo Watanzania tunaona Wakenya kama ndo wakombozi wa uchumi wetu. Miungu wetu. Leo tunawapa rukhsa waingie mbungani kwetu. Wawe huru. Wawekeze kila sehemu. Ni vizuri. Lakini tunaijua vema Kenya? Nani alivunja umoja wa Afrika mashariki? Nani alidhurumu mali za umoja huo? Nani alitumiwa na majasusi kuvunja huo umoja?
Eti leo economic democracy yetu ni kujiona sisi wajinga ila mataifa mengine ni wajanja. Kazi yetu ni ziara za kusaini mikataba tunayopewa kusaini. Hata hatuna muda wakufikiria. Kisa hatutaki hudhi mtu.
Naomba ziara zingine watanzania tuwe tuna taarifiwa kabla ili tujue nini kinaenda fanyika na pia kama ni mikataba ijadiliwe kwanza bungeni na watanzania tuelewe.
Mtamsema sana vibaya Mwl. Nyerere lakini hatabaki kuwa mdiplomasia wa hali ya juu. Alikuwa mbabe lkn bado aliheshimika na mataifa makubwa.
Mtamsema vibaya na kumtukana Magufuli lkn nchi nyingi zilimtambua kuwa alisimama kwa masilahi mapana ya Tanzania. Hata Mkapa hakuwa na siasa za kubembeleza mataifa ya nje.
Angalia marekani, Uchina, Uingereza, Ujerumani na mataifa mengine wapi wanasera za kubembeleza na kusifia mataifa mengine. USA ilifikia sehemu kuweka vikwazo katika biashara na nchina japo USA inamtegemea China kwa biashara. Kikubwa ni kuangalia maslahi mapana ya nchi.
Eti leo tunasifia wakenya wanademokrasia zaidi ya Tanzania. Ni vizuri. Watanzania wanabaki kujidharau. Wanajiona wao si kitu. Kweli katika kukua tunaona mengi. Kujipendejeza sio kusifiwa ni kuzidi kudharaulika tu. Magufuli alikuwa mkorofi na mbabe. Lakini Tanzania iliheshimika. Hakuongea kiingereza lkn hotuba zake zilifatiliwa dunia nzima kusikia nini atasema. UN wenyewe walikubali kuwa alikuwa mtu aliependa Taifa lake na Afrika.
Korea kaskazini aijipendekezi lkn Marekani wanaogopa na kuheshimu Korea kaskazini. Duniani hapa mataifa makubwa yenye nguvu yote yalitumia ubabe.
Hata ukoloni ulifanyika kwa ubabe ili watawala wapate watakacho. Hata katika Biblia watawala hakuna alie kuwa lele mama. Hakuna alie jipendekeza na kusifia wengine.
Haya twendelee na kusifia, kubembeleza na kujipendekeza tuone hayo maendeleo. Hii awamu ya (-6<+4) imenikumbusha mbali hesabu za mlinganyo na magazijuto.
Hongera Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Nakupenda ila kuwa makini na washauri wako. Hasa huyo ambae wakati wake nchi ilimshinda. Hata alipoulizwa kwanini Tanzania ni masikini wakati ina kila kitu. Alijibu hata yeye hajui na anashangaa kwanini Tanzania ni masikini. Ulikiri mwenyewe hotuba yako ya Bungeni kuwa anakushauri sana pamoja na yule bwana aliesema ataendeleza majengo alojenga babake lakini hakashindwa akabakiza majungu tu kule kwetu minazini.
Baba yake alikuwa na aakili kubwa. Ange kuwepo kule minazini kungekuwa dubai ndogo. Tusisingizie Muungano. Tunapotezwa tu. Yule baharia aliijenga nchi yetu ya minazini wakati huo huo wa muungano. Hata Dar wakati huo haikujengwa kama baharia alivyo ijenga minazini. Leo tunabaki lalamikia muungano badala ya kujikita kuijenga nchi yetu.
Yangu macho. Twendelee kujipendekeza. Kusifia na kuona sisi hatuwezi jenga uchumi wetu isipokuwa wawekezaji. China ilikuwa sawa na Tanzania miaka ya nyuma. Leo ni Taifa kubwa. Je, walitumia sera ya kujipendekeza na kusifia wengine na kujidharau?
Wachina walifanya kazi hawakutegemea wawekezaji uchwara kama Kenya. Walisomesha vijana wao nje, wakaiba tekinolojia toka mataifa makubwa. Wakaunda tekinolojia yeo. Rushwa ikapigwa vita ni kunyongwa tu. Taifa likasimama.
Watanzani leo hatuna scholarship kwa ajili ya Watanzania pekee kama yalivyo mataifa mengine. Mfano Afrika Kusini, Nigeria, Ethiopia na mengineyo hasa kwenda kusoma nje. Nashangaa balozi zetu hazina ubunifu.
Viongozi wengi tulionao leo walipelekwa kusoma nje na serikali. Leo wamekuwa wabinafsi.
Tanzania tu vijana wanaakili kwenye ubunifu na sayansi. Tuwatumie hawa. Tuwajari. Nchi imebaki majungu. Nchi imekuwa siasa kila kitu. Tunajenga shortcut ya maisha.
Viongozi tuwe na maono. Maendeleo hayaji kwa kujipendekeza. Watu watapata machungu ya maisha ila baadae wataenjoy. Nchi zote upitia huko. Ndo tutaona maendeleo ya kweli.
Karibu tena Ikulu kwa remote control. Nawe waziri wa mambo ya nje ulikuwa katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya nje wakati wa team Msoga. Uliishia kutuletea Bush, Obama na hatukuona tija. Tulipata neti za mbu pekee.
Rais na baraza na taasisi waliishia kwenda nje. Nakuomba ubadilike. Mshauri vizuri mama. Najua anashaurika na akitulia ni kiongozi na Rais mzuri.
, lakini sio 70%. Hata 5% haifiki. Gdp (per capita) Kenya wako juu- $4500+, nafasi ya21, wakati Tz ni $2700 nafasi ya 32 barani Africa. Ukiambiwa wameendelea kuliko sisi, ndio maana yake hatakama hutaki.Wakenya wameendelea nini ? Wana uchumi wa kati sawa nasi. Uchumi wao unatawaliwa na wachache. Ardhi inamilikiwa na wachache. Huku familia ya Kenyatta ikimiliki asilimia karibu 70 ya hyo nchi.
Nyerere hakuwa kuitetemekea. Na kunawakati alifunga mipaka. Eti Kenya wameendelea. Hujui Kenya.
OOooh, Kenya walishatangulia?Siku zote lazima ujifunze kwa waliotangulia. Kenya walishatangulia. Lazima tuangalie njia walizopita.
Wacha uongo. Ingekuwa tarakimu ndiyo hizo, asingekuwa kwenye Lower Middle Income, kama ilivyo Tanzania. Tofauti ya namba hizo kati ya Tanzania na Kenya sio kubwa kiasi hicho.Kenya wako juu- $4500+
Sijapata kusikia taifa lolote lililoendelezwa na watu wengine wenyeji wao wekiwepowepo tu kama masanamu.anacho jaribu kuwakilisha muandishi ni kwamba tusiwe tegemezi. tujikwamue kwa jituhada zetu
Nimezipenda hizo aya.Mtamsema vibaya na kumtukana Magufuli lkn nchi nyingi zilimtambua kuwa alisimama kwa masilahi mapana ya Tanzania. Hata Mkapa hakuwa na siasa za kubembeleza mataifa ya nje.
Magufuli alikuwa mkorofi na mbabe. Lakini Tanzania iliheshimika. Hakuongea kiingereza lkn hotuba zake zilifatiliwa dunia nzima kusikia nini atasema. UN wenyewe walikubali kuwa alikuwa mtu aliependa Taifa lake na Afrika.
Nje ya nini, ya Tanzania ?Nipo zangu nje naendelea na maisha yangu.
Ushaliwa kichwa wwHuyu mtoa mada inabd apimwe akili , Tabia za umaskini jeuri kama wa jiwe
OOooh, Kenya walishatangulia?
Tangulia kwenda wapi?
Wewe unaona Kenya wameendelea? Kwa akili za tope namna hii tutapata shida sana.
So hiyo kwako ndo kuendelea, Marekani inakipato cha juu kuliko Scandinavia. Lakini Marekani kuna maskini wa kutupwa. Unapoongelea uchumi ni kitu kipana. Na Scandinavian countries zinaongoza kwa huduma za kijamii na uwezi kuta umasikini kama uliopo Marekani japo Marekani inakipato kikubwa.Ni kweli familia ya Kenyatta wanamiliki ardhi kubwa
, lakini sio 70%. Hata 5% haifiki. Gdp (per capita) Kenya wako juu- $4500+, nafasi ya21, wakati Tz ni $2700 nafasi ya 32 barani Africa. Ukiambiwa wameendelea kuliko sisi, ndio maana yake hatakama hutaki.
Siyo peke yako uliyewahi kuishi huko, kama kweli uliwahi kukaa huko.Mkuu Hongera kwa post ndefu nimesoma yote kwa umakini. Mimi binafsi nimeishi sana Kenya na kuna baadhi ya kozi nimesoma huko, Kenya wako juu sana kwenye mambo mengi, raia kujitambua,seriousness, bidii na uwajibikaji, professionalism, mfano wengi wanaofundisha lugha ya kiswahili nchi za Ulaya ni wa Kenya kwa sababu wao wanachukulia lugha ya kiswahili kama lugha ya biashara wakati sisi watu wamelala wanalalamika, ukienda Nairobi leo hii ukiangalia utembeaji wa watu tuu utangundua kwamba tunatakiwa tujifunze kutoka kwao,shule nyingi za binafsi Tanzania wakenya wamejaa na Tanzania hatutaki kujifunza chochote kutoka kwao kwa sababu ya kuamini kuwa kujifunza kutoka kwa mtu ni kujipendekeza. Tulichowazidi wakenya ni ukarimu na Ukubwa wa eneo la nchi vingine wametuzidi sana.